Mzalendo_Mwandamizi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2007
- 1,116
- 4,773
Namfahamu vema Profesa Assad. Nilianza kusikia jina lake mwanzoni mwa miaka ya 1990s nilipokuwa Tanga kama mwalimu wa sekondari ya Eckenforde. Walimu wenzangu wawili - wote kwa sasa ni miongoni mwa wahasibu wabobezi - walikuwa wanafunzi wa Profesa Assad enzi hizo akiwa Dokta tu. Kwa mujibu wa maelezo yao, msomi huyo alikuwa kama mpishi wa wahasibu, na pengine tu hatuna utamaduni wa kuenzi mchango ya watu waliofanyia makubwa Taifa letu ndo maana mchango wa Prof Assad katika taaluma ya uhasibu hausikiki sana.
Lakini licha ya umahiri wake kitaaluma, Prof Assad ni mcha Mungu kweli kweli. Na hili in some way limemtemgenezea maadui kitambo. Mie ni Mkristo. Mkatoliki. Lakini pia ni mwanafunzi wa zamani wa Sosholojia ya Dini ambayo nilifundishwa na Dr Father John Sivalon, msomi ambaye thesis yake ya PhD inaeleza kwa undani kuhusu mahusiano ya dola na Kanisa, na kwa namna flani kutanabaisha "ubaguzi dhidi ya Waislamu."
Kadhalika, kuna "tafiti endelevu" ninayoifanya kuhusu mahusiano kati ya Dola na Waislamu Tanzania, na kuna findings zisizopendeza kuhusu Tanzania yetu. Hatupaswi kuyasema haya hadharani lakini ukiwa Muislam msomi kisha mcha Mungu, highly likely kutaambatana na label ya "mujahidina." Ni ubaguzi wa kidini usiozungumzwa hadharani kwa sababu sie ni wanafiki wazuri ambao, kwa mfano, hadharani twakemea ushoga ilhali mitandaoni mashoga wanaongoza kwa idadi ya followers (implying tunachosema hadharani sio tunachotenda faraghani).
Unafiki wetu unachangia sana kuzima mijadala ambayo siku ikilipuka inaweza kuwa na athari kubwa kwa mustakabali wa Taifa letu. Mijadala kama nafasi ya Uadilifu katika medani ya uongozi. It is this simple: kiongozi asiye mwadilifu kwa mkewe hawezi kuwa mwadilifu kwa taifa. Na kiongozi asiyeheshimu ndoa ya mteuliwa wake, hawezi kuheshimu haki za anaowaongoza. This is neither rocket science nor brain surgery.
Unafiki wetu unatuziba mdogo kuongelea ubaguzi wa kidini. Unafiki wetu unatuziba mdogo kuongelea wimbi hatari la ukanda na ukabila linalozidi kuchipuka tangu Jiwe ashike madaraka. Tunasubiri litokee la kutokea ndio tuanze mijadala ya kinafiki.
Na ni uadilifu na kinyume chake ndio hasa msingi wa hili sakata la Prof Assad vs Ndugai. Hawa ni watu wawili walio katika mizani tofauti kabisa. Wasifu wa Assad upo wazi kwa kila mmoja wetu kuufahamu. Mwanataaluma hiyo ni role model kwa Mtanzania yeyote yule, iwe kitaaluma au kiroho. Ikumbukwe kuwa sio rahisi sana kuwa "msomi sana" kisha "mshika dini sana" kwa sababu unfortunately usomi umeelemea katika facts ilhali dini imeelemea katika imani. So, kudos kwa msomi yeyote yule ambaye pia ni mcha Mungu, takes a lot of courage ku-negotiate usomi na dini.
Kwa Ndugai ni polar opposite ya Prof Assad. Nayajua maisha yake binafsi lakini hapa si mahala pale kuyaongelea. However, laiti sie tungekuwa sio wanafiki, leo hii Ndugai asingekuwa Bungeni, let alone kuwa Spika. We all know alichofanya kwa mpinzani wake wakati wa kampeni za ubunge. Laiti sheria ingefuata mkondo wake, huyu bwana angekuwa mahala anapostahili na si Bungeni wala kwenye wadhifa huo wa Uspika.
Tumeshusha threshold ya maadili kiasi kwamba ni poa tu kwa mtu aliyetenda alichotenda Ndugai kupewa wadhifa mkubwa kabisa kitaifa. Kimahesabu, Ndugai kama Spika anaweza kuwa Rais kwa mujibu wa Katiba yetu (Rais, Makamu, Jaji Mkuu, Spika).
Logically, kama Ndugai ali-behave namna hiyo alipokuwa Naibu Spika, what did we expect from him akiwa Spika kamili?
Moja ya mapungufu makubwa ya Ndugai ni short temper. Wanasema ana "anger management issues" ambazo japo wapo wanaoweza kutetea kuwa ni ubinadamu lakini si kila binadamu ni Spika. Moja ya sifa za uongozi hata uwe ukiranja tu let alone uspika ni kudhibiti hasira.
Kwa bahati mbaya suala hili litapita hivi hivi kama ambavyo suala la Bashite lilivyopita hivihivi. Kwa upande mmoja sie ni wepesi wa kukumbuka vitu vya ovyo ovyo lakini wagumu sana kukumbuka masuala muhimu kwa taifa letu. Angalia waliokuwa wakipiga kelele kuhusu Ben Saanane walivyomsahau. Angalia tukio la Lissu lilivyoachwa kuwa suala lake binafsi. Angalia unyama aliofanyiwa Lema na zaidi Sugu lakini jamii inaona poa tu. Angalia kilichojiri MKIRU lakini nobody gives a f*ck.
Sisi kama jamii ni chanzo muhimu cha haya mabaya yanayojiri katika nchi yetu. Tunasherehesha maovu. Tumekubali kuwa kutokuwa na maadili sio big deal lakini pindi dharau hiyo ikizua tatizo, twaanza kulalamika as if hatukujua kuwa "mzaha mzaha huzaa usaha."
Finally, no matter what happens kwa Prof Assad, kwa baadhi yetu anabaki kuwa moja la lulu adimu za taifa letu. Uadilifu wake unamfanya kuwa prone to attacks from watu wasio waadilifu. Ucha Mungu wake unamfanya atizamwe kwa jicho la hofu na "mfumo Katoliki" ambao ndo "umezaa" akina Jiwe, wanaseminari waliotengenezwa kutumikia Kanisa wakaishia kutumikia Taifa, ilhali deep in their beliefs kuna "conflicts za kiroho."
Sent using Jamii Forums mobile app