Atakayeiponya CCM itaiangamiza Tanzania!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atakayeiponya CCM itaiangamiza Tanzania!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Oct 12, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama kuna kitu kinakera ni kuona watu wakitaka CCM iwe Manusura wa kimbunga cha mabadiliko ya kisiasa na kijamii kinachovuma nchini. Watu hao bila kujijua au kwa makusudi au kwa kusukumwa na hofu zao dhidi ya mabadiliko wamekuwa wakihimiza CCM ijerekebishe au wakitaka CCM isimamishe mgombea "anayefaa" kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  kila CCM ikichagua viongozi wanaoonekana kuwa "wabovu" au hawafai utasikia watu hao wakilalamika ni kwa nini CCM imeendelea kuchagua viongozi wabovu wasiofaa. Na kila mara huwataka wale walio "wasafi" watoke CCM na kujiunga na M4C kama vile hawaoni faida kwa taswira inayopatikana kwa watu hao kubaki, CCM kwani wanajenga taswira kwamba watu safi hawatakiwi ndani ya chama hicho hivyo kuvipa faida ya kuaminiwa vyama vingine.

  Mtu yeyote anayesikitika kwa kufa kwa CCM basi ajue hasikitiki kwa kufa kwa Tanzania. Ili Tanzania iwe salama ni lazima CCM itoke madarakani na ili CCM itoke madarakani ni lazima iwe dhaifu na ili iwe dhaifu ni lazima iongozwe na viongozi wabovu wala na watoa rushwa, Mafisadi na vibaraka wa mfumo wa Ubepari uchwara. Anayetaka CCM iwe Imara haitakii mema Tanzania!!
   
 2. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Hongera Kigarama,

  Your analysis is simple, inclusive and to the point.
   
 3. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Umeiweka vizuri sana mkuu! Nakuunga mkono, lazima ccm ing'oke, ife ndio izaliwe upya na kufuata misingi.
   
 4. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada ebu tusaidie kwa hili, kama Dsm ni mji mkuu wenye wasomi wengi na watu wenye upeo wa kuona maovu ya ccm na access ya information nyingi za kisiasa, kuzidi hata watu wa vijijini, lakini ccm hiyohiyo imeendelea kuongoza majimbo mengi ktk jiji hilohilo la dsm kwa % kubwa kuzidi wapinzani kwa chaguzi za miaka yote! Je kuna kipya kitakacho wazuia kuendelea kushika dola?
   
 5. n

  ndoleha Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo la msingi kwa Dar ni hao wasomi na watu wenye upeo mkubwa hawapigi kura kwa sababu tu wanaona ccm wataiba tu kura na kushinda hivyo bora tu usishiriki. Kama tunataka mabadiliko ya kweli, ni wakati sasa kutumia haki yako ya kupiga kura kwa sisi wote kujitokeza kwa wingi kupiga kura anzia ngazi za mtaa mpaka uchaguzi mkuu.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Improvement is impossible without a change!!!!
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kigarama,

  Hongera kwa mada nzuri; nilivyokuelewa ni kwamba CCM now is beyond repair, lakini pia, infection iliyoingia CCM, chama kingine kitakachoipokea, kina chanjo dhidi ya hiyo infection; Je nipo sawa katika haya mawili?
   
 8. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hebu nizungumzie Manzese Kwa Mfuga Mbwa ninakokufahamu zaidi. Dar ni sehemu ambayo kwa sehemu kubwa sana wakazi wake wameruhusiwa kuishi kwa kuvunja sheria. viwanja havijapimwa, wanaofanya biashara hawalipi Kodi, sehemu kubwa wanaishi kwa "misheni tauni" kwa ujumla wana darisalamu ndiyo wanaofaidika kwa mfumo huu mbovu tunaotaka kuuondoa.

  Hebu nenda Bandarini Dar uone ni watu wangapi wanafaidika kwa hujuma zinazofanyika Bandarini pale, Dar kuna NGO na ofisi ngapi za mifukoni? Jamii ya namna hii ukiiambia kwamba unataka kuubadilisha mfumo unaowapa wao nafasi ya "kutajirika" hawakuelewi. Viwanja vilivyoporwa na CCM vinawatajirisha wangapi kwa miradi inayoendeshwa kwenye viwanja hivyo??

  Ukitaka CHADEMA ipendwe Dar ni lazima kundi hilo la watu wanaofaidika na mfumo huu mbovu wahakikishiwe usalama wao. Nani anataka kuwahakikishia usalama huo? Richmond, IPTL, RADAR,EPA, na madudu mengine mengi ni dili za wana darisalama!!
   
 9. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuiponya CCM ni kuiua Tanzania!
   
 10. S

  SUPERXAVERY Member

  #10
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wachafu na waroho wa madaraka tunawatema kutoka ccm na wengi wamehamia upinzani, hicho ndio kifo chenu wapinzani hususani cdm. Hongera sana kwa kutupokea hiyo mizigoz
   
 11. mtumishidc

  mtumishidc JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 488
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hakika wezi na wanaofaidika hawapo tayari kuyaruhusu mabadiliko chanya!
  lakini je CDM itakuja kutibu haya yote?
  je mabadiliko yatahusisha ccm to cdm ama kutoka ubovu kuelekea ubora na je ubora huo upo cdm ama miongoni mwetu wananchi? yatupasa tuwaongoze watanzania watafakari mustakabali wao sasa kwa ajili yaliyobora yajayo!
   
 12. mtumishidc

  mtumishidc JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 488
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ahsante kwa kutembea nami fikrani!na huo ni moja ya udhaifu wa vyama vyetu mbadala,yatupsa tujipange ili taifa lipite hapa salama
   
 13. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Uko sawa kabisa Mchambuzi. CCM kwa sasa hakuna mwenye uwezo wa kuirudisha kwenye mstari lakini pia ni kweli chama chochote kitakachoipokea CCM ni lazima kirithi chembechembe za uovu uliopo.

  Hata sasa ndani ya CHADEMA kuna chembechembe za tabia hizi za uovu kwani na wanachedema nao wanatoka kwenye jamii hii hii iliyojaa uovu. Ndiyo maana sisi wengine tukiona hata kikikosa kidogo kinatendwa na CHADEMA tunakuwa wakali kwani kwa CCM uovu huo umehalalishwa kwa CHADEMA hatutaki kifike huko!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Manager

  Manager JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CCM haiponyeki, na inakufa, ili Tanganyika izaliwe ikiwa na uongozi adilifu wa CDM
   
 15. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Nadhani ujio wa chadema ni jambo jema sana kwa wananchi, lakini CCM isipotee kwani kikibakia chama kimoja chenye nguvu, tutarudi kule kule kwenye BORA UTAWALA badala ya UTAWALA BORA; Ni jukumu la Chadema sasa kuzidi kujiimarisha katika eneo hilo ili wakifanikiwa kuingia Ikulu, wananchi waweze kukipima vizuri dhidi ya CCM; Lakini kwa vile muundo uliopo wa utumishi, vyombo vya dola n.k ni vya ki-ccm, Chadema inahitaji alliance na taasisi zote hizi za umma kuanzia mapema kabisa, vingonevyo utawala wa Chadema utavurugwa sana na pengine usifike 2020 iwapo itashinda 2015;
   
 16. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mchambuzi hoja hapa si kuifanya CCM ife kabisa lakini tunataka CCM iwe dhaifu ili ishindwe mwaka 2015, na hututaki udhaifu huo uzaliwe ndani ya CCM yenyewe bali tunataka uzaliwe kutokana na uimara wa vyama vya upinzani. Kwa hiyo tutapingana na yeyote yule anayetaka kwa hila au kwa bahati mbaya avidhoofishe vyama vya upinzani.

  Hata mimi sipendi CHADEMA ije kuwa na nguvu kama walizonazo CCM hivi sasa. Sitaki wabunge wa CHADEMA wawe 70% au zaidi bungeni kwani na wenyewe wataingia kwenye ule mtego wa "tulitakalo huwa" mtego ambao unaimaliza CCM taratibu. Ili bunge letu liwe na afya ni lazima vyama vigawane idadi ya wabunge kwa uwiano usiopishana sana.

  Kuna watu ndani ya CHADEMA wanaendesha ubabe (Mbowe si mmojawao) dhidi ya vyombo vya dola na watumishi wa Serikali. Ni lazima tukubali kwamba hata iweje hawa watumishi waliopo ndiyo watatumiwa na CHADEMA kama watashinda mwaka 2015, kwa hiyo vita yetu kubwa ni lazima iwe ni kubadili mitizamo yao na wala si kuwaonesha kwamba wao si lolote si chochote.

  Kwenye Uchaguzi wa mwaka 2010 vituo vingi vilivyokuwa kwenye maeneo ya Makambi ya Jeshi viliongoza kwa kuwapa kura nyingi wagombea wa CHADEMA dhidi ya wale wa CCM. Lakini leo hii wanasiasa lukuki wakisimama kwenye Majukwaa huwashutumu Polisi kama ni vibaraka waliotopea wa CCM. Wanalinda "mtaji" au wanakula "mtaji"?
   
 17. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  Na kuiponya Tanzania ni kuiua ccm pia
   
 18. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini pia hata huko vijijini, Kiongozi mmoja mwandamizi wa ccm aliwahi kusema ccm inahazina kubwa ya wanachama wengi na wapiga kura kule vijijini, ambayo ndio sababu kubwa ya chadema kuanza mikakati ya kupanua wigo wa wanachama wake hukohuko vijijini. Kama mwenyewe umekiri mijimikubwa kama Dsm pagumu kwa mabadiliko (cdm) na vijijini nako bado hapajasomeka .Je matumaini yatatoka wapi?
  Najua ccm hawana tena nia wala mikakati ya kuleta mabadiliko kwa wananchi, wamebakiwa na mbinu ya Ku attack upinzani kwa mbinu zote na wanazo resource zote.narudia tena bado matumaini kwa CDM yanasafari ngumu sana.
   
 19. M

  Mr jokes and serious Member

  #19
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Itakufa 2 mana nimeshanza kuamini kuwa ccm inakufa nina ushuda kitaani kwetu watu wanaizunguzia vibaya sana ccm,isitoshe mama yangu ameanza kuelewa da ulikuwa umwambii kitu kuhusu ccm lakini sikuizi ana niulizia ata mambo ya cdm nikasikia wanaongea na mzee mwezake wa jirani yetu haa safari jamani 2nataka mabaadiliko,tafakali ni wangapi kama wazee hawa tanzania hii.tumechoka.
   
 20. M

  MKALIMOTTO Senior Member

  #20
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtaichonganisha sana ccm na wananchi kwa kuua polisi, waandishi wa habari na wauza magazeti lakini ukweli utaja julikana tu.
   
Loading...