Atakachotupa Obama katika muhula wake wa pili

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,067
Reaction score
1,328
BARACK Hussein Obama alipochaguliwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Marekani 2008 dunia nzima ilisisimkwa. Sisi wazawa wa Afrika pamoja na wenzetu waliozaliwa ughaibuni lakini wenye asili zitokazo bara hili tulisisimkwa zaidi ya wote. Kuna waliolia na kuna waliotokwa tu na machozi.
Sote tulifurahi kumuona mtu anayefanana nasi kachaguliwa kuliongoza taifa lililo na nguvu kushinda yote duniani. Hilo lilikuwa tukio kubwa. Kwa mara ya mwanzo Marekani ilimchagua rais na amiri jeshi asiye mzungu kuliongoza taifa ambalo kwa karne kadhaa limekuwa likimuona mtu mweusi kuwa si kitu.
Sisi wa Afrika ya Mashariki tulizidi kushangilia kwa vile baba wa Rais mpya wa Marekani alikuwa Mkenya. Ni baba yake wala si babu wa babu wa babu yake. Zaidi ya Uafrika wake Rais huyo wa Marekani alizaliwa na baba aliyekuwa Mwislamu na babu aliyekuwa mswalihina.
Kuchaguliwa kwa Obama kuliwakashifu wengi Tanzania ambao bado hawako tayari kumkubali Mtanzania mwenzao awaongoze ikiwa ana hata tone la damu ya kigeni.
Ugonjwa huu uko Bara na Visiwani ambako karibuni tuliwasikia viongozi wa CCM wakieneza siasa za chuki za kikabila. Walitamka waziwazi kwamba wenzao waliochanganya damu hawafai kuaminiwa. Kilichoshtusha ni kukiona chama chao kikikaa kimya bila ya hata kuwakemea.
Katika kampeni zake za kuugombea urais mara ya mwanzo Obama aliahidi mengi kwa masikini wa Marekani ambao wengi wao ni wenye asili ya Afrika.
Baada ya Obama kuupata urais tabaka hilo la Wamarekani halikupata afuweni yoyote. Hali za masikini wa rangi zote zilizidi kudidimia kama zilivyodidimia hali za Wamarekani wengine, isipokuwa labda za wale walio miongoni mwa asilimia moja ya Wamarekani ambao ni matajiri kupita kiasi.
Kuhusu Afrika muhula wa kwanza wa Obama ulituvunja moyo. Obama alionyesha kama halijali bara la asili yake. Mbali na kuitembelea Misri ambako alizungumzia zaidi masuala ya Mashariki ya Kati, Obama aliizuru Ghana Julai 2009. Alitoa hotuba iliyojaa ahadi tele. Kwa ufupi, aliahidi kuwa Marekani italisaidia bara la Afrika lijipatie ufanisi kwa kuondosha utawala mbovu.
Ahadi hiyo hakuitimiza. Badala yake Obama amekuwa akishikiriana zaidi na wenye kuongoza tawala mbovu — mbovu ama kwa sababu zinaikiuka miiko ya kidemokrasia au kwa sababu zinavumilia ufisadi.
Tarehe 14 Juni 2012 Obama alitia saini waraka uitwao “Mkakati wa Marekani Kuhusu Afrika Kusini Mwa Sahara.” Hakuna lililo jipya katika ‘mkakati’ huo. Ni yayo kwa yayo maji ya futi kwa nyayo. Mambo manne yalitiliwa mkazo: kuimarisha demokrasia Afrika; kulikuza kiuchumi bara la Afrika kwa biashara na uwekezaji; amani na usalama; na fursa na maendeleo.
Hakuna lililo jipya katika hayo kwa sababu Marekani imekuwa ikiyapigia ngoma miaka na miaka. Na hakuna hata moja kati ya hayo lililoinufaisha Afrika kiasi cha mtu kusema: “Ama kwa hili Marekani imeifanyia jambo Afrika.” Tunaweza kusema hivyo kuhusu China lakini si kuhusu Marekani ya Obama.
Kuna wasemao kwamba Obama kwa makusudi alilipuuza bara la Afrika katika muhula wake wa kwanza asije akalaumiwa kwamba amelishughulikia bara la babake badala ya kuwashughulikia masikini wa Marekani.
Wenye kuamini hivyo wanahoji kwamba kwa vile huu muhula wake wa sasa ndio wa mwisho basi labda atakuwa na ujasiri wa kuyashughulikia masuala yote hayo.
Tunaloweza kulisema kwa uhakika ni kwamba katika muhula wake wa pili utaoanza rasmi atapoapishwa tarehe 20 mwezi huu Obama atazidi kulitumbukiza bara la Afrika katika vita. Hilo ndilo suala kuu litaloongoza sera yake kuhusu Afrika.
Usalama na vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa umempa Obama kisingizio cha kupeleka majeshi katika nchi mbalimbali za Kiafrika. Wakati huohuo Wizara yake ya Ulinzi (Pentagon) imekuwa ikiunda mtandao wa kijasusi unaozilenga nchi za Kiafrika na za Mashariki ya Kati. Inasemekana mtandao huo utakuwa mkubwa kushinda ule wa Idara ya Ujasusi ya Marekani (CIA).
Kuna wanaoshukuru kwamba Balozi Susan Rice hatokuwa tena waziri wa mambo ya nje. Ingawa angetaka Afrika ishughulikiwe zaidi hata hivyo misimamo yake kuhusu nchi kadhaa za Kiafrika, kwa mfano Sudan, ingetatiza mambo. Inavyoelekea ni kwamba seneta John Kerry ndiye atayekuwa waziri mpya wa mambo ya nje akimrithi Hillary Clinton.
Kerry hana uzoefu mkubwa kuhusu Afrika ingawa mkewe amezaliwa Msumbiji. Hata hivyo, pengine yeye atakuwa na msimamo mzuri kushinda Rice. Huenda waziri wake msaidizi kuhusu Afrika akawa Michele Gavin, Balozi wa Marekani nchini Botswana. Zamani akifanya kazi katika Senate alikokuwa msaidizi wa Seneta Russ Feingold.
Mtu aliye karibu zaidi na Obama kuhusu Afrika ni Johnnie Carson, waziri mdogo wa Afrika. Lakini sidhani kama Carson ataweza kumsaidia Obama kwa vile nafikiri huenda akastaafu karibuni.
Wengine wanaoweza kuwa na ushawishi kwa Obama kuhusu Afrika ni watumishi wa zamani katika utawala wa Rais Bill Clinton kama vile Gayle Smith mkurugenzi mkuu katika Baraza la Usalama wa Kitaifa na John Prendergast maarufu kwa kampeni zake kuhusu Sudan, magaidi wa Lord’s Resistance Army na Congo-Kinshasa.
Nje ya serikali kuna watu kadhaa wataoendelea kuwa na ushawishi juu ya sera ya Afrika. Miongoni mwao ni John Peter Pham mwenye siasa za mrengo wa chama cha Republican. Pham anaongoza kitengo cha Afrika katika taasisi ya Atlantic Council na huenda akawa miongoni mwa wataomshadidia Obama azidi kuingilia kijeshi Afrika.
Kwenye taasisi nyingine zisizo za kiserikali kuna Jennifer Cooke mkurugenzi wa Afrika katika Center for Strategic and International Studies (CSIS) na Balozi John Campbell wa Council on Foreign Relations.
Katika taasisi ya Brookings Institution kuna wataalamu wawili wa masuala ya Afrika: Dakta Mwangi Kimenya (aliyezaliwa Kenya) na Witney Schneidman waziri mdogo wa zamani wa Afrika. Wote hao watasikilizwa na wapangaji wa sera ya Afrika ya Obama katika muhula wake wa pili.

Source : Raia Mwema - Atakachotupa Obama katika muhula wake wa pili
 
kama viongoz wa africa awawez kusaidia wananchi wake,wametanguliza ufisadi mbele,basi usitegemee misaada ya marekan kuwafikia wananchi usika,pia itakuwa vibaya kumlaumu obama wakat marekan inatoa misaada mingi tu kwa africa tatizo ni viongoz wetu wa africa namna wanavyotumia hizo pesa
 
Mbali yalioandika katika gazeti kuna mengi ya kujifunza kwa waandishi wetu wa habari wa Tanzania toka kwa uandishishi wa Ahmed Rajabu. Nawakilisha
BARACK Hussein Obama alipochaguliwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Marekani 2008 dunia nzima ilisisimkwa. Sisi wazawa wa Afrika pamoja na wenzetu waliozaliwa ughaibuni lakini wenye asili zitokazo bara hili tulisisimkwa zaidi ya wote. Kuna waliolia na kuna waliotokwa tu na machozi.
Sote tulifurahi kumuona mtu anayefanana nasi kachaguliwa kuliongoza taifa lililo na nguvu kushinda yote duniani. Hilo lilikuwa tukio kubwa. Kwa mara ya mwanzo Marekani ilimchagua rais na amiri jeshi asiye mzungu kuliongoza taifa ambalo kwa karne kadhaa limekuwa likimuona mtu mweusi kuwa si kitu.
Sisi wa Afrika ya Mashariki tulizidi kushangilia kwa vile baba wa Rais mpya wa Marekani alikuwa Mkenya. Ni baba yake wala si babu wa babu wa babu yake. Zaidi ya Uafrika wake Rais huyo wa Marekani alizaliwa na baba aliyekuwa Mwislamu na babu aliyekuwa mswalihina.
Kuchaguliwa kwa Obama kuliwakashifu wengi Tanzania ambao bado hawako tayari kumkubali Mtanzania mwenzao awaongoze ikiwa ana hata tone la damu ya kigeni.
Ugonjwa huu uko Bara na Visiwani ambako karibuni tuliwasikia viongozi wa CCM wakieneza siasa za chuki za kikabila. Walitamka waziwazi kwamba wenzao waliochanganya damu hawafai kuaminiwa. Kilichoshtusha ni kukiona chama chao kikikaa kimya bila ya hata kuwakemea.
Katika kampeni zake za kuugombea urais mara ya mwanzo Obama aliahidi mengi kwa masikini wa Marekani ambao wengi wao ni wenye asili ya Afrika.
Baada ya Obama kuupata urais tabaka hilo la Wamarekani halikupata afuweni yoyote. Hali za masikini wa rangi zote zilizidi kudidimia kama zilivyodidimia hali za Wamarekani wengine, isipokuwa labda za wale walio miongoni mwa asilimia moja ya Wamarekani ambao ni matajiri kupita kiasi.
Kuhusu Afrika muhula wa kwanza wa Obama ulituvunja moyo. Obama alionyesha kama halijali bara la asili yake. Mbali na kuitembelea Misri ambako alizungumzia zaidi masuala ya Mashariki ya Kati, Obama aliizuru Ghana Julai 2009. Alitoa hotuba iliyojaa ahadi tele. Kwa ufupi, aliahidi kuwa Marekani italisaidia bara la Afrika lijipatie ufanisi kwa kuondosha utawala mbovu.
Ahadi hiyo hakuitimiza. Badala yake Obama amekuwa akishikiriana zaidi na wenye kuongoza tawala mbovu - mbovu ama kwa sababu zinaikiuka miiko ya kidemokrasia au kwa sababu zinavumilia ufisadi.
Tarehe 14 Juni 2012 Obama alitia saini waraka uitwao "Mkakati wa Marekani Kuhusu Afrika Kusini Mwa Sahara." Hakuna lililo jipya katika ‘mkakati' huo. Ni yayo kwa yayo maji ya futi kwa nyayo. Mambo manne yalitiliwa mkazo: kuimarisha demokrasia Afrika; kulikuza kiuchumi bara la Afrika kwa biashara na uwekezaji; amani na usalama; na fursa na maendeleo.
Hakuna lililo jipya katika hayo kwa sababu Marekani imekuwa ikiyapigia ngoma miaka na miaka. Na hakuna hata moja kati ya hayo lililoinufaisha Afrika kiasi cha mtu kusema: "Ama kwa hili Marekani imeifanyia jambo Afrika." Tunaweza kusema hivyo kuhusu China lakini si kuhusu Marekani ya Obama.
Kuna wasemao kwamba Obama kwa makusudi alilipuuza bara la Afrika katika muhula wake wa kwanza asije akalaumiwa kwamba amelishughulikia bara la babake badala ya kuwashughulikia masikini wa Marekani.
Wenye kuamini hivyo wanahoji kwamba kwa vile huu muhula wake wa sasa ndio wa mwisho basi labda atakuwa na ujasiri wa kuyashughulikia masuala yote hayo.
Tunaloweza kulisema kwa uhakika ni kwamba katika muhula wake wa pili utaoanza rasmi atapoapishwa tarehe 20 mwezi huu Obama atazidi kulitumbukiza bara la Afrika katika vita. Hilo ndilo suala kuu litaloongoza sera yake kuhusu Afrika.
Usalama na vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa umempa Obama kisingizio cha kupeleka majeshi katika nchi mbalimbali za Kiafrika. Wakati huohuo Wizara yake ya Ulinzi (Pentagon) imekuwa ikiunda mtandao wa kijasusi unaozilenga nchi za Kiafrika na za Mashariki ya Kati. Inasemekana mtandao huo utakuwa mkubwa kushinda ule wa Idara ya Ujasusi ya Marekani (CIA).
Kuna wanaoshukuru kwamba Balozi Susan Rice hatokuwa tena waziri wa mambo ya nje. Ingawa angetaka Afrika ishughulikiwe zaidi hata hivyo misimamo yake kuhusu nchi kadhaa za Kiafrika, kwa mfano Sudan, ingetatiza mambo. Inavyoelekea ni kwamba seneta John Kerry ndiye atayekuwa waziri mpya wa mambo ya nje akimrithi Hillary Clinton.
Kerry hana uzoefu mkubwa kuhusu Afrika ingawa mkewe amezaliwa Msumbiji. Hata hivyo, pengine yeye atakuwa na msimamo mzuri kushinda Rice. Huenda waziri wake msaidizi kuhusu Afrika akawa Michele Gavin, Balozi wa Marekani nchini Botswana. Zamani akifanya kazi katika Senate alikokuwa msaidizi wa Seneta Russ Feingold.
Mtu aliye karibu zaidi na Obama kuhusu Afrika ni Johnnie Carson, waziri mdogo wa Afrika. Lakini sidhani kama Carson ataweza kumsaidia Obama kwa vile nafikiri huenda akastaafu karibuni.
Wengine wanaoweza kuwa na ushawishi kwa Obama kuhusu Afrika ni watumishi wa zamani katika utawala wa Rais Bill Clinton kama vile Gayle Smith mkurugenzi mkuu katika Baraza la Usalama wa Kitaifa na John Prendergast maarufu kwa kampeni zake kuhusu Sudan, magaidi wa Lord's Resistance Army na Congo-Kinshasa.
Nje ya serikali kuna watu kadhaa wataoendelea kuwa na ushawishi juu ya sera ya Afrika. Miongoni mwao ni John Peter Pham mwenye siasa za mrengo wa chama cha Republican. Pham anaongoza kitengo cha Afrika katika taasisi ya Atlantic Council na huenda akawa miongoni mwa wataomshadidia Obama azidi kuingilia kijeshi Afrika.
Kwenye taasisi nyingine zisizo za kiserikali kuna Jennifer Cooke mkurugenzi wa Afrika katika Center for Strategic and International Studies (CSIS) na Balozi John Campbell wa Council on Foreign Relations.
Katika taasisi ya Brookings Institution kuna wataalamu wawili wa masuala ya Afrika: Dakta Mwangi Kimenya (aliyezaliwa Kenya) na Witney Schneidman waziri mdogo wa zamani wa Afrika. Wote hao watasikilizwa na wapangaji wa sera ya Afrika ya Obama katika muhula wake wa pili.

Source : Raia Mwema - Atakachotupa Obama katika muhula wake wa pili
 
Koffi Annan alisaidia nini?rose migiro ? Obama shangazi yake zituni yupo Kwenye government housing hata makaratasi Hana .George Bush alim grant zituni green card kumtoa aibu Obama .Obama hajali ndugu zake wa damu atajali Africa.Obama alikuwa anaenda kenya sasa hivi forget it.Waafrica ndio tulivyo" Mungu alivyoandika urithi waafrica walisahaulika
 
Mungu hajasahau waafrika wote LABDA kama unauhakika amekusahau wewe BASI utujulishe ili tukuombee akukumbuke
Koffi Annan alisaidia nini?rose migiro ? Obama shangazi yake zituni yupo Kwenye government housing hata makaratasi Hana .George Bush alim grant zituni green card kumtoa aibu Obama .Obama hajali ndugu zake wa damu atajali Africa.Obama alikuwa anaenda kenya sasa hivi forget it.Waafrica ndio tulivyo" Mungu alivyoandika urithi waafrica walisahaulika
 
  • Thanks
Reactions: kui

Anachofanya Obama na US gvt ni kuzidisha mtandao wa magaidi ili apate kisingizio kizuri cha kujikita kijeshi Afrika.
Lengo kudhibiti rasilimali za Afrika na kujaribu kudhibiti ushawishi wa China.

Baada ya NATO na US kumyeyusha Gaddafi, Afrika imekuwa Tambarare na wamepata utelezi, wanaingia wanapotaka na wanavyotaka.

Waafrika tutaambulia migogoro, vita na vifo tu. Waafrika wachache, watoto wa mjini watapata 10%.

Kuna utabiri huu kwa US link PressTV - US dollar to collapse in 2013: Economist
 
Mzalendo interesting post Atachotupa Obama, I have two thoughts 1: I think what we(Africans? for this matter) should expect from him is,.. nothing really much 😱hwell:
UNLESS the World Economy gets better, I dont think we should expect much. He got in power in such challenging times for the whole World and everybody expected a LOT from him, US viewed him as their messiah who could fulfill their dreams of hope/change and the world viewed him as their open door through the most powerful country in the World, unfortunately very little happened from all those expectations due to this duct taped world economy.
2. We might have a chance since that, this's his last term and he's free if not ready to take risks because he doesnt have to worry about getting re-elected, he can do things he wanted to do in his first term but didnt have a chance to do them(and may be African issues) And also, this's the time to strengthen his legacy so may be tutakumbukwa when he's trying to work on that. All in all we need to put our acts together instead of waiting for the fat cats to help us.
 
BARACK Hussein Obama alipochaguliwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Marekani 2008 dunia nzima ilisisimkwa. Sisi wazawa wa Afrika pamoja na wenzetu waliozaliwa ughaibuni lakini wenye asili zitokazo bara hili tulisisimkwa zaidi ya wote. Kuna waliolia na kuna waliotokwa tu na machozi.
Sote tulifurahi kumuona mtu anayefanana nasi kachaguliwa kuliongoza taifa lililo na nguvu kushinda yote duniani. Hilo lilikuwa tukio kubwa.

Source : Raia Mwema - Atakachotupa Obama katika muhula wake wa pili
He should speak for himself
 
Waafrica wanatakiwa kujisaidia wenyewe na si vinginevyo. Acheni mawazo ya kutegemea serikali za nje ama watu wa nje ya Africa waisaidie Africa. Africa itajengwa ama kubomolewa na waafrica wenyewe. Obama is American president na sio messiah wa kuikomboa Africa. Kama mlitegemea Obama will save Africa basi mmeumia ama mmekwisha!
 
Back
Top Bottom