MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo amesema Mungu amemjalia Rais Magufuli roho ya kutokuwa na hofu katika utendaji kazi zake.
Askofu Shoo amesema hayo wakati Rais Magufuli alipojumuika na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro.
Huku akishangiliwa na mamia ya waumini ndani ya kanisa, Askofu Shoo alisema, ‘’Wewe kwa ujasiri kabisa umesema lazima tuyatumbue majipu kama tunataka kuendelea kama taifa’’.
Aliendelea kusema, ‘’Watanzania tulio na nia njema, Mhemishiwa Rais tunakuelewa na kukubali, sisi kanisa tunakuombea na tutaendelea kukuombea uzidi kuwa na ujasiri huo, tunazidi kukuombea kwa Mungu akupe afya njema na usiache kusimama katika lile la kweli kama mwenyewe unavyosema msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Endelea kuwa Mpenzi wa Mungu Mheshimiwa Magufuli’’.
Askofu alimalizia kwa kusema, ‘’Tunamuomba Mungu azidi kukupa washauri wema, washauri wasio na unafiki, wasio na hila na malengo ya kujinufaisha binafsi, washauri ambao wanajikomba komba lakini wakiwa na ajenda binafsi. Mungu akupe washauri wema Mheshimiwa Rais’’.

VIDEO: