Askofu Zakaria Kakobe: Tanzania siyo nchi ya chama kimoja! Amtaka Rais Magufuli atubu

Mbunge wa wa Tarime John Heche amewaonya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuwa kama wanataka kumjibu Askofu Zacharia Kakobe kwa niaba ya serikali iliyopo madarakani basi wajibu kwa hoja na siyo kuropoka.

Heche amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa huo, Frank Kamugisha kumtaka Askofu Kakobe aende kufanya toba na kisha kuwaomba radhi wana CCM wa Dar es salaam kwa kuacha miiko ya kidini na kushindwa kutumia busara na kisha kusema hovyo.

Akizungumza jana na Wanahabari Kamugisha alivitaka vyombo vinavyohusika na sheria vihakikishe hakuna mtu anayepata fursa ya kumtukana au kumbeza Rais wa nchi na kufafanua kwamba Rais amejipambanua katika kuwasaidia wananchi na anafanya mambo hayo kwa udhati wa moyo wake hivyo mtu anyebeza moja kwa moja atakuwa msaliti.

Heche amandika kwenye ukurasa wake wa Twitter na kusema kwamba "CCM kama mnataka kujibu hoja za Askofu Kakobe kwa niaba ya Rais Magufuli na Serikali jibuni kwa hoja, sio kuropoka! kazi za wachungaji ni kukemea maovu yote yaliyopo duniani, watu wanapotea, wanapigwa risasi, wanaokotwa baharini, sheria za nchi hazifuatwi, haya yatakemewa na kila mtanzania" Heche.

Source eatv news.
KAKOSEA NJIA.

Na Thadei Ole Mushi.

[HASHTAG]#Mahubiri[/HASHTAG] ya jana ya sikukuu ya Christmass yalitanguliwa na Mkutano wa maaskofu ambao kwa pamoja walikubaliana kuweka agenda zinazofanana katika mahubiri yao. Huu ndio utaratibu wao na ndio maana kwa pamoja walizungumzia, amani ya nchi, Hali ya kisiasa, umoja na uchumi wa nchi.

[HASHTAG]#Hakuna[/HASHTAG] walipokubalia mtu akamshambulie mtu mwingine kwenye mimbari ya kanisa lake na sio utaratibu. Ubaya zaid unatumia story za vijiweni kutaja jina la mtu ambaye ndiye image ya nchi.

[HASHTAG]#Kufanya[/HASHTAG] hivyo ni kuaminisha jamii kuwa Rais wa nchi hafai na ni mdhambi na anapaswa kwenda kutubu. Ni ujasiri wa aina yake huu nimeuona. Hakuna kanisa linaloweza kufanya hivyo pale Urusi Kwa Valdimir na ndio maana Urusi inaendelea.

[HASHTAG]#Lazma[/HASHTAG] nchi iwe na one Chain of Comand si kila mtu anapaswa kutoa kauli. Hapa Askofu katugawa badala ya kutuunganisha kama wananchi.

[HASHTAG]#Taasisi[/HASHTAG] ya Urais ina hadhi yake haipaswi kutajwa tajwa kwa Tuhuma tu...... njia aliyotumia lazma aambiwe kuwa haifai. Hawezi kuachwa akashambulia tu mtu kwa tuhuma.

[HASHTAG]#Sijawahi[/HASHTAG] kusikia mahali katika mimbari ya Dini kasisi au Shekhe kumshambulia mtu wazi wazi kuwa ni Mdhambi hata Yesu hakufanya hivyo japokuwa alikuwa na uwezo wa kuona yaliyofichika. Hakuwahi kuhukumu moja kwa moja kuwa ni mdhambi wewe. Kwa hili mm binafai nakataa hakutumia njia iliyosahihi kufikisha ujumbe wake.

KILA ZAMA NA KITABU CHAKE.

Nani anaifahamu nadharia ya Hot Stove Rule ya McGregory.

Serikali ya JPM imeamua kutumia nadharia hii katika utekelezaji wa majukumu yake. Ni nadharia iliyopaswa na inayofaa sana kutumia na nchi kama Tanzania ambao watu wake wanataka kupiga Soga zaidi kuliko kazi.

INAFANYAJE KAZI.

Hii huhusika na kutoa mwongozo wa nini kitakupata kama utaweka mkono wako kwenye jiko la Stove linalowaka. Kama utavunja sheria zilizowekwa kwa kutumia nadharia hii adhabu utaipata katika mazingira yafuatayo.

1. Burns immediatelly:- Utachomwa haraka sana mara ushikapo jiko hilo. Na mhusika atatambua kuwa kachomwa kwa kuwa tu alilishika jiko hilo. Magufuli na serikali yake inavyokwenda hakuna subira hata kidogo. Nimeangalia kuanzia bungeni na nje ya bunge serikali hii haina muda wa majadiliano. Ukijichanganya wanakuchangamkia mara moja ni tofauti na ile ya mh Kikwete. Angalia hata wateule wake wanapokosea hakuna muda wa kusubiri kesi.......

2. Provides warning:- Ni kama ilivyo kwa jiko la stove kadri unavyosogeza mkono wako kuelekea kwenye jiko ndivyo hivyo joto huongezeka. Hii hutoa tahadhari kwa kitakachokukuta kama utaendelea kuusogeza mkono wako..........

3. Give Consistent punishment:- Hapa ni pale uhakika wa stove kurudia jambo lile lile kwa ufanisi ule ule. Kila ukishika utachomeka kwa kiwango kile kile bila kupunguza au kuongeza.Hii haitajalisha ni mara ngapi utakuwa umelishika jiko hilo. Ukishika mara moja utachomwa mara moja. Ukishika mara mbili utachomwa mara mbili na ukishika mara mia utachomwa mara mia.

4. Burn impersonally:- Kama jiko hili lilivyo litakuchoma bila kujua huyu ni nani. Moto wa jiko hauangalii huyu ni nani alimradi tu umejichanganya kuushika. Awe mtoto, mtu mzima, Askofu, Shekhe, Tajiri, Maskini au yeyote atachomwa tu kwa kadiri ya alivyoshika.

Ole Mushi.
0712702602
 
Namuunga mkono Heche. Sio kwamba nitamuunga mkono mtu yeyote, kwa cheo chake au hata kwa mdomo wake amtukane rais. Siungi mkono kabisaaaaa. Ila mngeweza kunionyesha matusi ya Kakobe nadhani ningeelewa. Jamani, tusiwe na kawaida ya kuongeza chumvi ili tu kuchajisha rais akasirike. Rais ni mtu ambaye Mungu kamjalia hekima tele hivyo mnatenda dhambi kumpotosha. Ana uwezo wa kuyatafakari maneno ayasikiayo. Msimsaidie kufikiri.
Tuna rais wa hovyo sana!
 
Okay hypothetically tuseme huyo bwana ametumwa au anatafuta kiki, vyovyote vile au sadaka but it is indeed what he claims is a somewhat naked truth only retards will repudiate that..
Hii lugha uliyoandika, baada ya maneno ya kiswahili, ni lugha gani? Ni maneno ya kiingereza lakini, yalivyopangwa hayaleti maana ya lugha yenyewe. Hypothetically? Yes hypothetically. Baada ya hypothesis unaleta conclusion! Hypothesis hufuatwa na uchunguzi wa ziada. Hypothesis huwekwa kwa sababu ya limited evidence. Huo ndo usomi.
Baada ya hayo, angalia ulichoandika ndo ujue unahitaji kuongeza miaka ya kukaa shuleni. Hujahitimu

Fella, logic doesn't play well with stupid people.
 
*ASKOFU KAKOBE AJIPE MUDA KUTAFAKARI .

Nimesoma mitandaoni maneno anayosadikiwa kuyasema kiongozi mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) lililopo Mwenge, Askofu Zakaria Kakobe akimsakama Rais Magufuli kwa maneno mazito na kumtaka atubu. Lahaula!

Nimebaki nikijiuliza kati ya Rais Magufuli na Askofu Kakobe nani anatakiwa atubu?!. *Askofu Kakobe anatakiwa aanze kutubu yeye* kwa sababu:-

1. Mwaka 1995 aliwaaminisha Watu kuwa Augustine Mrema atashinda urais na kuingia Ikulu. Kakobe alidai amepewa maono hayo lakini mwisho wa siku Mrema aliangushwa vibaya na Benjamin Mkapa akashinda urais. Kakobe ulishatubu juu ya hili?

