Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Jeep rubicon

JF-Expert Member
Jan 7, 2023
738
1,439
Hello Africans.

Hakuna binadamu ninaowadharau kama wanaoamini mauchawi na mauganga.

Huwa nawaona ni watu wenye kasoro kubwa kichwani na wameoza kiasi kwamba hata uwaambie nini huwezi kuwabadili imani.

Hizi imani pumbavu zinaonesha vile Africans tuko na IQ ndogo. Na ndio maana pamoja na utajiri uliopo ktk hili bara tunateseka na shida karne kwa karne huku wenzetu wasioamini haya maujinga wakituacha mbali kwa maendeleo. (Najua kuna wazungu wachache vichaa pia wanaamin ushirikina).

Ukweli hizi imani zinanikera sana maana mbali ya kuchelewesha maendeleo ya hili bara pia ni hatari. Tushaua sana wenzetu wasio na hatia sbb ya hizi imani pumbavu. Albino, Vipara, wazee with red ayes na wengine wengi.Upumbavu mtupu.

Mimi binafsi nilishahama sehemu kwa kusingiziwa eti mimi ni freemason. Nilifanya kosa nikaporomosha hekalu wanakoishi wajinga. Mjengo wetu uko tofaut by far na nyumba zingine zote.

Wale wapuuzi walishindwa kujua kuwa kufanikiwa hakuna uchawi bali janja janja na timing kwenye fursa, basi yenyewe yakajiongoza eti hapa ni masonic na makafara tu.

Mwanzoni niliwapuuza ila badae kuna kitu ilitokea nikaona hawa wapuuzi kuna siku wanaweza wakajiunga wakanichoma mle ndani wakiamin mie natoa damu za watu kafara.Ikabidi niondoke.

Yupo mfanyakazi wangu alinichana Live kuwa "boss najua huwez kutoa siri zako ila siwez amini umefika hapa ulipofika bila ndumba kuhusika"

Mimi siamini kama kuna mtu yeyote anayeweza fanya kitu digits zangu bank zikaongezeka. Siku zote ninaamini katika kutumia akili ktk kutafuta.

Pia siamini kama kuna mjinga yeyote anayeweza kuniloga kitu kibaya kikanipata sbb havifanyi kazi. Mnadanganywa tu.

UCHAWI NA UGANGA NI UONGO havipo na havifanyi kazi. Mpo wengi humu mnaoamini hayo matakataka sasa nawapeni ofa ya 25M kwa atakayeweza kuniloga.

Nifanyeni chochote kibaya na mhakikishe hamnisamehi mpaka nije hapa niandike uzi wa kuomba msamaha na kukiri kuwa kweli uchawi upo nimelogwa na pia nilipe hiyo 25M kwa mchawi wangu.

Mkitaka niwatukane babu na bibi zenu wanaoogopwa kwa uchawi ili hasira ziwapande mniloge vizuri semeni. Nitawavurumishia mitusi hao babu/bibi zenu hamjapata kuona. Nitawatukana na kuwakashifu ma hawatanifanya chochote wajinga hao😂

Haya kazi kwenu.

NILOGENI

UPDATE:Mnaotaka jina ili mniloge siwezi kuwapa sbb ua Privacy ila nawawekeeni picha yangu muitumie kuniloga. Kateni mikono,vidole,nifanyeni niwe na miguu 4 kama ng'ombe vyovyote.

Screenshot_20230504-121424.jpg
 
Kuna jamaa wana maduka ya vifaa vya ujenzi,wamewekeana hadi mipaka ya kumwaga hzo dawa zao

Mmoja akiona tu siku hyo hauzi,anachukua dawa hata kama ni mchana anaanza kumwagilizia

Uchawi upo na unafanya kazi,ukiona kitu kinafatwa na watu wengi usizan ni wajinga ujue kuna kitu wanapata

Zamani nilitaka kuamini kuwa kwenye hz dini ukiristo na uislamu watu wanapoteza tu muda lakin siyo kwel kuna nguvu zipo huko na zinasaidia watu
 
Unakuta mtu na elimu yake anaenda kwa mganga aliyeishia darasa la 7 ili apewe dawa ya utajiri,wakati huyo mganga mwenyewe ni choka mbaya,anaishia tu Kukuagiza Jogoo kisha analifanya supu na kula na wanae huku wewe ukisubiri utajiri uje kimiujiza!

:D:D
 
Kuna jamaa wana maduka ya vifaa vya ujenzi,wamewekeana hadi mipaka ya kumwaga hzo dawa zao

Mmoja akiona tu siku hyo hauzi,anachukua dawa hata kama ni mchana anaanza kumwagilizia

Uchawi upo na unafanya kazi,ukiona kitu kinafatwa na watu wengi usizan ni wajinga ujue kuna kitu wanapata

Zamani nilitaka kuamini kuwa kwenye hz dini ukiristo na uislamu watu wanapoteza tu muda lakin siyo kwel kuna nguvu zipo huko na zinasaidia watu
Mpaka nilogwe ndo nitaamin la sivyo usijisumbue kunielewesha ujinga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom