Askofu Shoo: Watu waovu watambue kumuondoa Tundu Lissu mmoja kutazalisha Lissu wengine maelfu

Hongera kwa huyo Mhariri. Taifa letu linahitaji sana watu wenye kujitambua na wenye kutenda kazi/wajibu wao bila woga wala unafiki.
 
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo amewataka watu waovu watambue kumuondoa Tundu Lissu mmoja kutazalisha Lissu wengine maelfu.

Kauli ya Askofu Shoo inatokana na kuchukizwa na jaribio lililoshindwa la kumuua Lissu Alhamisi iliyopita mjini Dodoma, ambapo watu waliokuwa na silaha walishambulia gari lake kwa risasi 32.

Katika shambulizi hilo, kati ya risasi hizo 32 zilizofyatuliwa, risasi tano zilimpata Lissu maeneo mbalimbali ya mwili wake, na sasa anatibiwa katika hospitali ya Aghakhan ya Jijini Nairobi,Kenya.

Akizungumza kutoka Bonn Ujerumani leo , Askofu Shoo ametoa wito maalum kwa Serikali ya Rais John Magufuli, kuhakikisha wote waliohusika na unyama huo wanakamatwa.

“Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na taarifa za kupigwa risasi Mheshimiwa Tundu Lisu. Watanzania tunapaswa kukataa na kulaani kwa nguvu zote vitendo kama hivi,”amesema na kuongeza;-

“Mimi ninaamini kuwa nguvu zile zile za uovu zilizokuwepo tangu awamu zilizotangulia ndizo zinazoendeleza unyama kama huu. Ninamwomba Mungu ampe (Lissu) uponyaji wa haraka”.

“Tundu Lissu amekuwa mstari wa mbele kufunua ufisadi unaoendeshwa na wababe wachache. Hawa wanaona sasa wameanza kutikiswa, na kwa kuwa kwao wingi wa mali na pesa ndio mungu wao”

“Hatushangai wakitumia kila njia kuzuia ufisadi wao usianikwe hadharani. Watajaribu kila njia kuzuia ukweli lakini wanasahau kuwa ukweli hauzuiliki milele kuna siku utajitokeza tu”.

“Kumwondoa Lissu mmoja kutazalisha Lissu maelfu. Wito wangu kwa serikali ya Dr Magufuli ni huu, kwamba watu wote waliohusika wasakwe na wafikishwe mbele ya sheria,”.

Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT amesema Serikali yoyote makini inajua namna ya kuulinda upinzani kwani ukitumika vizuri unakuwa kioo cha serikali cha kujitazama.

Mara kadhaa, kiongozi huyo amekuwa akitoa hotuba zenye hisia kali akitaka Serikali na vyombo vyake vya usalama kuchukua hatua, kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ajabu ya kihalifu.


Mwananchi
 
Ona sasa malisu siku hizi yamekuwa kubaooooo.

Yani ni tume Sio huru,hakika Kwa hali iliyopo nawaambia ccm haiwezi pata kura hata 1000 kwny urais.
Taifa limegawanyika kabisa chanzo ni Fulani.

Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana
 
Ona sasa malisu siku hizi yamekuwa kubaooooo.

Yani ni tume Sio huru,hakika Kwa hali iliyopo nawaambia ccm haiwezi pata kura hata 1000 kwny urais.
Taifa limegawanyika kabisa chanzo ni Fulani.

Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana
Waliompiga Lisu walidhani wanatokomeza upinzani, badala yake wamezalisha akina Lisu kibao. Dawa ni kutenda haki na usawa kwa watu wote bila kuangalia hali, jinsia, ukanda, ukabila, udini na mengine yafananayo na hayo.
 
Back
Top Bottom