2. Kakobe huyu huyu akaibuka tena 2015 akasema Mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa atashinda urais lakini akaishia kupata aibu nyingine ya Mgombea wake huyo kushindwa urais. Kakobe hakuwahi kutubu dhambi hii ya kuwadanganya Watanzania.

3. Kakobe aliwahi kuwaambia waumini wake umeme uliopita juu ya kanisa lake hautakaa ufanye kazi. Mpaka kesho umeme huo unafanya kazi. Kakobe alitakiwa aendelee kutubu tu kwa dhambi hii ya kuwadanganya mpaka waumini wake.

4. Kakobe huyu anayemvaa na kumrarua Rais Magufuli kwa maneno makali anatakiwa kuanza kutubu yeye maana ameshindwa kuheshimu mamlaka ya hapa Duniani wakati kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia Mwenyezi Mungu amewaagiza Wanadamu kuheshimu mamlaka za hapa Duniani na za Mbinguni lakini huyu anayejiita Askofu Kakobe ameshindwa kulitambua na kuheshimu hili. Kakobe nenda katubu kabisa kwa kushindwa hata kuheshimu mamlaka, kuitii Biblia na kuheshimu agizo la Mwenyezi Mungu.

5. Kakobe huyu huyu anatakiwa atubu kabisa kwa kuanza kuhubiri siasa kanisani tena Madhabahuni (sehemu takatifu) badala ya kuhubiri neno la Mungu, kuhubiri Biblia inasemaje na kumuhubiri Mwenyezi Mungu. Kitendo cha kutelekeza neno la Mungu na kuvaa uanasiasa si tu kuwagawa Waumini wake bali pia ni kutikisa misingi ya amani ambayo imejengwa kwa gharama kubwa za jasho, mateso na kujitoa kwingi kwa Waasisi wetu. Kakobe nenda katubu kwa uchochezi huu.

Askofu Kakobe alitakiwa ajipe muda wa kutosha wa kufikiri juu ya matendo yake na kauli zake kabla ya kuzitoa madhabauni. Alipaswa kujifunza faida na hasara zake.

Askofu Kakobe alitakiwa aendelee kujifunza juu ya mwelekeo wa Tanzania Mpya na mwelekeo wake Mpya kwa sasa. Tanzania mpya ya sasa inayoongozwa na Rais Magufuli haina muda wa siasa za chini ya Mwembe tena.

Kwa Wahubiri wanasiasa kama Kakobe watamuona Magufuli ni tatizo ila kwa Watanzania Wazalendo tunamuona Rais Magufuli ni Mkombozi kwa Taifa letu. Tunamuona Rais Magufuli ndiye Mussa wa Watanzania wetu kwa sasa anayetutoa Misri kwenye mateso, anatuvusha bahari ya Shamu na kutupeleka Kaanani, nchi ya Maziwa na Asali. Daima sisi Watanzania wanyonge tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli siku zote, nyakati zote.
Tulidhania kilaza Kamugisha Tu kumbe wengine wko huku Jf
 
Kwani ukiwa Rais ndio haukosei? no one is perfect under the sun. akikosea lazima asemwe.
Mi naamini kila mtu hukosea lakini, siyo kila anayekosea unayo madaraka ya kumkosoa au kumurekebisha. Mitaani kwetu kuna vibaka lakini sina madaraka ya kuwarekebisha au kuwapa kifungo.
Tatizo la Kakobe kajisahau kwamba madaraka aliyonayo ni ya pale, kwake, Mwenge. Tatizo amejiamini eti Mungu kamtuma kurekebisha hata rais wa nchi. Hiyo ni nonsense! Kuwinda sifa asizokuwa nazo.
 
