Atafia mikononi mwangu

Atafia mikononi mwangu

Dr.

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2014
Posts
217
Reaction score
193
Mimi ni Daktari wa hospitali moja kubwa binafsi hapa Dar es salaam mzaliwa wa kanda ya ziwa na huu ni mwaka wangu wa pili kazini. Nilikua na rafiki yangu sana ambae sasa ni marehemu. Huyu rafiki yangu tulipendana sana kwa vile tulikua majirani na hata wazazi wetu walikua marafiki pia. Tulisoma wote shule ya msingi hadi A level mkoani Mtwara.

Baada ya kumaliza kidato cha sita sote tulifaulu vizuri na kubahatika kujiunga na masomo ya elimu ya juu hapa hapa Dar kusomea udaktari. Tukiwa mwaka wa kwanza rafiki yangu alibadilika sana na alinishtua sana aliponiambia kua ameamua kuhairisha masomo amepata kazi kwenye kampuni ya kuuza magari. Nilimshauri na kumsihi aendelee na masomo lakini hakubadilisha uamuzi wake.

Alianza kusafiri sana nje ya nchi, mara Afrika kusini, India, China, Brazil, Marekani n.k. Nilienda kuishi nae kwake baada ya kupanga nyumba nzima. Alinipeleka chuo kwa gari lake na kunirejesha kila alipopata nafasi. Niliishi maisha mazuri kiasi ingawa ilikua siri nyumbani hawakujua kama rafiki yangu alisitisha masomo. Skuwahi kupajua anapofanya kazi, kila nilipomwambia anipeleke hakukubali.

Sku moja usiku wa manane nikiwa mezani najisomea na yeye akiwa chumbani kwake alipigiwa sim na mtu ambae walijibizana sana huku kaka akisistiza kua amechoka kusafirisha dawa za kulevya anaacha. Niliogopa sana, niliondoka taratibu na kwenda kulala chumbani kwangu ili asigundue kua namsikiliza. Skupata usingizi kabisa. Asbuhi alionekana mwenye mawazo na hasira nyingi tofauti na siku zote. Nilimuuliza kulikoni akanambia ana mgogoro na bosi wake, nilmuuliza kwani huyo bosi anaishi hapa nchini akasema ndio na kunionesha picha yake kwenye sim.

Kama kawaida alinipeleka hadi chuo, aliponishusha na kuondoka nikachkua taksi na kuanza kulifuata gari lake kwa nyuma, Nilidhamiria kupajua anapofanyia hizo kazi zake. Sku hiyo ndio siku niliposhuhudia rafki yangu akipigwa risasi na mtu aliyekua amepakizwa kwenye pikipiki (Ni yule nilooneshwa na rafki yangu kwenye picha), na kufariki hapohapo. Baada ya kifo cha rafiki yangu yalitokea mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na mimi kuachishwa masomo kutokana na kua sehemu ya washukiwa, kuparaganyika kwa familia zetu n.k.

Usiku wa kuamkia leo hapa hospitalin ameletwa mtu yuleyule aliyemuua rafiki yangu na kusababisha misukosuko mingi katika maisha yangu akiwa hoi kwa presha ya kupnda. Sijawahi kufikiria kuua katika maisha yangu ila kwa sasa dhamira inanituma nimchome sindano ya sumu, nimtundike dripu ya glucose, nimuoverdose au ninyonge kabisa.

ENDELEA HAPA
 
usifanye lolote..usimpe dawa tu...mchunie kiaina..
 
Unataka kuubeba msalaba wa mwenzio? Huyo rafiki yako tamaa ndiyo ilimuua
 
Kumbuka kiapo chako cha udaktari...
Mtibu huyo mgonjwa...
 
sio vizuri kulipiza kisasi, wacha Mungu ammalize mwenyewe.....kemea hilo pepo la kuua
 
Dr dont do that please be good.. mtibu tu Mungu ndiye anayelipa kisasi mkuu itakusumbua zaidi maishani mwako ukimuua... let him go if possible ask someone else to take care of him usiwe karibu nae ... pole sana be good
 
Hata ukimuua rafikiyo hatarudi na kifo chake hakita undo yaliyokupata maishani.
Msamehe tu umtibu,hukumu yake atakutana nayo kwa aliyemuumba.
USIHUKUMU
 
Dah daktari think twice before you do something you will regret for the rest of your life,hata ukimuua huyo muhusika haitokupunguzia maumivu yoyote na wala haitomrejesha huyo rafikiyo…isitoshe huyo rafikiyo alikuwa na chaguo la kujihushisha na hizo biashara haramu au la….
Wewe si muuaji bali ni daktari,huna haki za kuhukumu wengine,wewe ni mtu mwema unaesaidia watu toa huduma yako kama unavyowatibu wagonjwa wingine au kama huwezi kufanya hivo msihi aende hospitali nyingine atibiwe wewe sio huyo muuaji,nafsi yako itakusuta maisha yako yote ww ukifanya jambo kinyume na sheria...huyo muuaji mungu atamhukumu!
 
