Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,403
Tofauti ya muda wa kupigwa picha hizi haizidi masaa 10. Picha ya kwanza, asubuhi tar.9 Sep 1990 akiwa Rais wa Liberia akielekea makao makuu ya vikosi vya ulinzi wa amani Afrika Magharibi (ECOMOG). Alikuwa akipokea mwaliko wa mkuu wa vikosi hivyo Jenerali Anold Quinoo aliyemuhakikishia ulinzi na usalama. Alijiamini lakini hakujua.
Picha ya pili, jioni tar.9 Sep 1990 akiwa chini ya ulinzi wa vikosi vya waasi vya INPFL. Vikosi hivi vya uasi vilipata taarifa ya ziara ya Rais, vikajipanga na kuvamia kambi ya ECOMOG na kumkamata Rais. Aliteswa sana. Alikatwa sikio, akakatwa uume, akafungwa kamba miguuni, halafu ikaning'inizwa kwenye gari na kuanza kuburuzwa mitaani. Mwili wake uliburuzwa mitaa ya Monrovia ukiwa umewekewa sigara mdomoni, huku raia wakishangilia.
Naam! Tofauti ya muda wa kupigwa picha hizi mbili haizidi masaa 10. Ni ushahidi wa wazi kuhusu mambo yanavyobadilika haraka, ni somo kwa walio tayari kujifunza.
Huyu ni Samuel Doe aliyekuwa Rais wa Libeira asiyejali utu wala ubinadamu. Aliteka waliomkosoa, akawatesa, akawaua. Alifunga jela wapinzani wake, alidiriki hata kuwateka na kuwapoteza viongozi wa dini. Miili wa watu iliokotwa katika fukwe za Buchanan na Monrovia ikiwa imeharibika vibaya na mingi haikutambulika. Ilidaiwa ni miili ya wale waliomkosoa. Alikua katili na alifurahia kuona wengine wakiteseka.
Aliingia madarakani kwa mapinduzi na mauaji, naye akatolewa kwa mapinduzi na kuuawa na vikosi vya Prince Johnson aliyekuwa mshirika wa Charles Taylor. Kikombe kilekile alichowanywesha raia wake ndio hichohicho alichokinywea.
Habari za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Liberia na Sierra Leone zinatisha sana. Hazipendezi. Lakini ni kumbusho kwa watawala wanaotesa na kusababisha maumivu makali kwa wengine. Wanaoua na kupoteza wengine. Wajue ya kwamba ipo siku utawala wao utatamatika. Kwa kupenda au bila kupenda. Ni lazima itokee. Ni asili.
Si sahihi kutoa hukumu ya mateso na kifo nje ya mfumo wa kimahakama, lakini baadhi ya watawala wanafanya hayo bila kujua wanaimarisha utamaduni wa kishetani. Na siku yakiwakuta, tutasema; wametumbukia shimo walilochimba wenyewe.