Askofu: Serikali ya CCM ilikabidhiwa kwa mizimu wakati wa Uhuru na Nyerere

Katika kipindi cha Asubuhi cha cha jana ITV alialikwa Askofu wa kanisa Katoliki ambaye alinishangaza kwa jambo jipya.

Alisema wala tusishangae yanayo fanywa na serikali ya CCM ni matokeo ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa mashehe fulani wa Bagamoyo ambao walifanya tambiko ili Nchi ipate uhuru chini ya mwalimu Nyerere kwa kibali cha mizimu.

Kusema ukweli hata mimi niliwahi kumsikia Mwalimu akisema hao wazee walimwambia aruke shimo moja lililo fanyizwa dawa kisha akaambiwa mkoloni hakuwezi.

Sasa kwa mjibu wa mtumishi huyo wa Mungu anasema hata Uhuru ulipo patikana nchi ili kuwa chini ya laana kubwa kiasi kila jitihada zilikuwa zikienda mrama daima.

Yeye ansema ameoteshwa juzi tu kuhusu mkasa huo na kuambiwa Watanzania wasipotubu tuta kuwa tuna shuhudia viongozi wetu wakifanya vituko.

Aliongeza kuwa tabia ya mtu aliye laaniwa inajulikana anakuwa haelewi anafanya nini.Mkimlaumu atakuwa ana washangaa ninyi.

Anasema madudu yote ya CCM mathalani kutoa nguzo za umeme toka mafinga kupelekaKenya na kisha kurudisha Nchini kwa kununua kwa fedha za kigeni ni jambo linalo weza kufanywa na waliolaaniwa tu.

Chanzo: ITV
mlaaniwa anapoiongelea laana yake na jinsi ilivyopatikan!!! huu ushenzi kutoka kwa viongozi wa dini unapatikana tanzania tu.
yaani leo hii askofu wa kanisa katoliki LINALOENDESHA MCHAKATO WA KUMTANGAZA NYERERE KUWA MWENYE HERI NA HATIMAYE MTAKATIFU,leo hii anasimama na kusema eti NYERERE aliikabidhi nchi kwa mizimu ni aina nyingine ya uwendawazimu toka kwa viongozi wa dini walioshibishwa milungula toka kwa wanasiasa.
na ndio maana nina hakika hawa wapumbavu hawawezi kuuona ufalme wa mungu.
binafsi ntakapoingia kwenye ufalme wamungu halafu nikakuta mungu amemleta na huyo askofu, kwa kweli ntamwambia mungu ANITOE NA KUNIPELEKA MOTONI.
NGOJA NISIHARIBU SIKU YANGU
 
Askofu si akemee pepo la mizimuuu...ili taifa liondokane na laanaaa...

Hahaaa

Mkuu hapo ht ukikemea utakesha!
Laana haiondolewi hivyo!

Hapa ni kuomba toba na rehema!
Then tunavunja maagano yaliyowekwa!na sio kazi ndogo!
Kumbuka shetani ana uhalali kwasbb alikabidhiwa,kwahiyo huwezi kukemea kilicho na uhalali!
 
Askofu si akemee pepo la mizimuuu...ili taifa liondokane na laanaaa...

Hahaaa nimecheka
Mkuu hapo ht ukikemea utakesha!
Laana haiondolewi hivyo!

Hapa ni kuomba toba na rehema!
Then tunavunja maagano yaliyowekwa!na sio kazi ndogo!
Kumbuka shetani ana uhalali kwasbb alikabidhiwa,kwahiyo huwezi kukemea kilicho na uhalali!
 
Mnajimu Mkuu Afrika Mashariki na Kati alikuwa nani vile? Na alikuwa na nafasi gani katika dini vile? Sio masheikh wote ni wachawi lakini hapakosekani masheikh wachawi nadhani kama Nyerere alienda basi alienda kwa hawa.

Mnajimu ni mchawi? Wote wanaobashri nyota kwenye magazeti ya Ulaya ni wachawi?
 
Tz ukitaka uongoZi LA IMA ukaloge ukitaka kazi yenye kipato lazima ukaloge ukitaka kuanzisha kanisa au kuwa koongozi wa dini yeyote Tz LA IMA ukaloge tusimsingizie Nyerere uchawi na mitambiko niasili ya Tanzania makanisa mengi yamepoteza imani yaki ongoza na kanisa katoliki duniani
 
Afadhali Askofu kazindua wengi wasiofahamu hili. Hili jambo liko wazi, hii nchi ilikabidhiwa kwa mizimu siku ya uhuru chini ya uongozi wa ccm, ndio maana bila kuiondoa ccm madarakani nchi hii ni ngumu kuendelea pamoja na amani na rasilimali zilizopo. Duniani Mt.kilimanjaro inajulikana uko kenya, Tanzanite wauzaji wakubwa ni SA japo inachimbwa Tanzania. Hii sii laana kumbe ninini? Kama alivyoshauri Askofu, toba na rehema kwa Mungu ndio njia pekee ya kuondokana na laana hii.
 