Mimi sikujua kama Lowasa ni fisadi, ila nilipoaminishwa na ushahidi uliotolewa Na Lissu pamoja na mbowe kwenye media angalau ndipo nilianza kuamini,
Amini na hiki kuwa magufuli ni fisadi na dikteta amesema Lissu
 
Mimi sikujua kama Lowasa ni fisadi, ila nilipoaminishwa na ushahidi uliotolewa Na Lissu pamoja na mbowe kwenye media angalau ndipo nilianza kuamini,
Amini na hiki kuwa magufuli ni fisadi na dikteta amesema Lissu
 
Zakharia Kakobe ni Mrundi ambae Wazazi wale walihamia Kigoma kwa Njia haramu Miaka ya 1960 Uhamiaji wafuatilie tumechoka kuishi na Wahamiaji Haramu

Pili Huyu Ana kesi ya kukutwa na fuvu la Binadamu Kanisani kwake Mwenge wakati wa Jk lakin kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji wakati wa Kikwete aliachiwa huru bila ya kuhojiwa ipasavyo, Jeshi la Polisi chini ya Jemedari Simon Sirro ifufue huu upelelezi

Kakobe anatafuta kick Kama ya Gwajima kwa kuwa anajua Next Sunday Team Ufipa yote itahamia kwa Kakobe kusikiliza 'Mahubiri' baada ya Gwajima kupoa
Mkamateni akapimwe mkojo
 
# Nimekusiliza kwa makini Sana toka Jana na nimekua nikiirudia mara kwa mara clip yako ili nipate kujua Ulikua ukimaanisha nini. Katika kipande kile cha sauti nimekusikia ukilalamika kua raisi Magufuli hataki kushauliwa. Naomba nikuulize,Hivi unajua maana ya Ushauri? Naje unajua katiba inasema nini kuhusu Ushauri anao pewa raisi?

# Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Sura ya Tatu ya katiba inayoelezea haki na wajibu wa Raia, ibara ya 37 kifungu kidogo cha Kwanza kinasema na nitanukuu "37.-(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuataushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu paleanapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote."

# Nafikiri utakua umenielewa nini nilikusudia kusema, Kila mmoja anashauri kwa namna anavyoona yeye inafaa lakini rais anafuata katiba hivyo haruhusiwi wala halazimishwi eti kutembea kazi Ushauri wa mtu. Atafanya hivyo tu pale anapoona inafaa.

# Baba askofu unapaswa ujue maana ya Ushauri, Ushauri maana yake ni Mawazo ama mapendekezo anayo pewa mtu juu ya jambo fulani. Na mapendekezo hayo yaweza kukubaliwa ama kutaliwa, sasa yanapo kataliwa kwanini iwe nongwa?

# Baba askofu ukiisoma biblia vizuri katika kitabu cha injili ya Luka, Yesu alipo kua mlima sayuni akiomba na kulia huku jasho Kama matone ya damu yakitililika mpaka chini akiomba kwa Mungu kua,kama ikimpendeza amuepushie kikombe hiki cha Mateso lakini mapenzi ya Mungu ya timie na sio Ya kwake Yesu.

# Huu Ulikua ni Ushauri wake Yesu kwenda kwa Mungu, na Mungu alipo iona Hofu ndani yake alimtuma Malaika kuja kumtia moyo na yaliyoandikwa yakatimia.

# Hivyo baba askofu Kakobe Ushauri unaotolewa na watu mbali mbali usiufanye kua ati kwamba ni Lazima Raisi autekeleze.

# Hata wewe nakumbuka Ushauri uliopewa wa kuondoa kanisa hapo lilipo ulikataa na mpaka ukawavika T-shirt waumini wako kuiomba Tanesco Umuogope Mungu. Sasa kama wewe ulishindwa kufuata ushauri inakuaje iwe halali kwako kwa wengine iwe dhambi?

# Note Injili ya Luka Yesu anasema,mbona unakitazama kibanzi kilichomo katika jicho la nduguyo ilihali huoni boriti iliyo Katika jicho lako mwenyewe.

# Mnafiki wewe toa boriti katika jicho lako kisha uje utoe Kibanzi kwa nduguyo.
yaani nyie watu, mbona iq zenu ndogo sana kiasi hichoo?? umesikiliza vizuri audio ile ama umekurupuka tu!? ni wapi amesema hakubali kushaurika?

Vitu/hoja nilizozisikia ziko tatu tu:

1.Busara na hekima
2.Akitukanwa asiogope
3.Afuate sheria za nchi
 
Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuataushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu paleanapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote
kuzuia mikutano ya kisiasa ni kufuata katiba? tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom