Askofu: Serikali ya CCM ilikabidhiwa kwa mizimu wakati wa Uhuru na Nyerere

Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
2,325
719
Katika kipindi cha Asubuhi cha cha jana ITV alialikwa Askofu wa kanisa Katoliki ambaye alinishangaza kwa jambo jipya.

Alisema wala tusishangae yanayo fanywa na serikali ya CCM ni matokeo ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa mashehe fulani wa Bagamoyo ambao walifanya tambiko ili Nchi ipate uhuru chini ya mwalimu Nyerere kwa kibali cha mizimu.

Kusema ukweli hata mimi niliwahi kumsikia Mwalimu akisema hao wazee walimwambia aruke shimo moja lililo fanyizwa dawa kisha akaambiwa mkoloni hakuwezi.

Sasa kwa mjibu wa mtumishi huyo wa Mungu anasema hata Uhuru ulipo patikana nchi ili kuwa chini ya laana kubwa kiasi kila jitihada zilikuwa zikienda mrama daima.

Yeye ansema ameoteshwa juzi tu kuhusu mkasa huo na kuambiwa Watanzania wasipotubu tuta kuwa tuna shuhudia viongozi wetu wakifanya vituko.

Aliongeza kuwa tabia ya mtu aliye laaniwa inajulikana anakuwa haelewi anafanya nini.Mkimlaumu atakuwa ana washangaa ninyi.

Anasema madudu yote ya CCM mathalani kutoa nguzo za umeme toka mafinga kupelekaKenya na kisha kurudisha Nchini kwa kununua kwa fedha za kigeni ni jambo linalo weza kufanywa na waliolaaniwa tu.

Chanzo: ITV
 
Laana inayoitafuna na kuliangamiza taifa la Tanzania ilisababishwa na matukio mawili.

1. Tukio la kwanza ni tambiko la Bagamoyo kati ya Nyerere na wachawi wa Bagamoyo

2. Tukio la pili ni zindiko la kichawi la kuzindika taifa la Tanganyika lililofanyika Lindi mara tu baada ya Uhuru
 
Kweli hapa kuna laana kubwa sana..!!

Haiwezekani kwa taifa lenye umri wa binadamu mzee (54) kushindwa kila kitu. Siasa imetushinda, Michezo imetushinda, Huduma za jamii zimetushinda, Wachungaji wanaandaliwa Kenya. Yaani sisi hatuna hata kitu kimoja cha kujivunia, Tulikuwa tunajivunia kama Taifa lenye Amani ulimwenguni, lakini sasa hata kwenye top 50 hatumo..!! Inashangaza sana..!!

Sasa huko kutubu anakosema Askofu, tukatubu kwa nani? Wapi? Kwa lipi? Kiukweli yaani Taifa limechanganyikiwa, Waganga wanajiona Wababe kwenye Taifa hili... Mashehe na Wachungaji wanajiona wababe kwenye Taifa hili, Wavutabangi na Wazinzi vilevile wajiona Wababe, Hawaambiliki hawashikiki..!!! yaani ikimradi vurugu tu Taifa halitawaliki wala Haliongozeki, Kila mmoja ni kiongozi..!!!

BACK TANGANYIKA
 
AH AH KINDLY MTUACHE WAISLAM NA WALA MSITUHUSISHE NA CCM aka HAWA LAAANA TULWAH, TAFADHALI TUSIHARIBIANE SWAUMU ZETU, CCM ILILAANIWA HATA KABLA HAIJAZALIWA TOKA TANU, NA WAISLAM HATUHUSIKI NA KWA LOLOTE NA HAWA CCM MBWA KOKO WEUSI
Nakusihi wewe kama wewe usijihi kuhusika kwa sababu mambo hayo yalifanyika huenda kabla hujazaliwa maana ni kabla ya Uhuru.Na wenyeji wa pwani wa wakati huo haikuwa kama ni dini bali ilikuwa kama matambiko ya kienyeji.
 
