Ataka Mkapa na Kikwete Wafutiwe Kinga ya Kutokushitakiwa, Wapandishwe Kizimbani- Renatus Mkinga

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,681
119,317
Wanabodi

Watch Star TV Live saa hizi, Mwanaharakati Renatus Mkinga yuko Live Star TV asubuhi hii amesema watuhumiwa wakuu nambari moja kwenye sheria mbovu sio waliotunga bali waliopitisha, hivyo watuhumiwa wakuu ni Rais Mkapa na Rais Kikwete.

Ametoa wito kwa rais Magufuli kuifuta Kinga ya marais wastaafu hawa Wafutiwe Kinga ya Kutokushitakiwa, wawe ndio watu wa kwanza kupandishwa Kizimbani kwa nini waliridhia sheria hizi mbovu na kuzipa baraka zitumike? .

Endelea kufuatilia.

Paskali
 
Thubutu. Huyuhuyu aliyesema atawalinda?! Hao hao waliompigania na kumpikia ushidni dhidi ya mamvi?!

Inatafutwa kick tu ya kubuy time kwenye awamu ya viwanda ili ifike 2019 mwaka wa bajeti waanze kutoa 50mln kila kata then 2020 kila kijiji iwe rushwa ya uchaguzi!!!!
 
Kwa sababu ya watu hao wawil, hapa ndipo vita hii inaposhindwa na hata hao wengine waiotajwa watapona kwa sababu ya vichwa hivi viwili. Usicheze na mabepari
 
Vinginevyo tuendelee kuiombea Ardhi ya nchi iitwayo Tanzania I we na amani hadi tutakapowaondoa kupitia sanduku la kura ili kuweka [HASHTAG]#Strong[/HASHTAG] Institution!

Kumtegemea mtu mmoja kutengenza Nchi yetu ni kujidanganya labda kama hajawahi kuhusika.
 

Attachments

  • PhotoGrid_1492887665712.png
    PhotoGrid_1492887665712.png
    217.7 KB · Views: 38
Na ndiyo makosa makubwa anayoyafanya mh Rais.Tatizo kubwa mh Rais anachukua maamuzi ila kuna maamuzi magumu zaidi Rais anatakiwa achukue hatua.Kwa mfano kuwakamata mara moja watuhumiwa wa mikataba mibovu pamoja na kuseize mali zao,hii iendane na ku enact sheria kali za kunyonga hadharani ili iwe fundisho.Rais asiangalie majina au vyeo atoe tamko wakamatwe wote kama wanalindwa na katiba ibadilishwe sasa hivi.
 
Kwa Makosa haya yaliyotajwa siyo ya kuanza na watu Wa chini .

Kwa maoni yangu hata wale waliopitisha sheria ya gesi na mafuta bungeni mwaka Jana saa tano usiku Wanapaswa kushughulikiwa !

Eti wakamwambia Johnn Mnyika document zake kuhusu rasilimali za taifa ni za kufungia vitumbua !

sijasahau mpaka leo !
Hao hao Mnyika akiwakumbusha watamwita Dalali
 
Mbona ripoti hazijawataja Rais Mkapa na Rais Kikwete!
Kwa hiyo na wewe unawatetea!???
Nyinyi ndo mnatusumbua kwa maamuzi yenu ya hovyo katika maswala ya msingi. Sasa hivi kila mtu analalamika eti Acacia wametuibia. Acacia hawajaiba ila nyinyi CCM ndo mmewapa sandakarawe malu zetu.
Mwizi wetu ni nyinyi wazee wa 10% na NDIYOOOOO
 
Back
Top Bottom