Jitahidi kuficha upumbavu kidogo, inamaana Nyerere huyu huyu atakaetangazwa karibuni kua mtakatifu ndie aliyekua anaongoza hiyo mizimu au kulikua na raisi mwingine. Kanisa lina interijensia kubwa sana na haliwezi kumwita Mtakatifu mtu anaeshirikiana na mizimu.
 
Hii taarifa ina mashaka, mbona huyo Askofu wa kanisa katoliki aliyesema haya hatajwi?
 
Jitahidi kuficha upumbavu kidogo, inamaana Nyerere huyu huyu atakaetangazwa karibuni kua mtakatifu ndie aliyekua anaongoza hiyo mizimu au kulikua na raisi mwingine. Kanisa lina interijensia kubwa sana na haliwezi kumwita Mtakatifu mtu anaeshirikiana na mizimu.

Mpumbavu ni wewe uliyeko kwenye chungu. Uliambiwa nyerere alikuwa malaika? Au unafikiri kwa akili yako ndogo wote waliotangazwa watakatifu hawakuwahi kumwasi Mungu? Unamfagamu Paulo kipindi akiwa Saul? Jinga kabisa
 
Hivi kwa nini masheikh wakisoma dua mtu akafsnikiwa huwa inaitwa UCHAWI? Lakini mapadri na wachungaji wakifanya hivyo huwa inaonekana ni nguvu ya Mungu? Hii si propaganda ya kufanya uislamu uonekane ni dini ya mizimu kweli? Nina mashaka makubwa....labda faiza foxy
 
Last edited by a moderator:
Jitahidi kuficha upumbavu kidogo, inamaana Nyerere huyu huyu atakaetangazwa karibuni kua mtakatifu ndie aliyekua anaongoza hiyo mizimu au kulikua na raisi mwingine. Kanisa lina interijensia kubwa sana na haliwezi kumwita Mtakatifu mtu anaeshirikiana na mizimu.

Mkuu unafaham jinsi mwenge wa uhuru ulivyoanzishwa? Kama hujui tafuta humu humu JF ndo utaamini hii nchi inaendeshwa kwa imami za ajabu.
 
cha kwanza tungeanza na mwenge then vngne vnafata mwenge ndo movng monster we2 coz kuna v2 vnafanyika tanzania cdhan kama vnaweza kufanyika sehem yeyote dunian yan 2mekuwa wajnga sana naamini kwel 2merogwa c bure

By :
Huyu Forojo Ganze, alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo. Walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote (Mwl.Nyerere). Zindiko hilo lilifanyika bagamoyo ktk moja ya
mashimo yanayopatikana wilayani hapo.

Zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee. Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia ktk hilo shimo kwa ajili ya kuuliza. Alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar Es Salaam.

Kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi akiwakama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika. Wenzake wakiwa wanaongozwa naYahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar Es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa Kiswahili kasha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho. Baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani.

Baada ya hapo aliwagiza Yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115. Kama kawaida ya sheheYahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wamiaka
38,hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115, na hii ndivyo ilivyokuwa. Mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115).

Pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar Es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema. Mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa Bukoba jambo la kitaifa? Zindiko la Bagamoyo linafanya
kazi. Safu hii ilikuwa ya watu 5 ambao ni.

1. Mzee Ramadhan, alizaliwa mwaka 1920,
2. Ally Tarazo(1929),
3. Komwe wa Komwe(1918),
4. Sheihe Yahya Hussein(1925),na
5. Forojo Ganze (1902)
 
Katika kipindi cha Asubuhi cha cha jana ITV alialikwa Askofu wa kanisa Katoliki ambaye alinishangaza kwa jambo jipya.

Alisema wala tusishangae yanayo fanywa na serikali ya CCM ni matokeo ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa mashehe fulani wa Bagamoyo ambao walifanya tambiko ili Nchi ipate uhuru chini ya mwalimu Nyerere kwa kibali cha mizimu.

Kusema ukweli hata mimi niliwahi kumsikia Mwalimu akisema hao wazee walimwambia aruke shimo moja lililo fanyizwa dawa kisha akaambiwa mkoloni hakuwezi.

Sasa kwa mjibu wa mtumishi huyo wa Mungu anasema hata Uhuru ulipo patikana nchi ili kuwa chini ya laana kubwa kiasi kila jitihada zilikuwa zikienda mrama daima.

Yeye ansema ameoteshwa juzi tu kuhusu mkasa huo na kuambiwa Watanzania wasipotubu tuta kuwa tuna shuhudia viongozi wetu wakifanya vituko.

Aliongeza kuwa tabia ya mtu aliye laaniwa inajulikana anakuwa haelewi anafanya nini.Mkimlaumu atakuwa ana washangaa ninyi.

Anasema madudu yote ya CCM mathalani kutoa nguzo za umeme toka mafinga kupelekaKenya na kisha kurudisha Nchini kwa kununua kwa fedha za kigeni ni jambo linalo weza kufanywa na waliolaaniwa tu.

Chanzo: ITV
katika Uilamu hakuna tambiko wala baba yake tambiko, kuna kuomba dua tena kwa Mungu alie moja na sio kupitia kwa mizimu wala mtoto wa mizimu. Kwahiyo huyo askofu aseme kuwa huyo Nyerere ameenda kwa wachawi kupewa hio mizimu anayosema yeye
 
Back
Top Bottom