Aston Villa yamsajili John Terry

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,521
9,325
_96794050_terry2.jpg


Aston Villa wamemsajili aliyekuwa mchezaji wa Chelsea na nahodha wa timu ya Uingereza John Terry.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 36 ambaye kandarasi yake katika uwanja wa Stamford Bridge ilikuwa imekwisha mnamo tarehe 30 mwezi Juni ametia saini kandarasa ya mwaka mmoja na klabu hiyo ya ligi ya mabingwa.

Terry alisema kuwa alikataa maombi ya kuendelea kucheza katika ligi ya Uingereza ili kujipatia fedha zaidi kwa sababu hakutaka kucheza dhidi ya Chelsea.

Aliichezea Uingereza mara 78, akaichezea Chelsea mara 717 na kuweza kushinda taji la 5 la ligi ya Uingereza mwezi Mei.

Villa ilimaliza ya 13 katika ligi hiyo ya daraja la kwanza msimu uliopita lakini kikosi hicho cha Steve Bruce ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upato kupanda na kucheza katika ligi ya Uingereza ya msimu wa 2017-18.

Meneja wa Birmingham Harry Rednapp alisema mnamo mwezi Juni kwamba klabu yake ilikuwa imemtumia ombi Terry ambaye alitangaza mnamo mwezi Aprili kwamba ataondoka Chelsea.

Terry amechezea Chelsea na Nottingham forest ambayo alicheza kwa mkopo 2000.


chanzo
bbc swahili
 
Amejidhalilisha sana kwa heshima na rekodi yake sio wa kucheza daraja la kwanza bora angenda Hata Newcastle iliyopanda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom