Askofu: Viongozi wa dini acheni matanuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu: Viongozi wa dini acheni matanuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Jan 2, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  2nd January 12
  Askofu: Viongozi wa dini acheni matanuzi

  Waandishi Wetu
  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa, Dk. Owdenberg Mdegella, ameonya kuhusu hatari ya viongozi wa dini kupingana na wanaharakati katika vita ya kupunguza matumizi ya serikali kutokana na wao kugeuka vinara wa ununuzi wa magari ya kifahari.

  Amesema inashangaza kuona baadhi ya viongozi wa dini kununua na kutembelea magari ya kifahari huku wakijua yapo makundi ya yatima na watu maskini ambao wanahitaji misaada ya kijamii.

  Aliyasema hayo jana katika Kanisa Kuu la KKKT mjini Iringa wakati akitoa salamu za Mwaka Mpya katika ibada.

  "Kiongozi wa dini kununua gari la kifahari la zaidi ya Shilingi milioni 200 la nini, watu wetu hujiuliza shughuli yake hasa ni nini au la kufanyia nini...wanatafuta umaarufu eti na mimi niwe na gari," alisema huku akihoji Wakristo wanapata faida gani wakati yatima na watoto walio katika mazingira magumu wapo wanaombaomba vyakula bila msaada.

  Aidha, alisema hadhi ya uchungaji imeshuka na kwamba kanisa linachafuliwa na watheolojia pamoja na wachungaji ambao hawana huruma na kanisa.

  "Wapo wachungaji wanaodhani kwamba uchungaji ni kula kondoo badala ya kuchunga kondoo. Uchungaji umechakachuliwa na mwaka huu wa 2012 ni mwaka wa uchungaji," alisema.

  Kuhusu mustakabali wa taifa kwa sasa, Askofu Mdegella alisema ipo haja kwa madhehebu yote ya dini kuwa na jukwaa maalum la kuishauri serikali kuhusu mambo mbalimbali.

  Alisema kwa kufanya hivyo, kila upande utapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa mwenzake na kuisaidia serikali.

  ASKOFU MTEGA: TAIFA LIMGEUKIE MUNGU

  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, Norbeth Mtega, amelitaka taifa kumgeukia Mungu na kumfanya kuwa yeye ndiye muweza wa yote, badala ya watu kuamini kuwa wanaweza kufanya kila kitu bila Mungu.

  Askofu Mtega alitoa kauli hiyo jana wakati wa misa ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2012 iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba mjini Songea ambapo alisema jamii inapaswa kuwa na uoga wa Mungu na viongozi wa taifa wanapaswa kutambua uongozi ni fursa ya usimamizi kwa wengine ambao wamepewa na Mungu.

  Amesema viongozi wenye dhamana dhidi ya wananchi walio wengi wanapaswa kutambua kuwa uongozi ni dhamana waliopewa na Mungu kwa ajili ya walio wengi na jukumu lao ni pamoja na kusimamia rasilimali za nchi kwa ajili ya walio wengi, lakini baadhi ya viongozi badala ya kusimamia rasilimali hizo kwa ajili ya walio wengi, wao hujichukulia na kuzitumia kwa maslahi yao.

  Amesema kuwa taifa hivi sasa linaadhimisha miaka 50 ya uhuru na ikiwa taifa litampa Mungu kisogo na kudhani kuwa linaweza kufanya kila kitu bila kumtanguliza Mungu, upo uwezekano mkubwa wa amani iliyopo kutoweka kwa sababu ya kuzidi kukithiri kwa roho za ubinafsi za baadhi ya viongozi.

  Askofu Mtega alisema kuwa taifa na viongozi wake linapaswa kutambua kuwa ipo miiko ya Mungu na miiko ya viongozi na kuwa miiko yote hiyo ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa taifa lolote na inapopuuzwa madhara yake huwa ni makubwa kwa jamii na ni vyema kila anayekosea kukiri kwa ajili ya ustawi wa taifa lake.

  Amesema kuwa baadhi ya viongozi wanajengeka katika ubinafsi zaidi na kusahau kuwa wamepewa dhamana kwa ajili ya walio wengi na taifa linapaswa kukiri pale linapokosea.

  VIONGOZI WA DINI ACHENI KUILAUMU SERIKALI-RC  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, amewataka viongozi wa dini nchini kuacha kuilaumu serikali kuhusu ufisadi ambao unafanywa na viongozi, badala yake waiombee serikali isonge mbele.  Alitoa kauli hiyo jana wakati wa kutoa salamu zake za mwaka mpya kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la EAGT Siloam Ipagala mjini Dodoma.  Dk. Rehema alisema viongozi wa dini nchini wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanaliombea taifa ili liwe na viongozi waadilifu na si kuendelea kuilaumu.

  Alisema viongozi wa serikali wanamilikiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa dini hivyo hakuna sababu yoyote ya kuwafumbia macho watumishi ambao siyo waaminifu na badala yake wanatakiwa kuwakemea.  Alilitaka kanisa hilo kujenga tabia ya kujitegemea kwa kuwekeza katika kilimo na ufugaji ili kuondokana na tabia ya kuwa tegemezi.  Naye Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Evance Lucas, aliitaka serikali kukemea baadhi ya viongozi wa siasa wanaohubiri udini na ukabila.  "Sisi viongozi wa dini, hatutaki kusikia viongozi wa siasa wakihubiri masuala ya udini na ukabila kwa kufanya hivyo ni dalili za kutaka kuwapandikiza Watanzania tabia ambayo haikuwepo tangu kupatikana kwa Uhuru ambao ulitafutwa kwa hekima na busara za waasisi wa nchi," alisema Mchungaji Evance.  Alimtaka mkuu huyo wa mkoa kufikisha salamu za kanisa kwa viongozi wa kitaifa kuwa kanisa lina ushirikiano na vyama vyote vya siasa hivyo hakuna sababu yoyote ya kubagua na kuongeza kuwa yapo makanisa ambayo kwa sasa yanahubiri udini na ukabila.

  MCHAKATO WA KATIBA MPYA

  Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Njombe, Issa Mengele, amewataka Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa Katiba mpya kwa kuyajumuisha makundi maalumu wakiwemo walemavu katika utoaji wa maoni.

  Wito huo ulitolewa jana wakati wa ibada maalum ya mwaka mpya iliyofanyika katika kanisa hilo Usharika wa Songea.

  Askofu Mengele alisema kila Mtanzania anayo haki ya kushiriki na kuijadili Katiba iliyopo ambayo kwa sasa imeonekana kuwa ina mapungufu mengi hivyo kila mwananchi ni vyema ashiriki kuchangia mchakato wa Katiba kwa kuyaainisha mambo muhimu ambayo yanapaswa kuongezwa.

  Alieleza kuwa Watanzania ni lazima wafahamu haki yao ya msingi kwa kuwa wawekezaji wa nje kwa muda mrefu wamekuwa wakijishughulisha na uchimbaji wa madini ambayo ni rasilimali kubwa ya nchi na kwamba iko haja sasa mambo hayo yakawekwa bayana kwenye Katiba mpya kwani katika maeneo mengi ambayo yana madini, wawekezaji wamekuwa wakichimba madini na kuondoka nayo huku wakiwaachia wenyeji mashimo.

  Imeandikwa na Godfrey Mushi, Iringa, Jacquelina Massano, Dodoma na Nathan Mtega, Songea.

  NIPASHE

  NIPASHE  MY TAKE
  Hivi kuna kiongozi wa kanisa lets say KKT au RC au Anglican anayeendesha V8? au kanisa nalo limeingiliwa na serikali katika counter accusation shutuma za kanisa kuelekea serikali! Hii picha kali tusubiri...
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Who is Rehema chimbi?? naona anapenda sana media huyu mama..
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Shida yetu watanzania ndo hiyo, we can never take responsibilities hata kidogo, sasa hao waumini wenyewe kama wako kimya na matumizi makubwa ya hao viongozi wao wa dini hadi wasemewe na Askofu ambye hata si wa dhehebu lao.

  Na ontop of that hawatachukua hatua yoyote!

  Just kama ilivyo kwa viongozi wetu wa kisiasa, yani sisi wananchi tuko tuko tu hadi baadhi ya wabunge wanaolipwa posho kubwa wanaanza kuzipinga.

  Naamini hayo yalitakiwa yaanzishwe na wananchi wenyewe na si kusubiri kusemewa tu kila mara.

  Na hata kama akitokea mtu akawasemea wananchi, bado hawaoni kama ni suala muhimu, wanaona kama ni stories tu zitakazopita.

  Tanzani ni Taifa linalotia huruma kwa sana.
   
Loading...