Hapo alipo huwezi jua na hayo mabiashara yake na watu aliokwishaua au kuwasababishia mateso ni mangapi kashapitia. I mean huenda ni mtu anaeishi maisha magumu kuliko ufikiriavyo. Nakushauri umtibu kwa moyo wote na hakikisha anapona labda iwe nje ya uwezo ila usiache kumtibu ili apone aendelee kuteseka. Karma is a bitch believe me, huenda akaishi na akaja kushuhudia watoto wake mwenyewe wakiuawa na hutahusika kwa jinsi yoyote. So acha Mungu afanye take.
 
kama we n profesional dkt, nadhan course inayohs ethics za kaz yako ulifail ndo mana
unamawazo uchwara km hyo, Kwan unafanya hyo kaz ili ulipe visasi? Fungua milango ya kuwa fired hapo kazin uje uone kitaa bila job knavynukia ujambazi au kubeba madawa ya kulevya kupeleka uchna na brazil.,...
 
muaache bana mpe tiba sahihi kwani malipo ya dhambi ni mauti
 
Mimi ni Daktari wa hospitali moja kubwa binafsi hapa Dar es salaam mzaliwa wa kanda ya ziwa na huu ni mwaka wangu wa pili kazini. Nilikua na rafiki yangu sana ambae sasa ni marehemu. Huyu rafiki yangu tulipendana sana kwa vile tulikua majirani na hata wazazi wetu walikua marafiki pia. Tulisoma wote shule ya msingi hadi A level mkoani Mtwara.

Baada ya kumaliza kidato cha sita sote tulifaulu vizuri na kubahatika kujiunga na masomo ya elimu ya juu hapa hapa Dar kusomea udaktari. Tukiwa mwaka wa kwanza rafiki yangu alibadilika sana na alinishtua sana aliponiambia kua ameamua kuhairisha masomo amepata kazi kwenye kampuni ya kuuza magari. Nilimshauri na kumsihi aendelee na masomo lakini hakubadilisha uamuzi wake.

Alianza kusafiri sana nje ya nchi, mara Afrika kusini, India, China, Brazil, Marekani n.k. Nilienda kuishi nae kwake baada ya kupanga nyumba nzima. Alinipeleka chuo kwa gari lake na kunirejesha kila alipopata nafasi. Niliishi maisha mazuri kiasi ingawa ilikua siri nyumbani hawakujua kama rafiki yangu alisitisha masomo. Skuwahi kupajua anapofanya kazi, kila nilipomwambia anipeleke hakukubali.

Sku moja usiku wa manane nikiwa mezani najisomea na yeye akiwa chumbani kwake alipigiwa sim na mtu ambae walijibizana sana huku kaka akisistiza kua amechoka kusafirisha dawa za kulevya anaacha. Niliogopa sana, niliondoka taratibu na kwenda kulala chumbani kwangu ili asigundue kua namsikiliza. Skupata usingizi kabisa. Asbuhi alionekana mwenye mawazo na hasira nyingi tofauti na siku zote. Nilimuuliza kulikoni akanambia ana mgogoro na bosi wake, nilmuuliza kwani huyo bosi anaishi hapa nchini akasema ndio na kunionesha picha yake kwenye sim.

Kama kawaida alinipeleka hadi chuo, aliponishusha na kuondoka nikachkua taksi na kuanza kulifuata gari lake kwa nyuma, Nilidhamiria kupajua anapofanyia hizo kazi zake. Sku hiyo ndio siku niliposhuhudia rafki yangu akipigwa risasi na mtu aliyekua amepakizwa kwenye pikipiki (Ni yule nilooneshwa na rafki yangu kwenye picha), na kufariki hapohapo. Baada ya kifo cha rafiki yangu yalitokea mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na mimi kuachishwa masomo kutokana na kua sehemu ya washukiwa, kuparaganyika kwa familia zetu n.k.

Usiku wa kuamkia leo hapa hospitalin ameletwa mtu yuleyule aliyemuua rafiki yangu na kusababisha misukosuko mingi katika maisha yangu akiwa hoi kwa presha ya kupnda. Sijawahi kufikiria kuua katika maisha yangu ila kwa sasa dhamira inanituma nimchome sindano ya sumu, nimtundike dripu ya glucose, nimuoverdose au ninyonge kabisa.

You are unethical Dr, how can you end someone's life for personal matters? Look now you are in moral dilemma please treat that patient heartedly
 
Kama kweli ulipitia masomo ya Udaktari hadi mwisho, ukasoma na maadili ya Udaktari na leo uko hapo....... na una dhamiri ambayo iko hai. ....... Sina mchango!!!!!!
 
Back
Top Bottom