Katika kipindi cha Asubuhi cha cha jana ITV alialikwa Askofu wa kanisa Katoliki ambaye alinishangaza kwa jambo jipya.

Alisema wala tusishangae yanayo fanywa na serikali ya CCM ni matokeo ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa mashehe fulani wa Bagamoyo ambao walifanya tambiko ili Nchi ipate uhuru chini ya mwalimu Nyerere kwa kibali cha mizimu.

Kusema ukweli hata mimi niliwahi kumsikia Mwalimu akisema hao wazee walimwambia aruke shimo moja lililo fanyizwa dawa kisha akaambiwa mkoloni hakuwezi.

Sasa kwa mjibu wa mtumishi huyo wa Mungu anasema hata Uhuru ulipo patikana nchi ili kuwa chini ya laana kubwa kiasi kila jitihada zilikuwa zikienda mrama daima.

Yeye ansema ameoteshwa juzi tu kuhusu mkasa huo na kuambiwa Watanzania wasipotubu tuta kuwa tuna shuhudia viongozi wetu wakifanya vituko.

Aliongeza kuwa tabia ya mtu aliye laaniwa inajulikana anakuwa haelewi anafanya nini.Mkimlaumu atakuwa ana washangaa ninyi.

Anasema madudu yote ya CCM mathalani kutoa nguzo za umeme toka mafinga kupelekaKenya na kisha kurudisha Nchini kwa kununua kwa fedha za kigeni ni jambo linalo weza kufanywa na waliolaaniwa tu.

Chanzo: ITV
Watu pekee wanaoweza kuliweka Taifa hili katika misukosuko ya Udini ni hawa wachungaji na Masheikh kwa sababu kiongozi wa dini huwezi kutumikia chama bali kazi yako ni kuwahubiri neno la Mungu. Laana za Mwenyezi Mungu azijue nani? sisi kina nani wa kuhukumu watu wa Taifa zima wakati wewe unaishi humo humo. Kama kweli huyu Mchungaji ameweza kuoteshwa basi bora akimbie haraka asije kuwa kati ya wale waliolaaniwa..
 
Kweli hapa kuna laana kubwa sana..!!

Haiwezekani kwa taifa lenye umri wa binadamu mzee (54) kushindwa kila kitu. Siasa imetushinda, Michezo imetushinda, Huduma za jamii zimetushinda, Wachungaji wanaandaliwa Kenya. Yaani sisi hatuna hata kitu kimoja cha kujivunia, Tulikuwa tunajivunia kama Taifa lenye Amani ulimwenguni, lakini sasa hata kwenye top 50 hatumo..!! Inashangaza sana..!!

Sasa huko kutubu anakosema Askofu, tukatubu kwa nani? Wapi? Kwa lipi? Kiukweli yaani Taifa limechanganyikiwa, Waganga wanajiona Wababe kwenye Taifa hili... Mashehe na Wachungaji wanajiona wababe kwenye Taifa hili, Wavutabangi na Wazinzi vilevile wajiona Wababe, Hawaambiliki hawashikiki..!!! yaani ikimradi vurugu tu Taifa halitawaliki wala Haliongozeki, Kila mmoja ni kiongozi..!!!

BACK TANGANYIKA

yaani inasikitisha na inachekesha sana.....Tanzania? sijui tunakwenda wap
 
Watu pekee wanaoweza kuliweka Taifa hili katika misukosuko ya Udini ni hawa wachungaji na Masheikh kwa sababu kiongozi wa dini huwezi kutumikia chama bali kazi yako ni kuwahubiri neno la Mungu. Laana za Mwenyezi Mungu azijue nani? sisi kina nani wa kuhukumu watu wa Taifa zima wakati wewe unaishi humo humo. Kama kweli huyu Mchungaji ameweza kuoteshwa basi bora akimbie haraka asije kuwa kati ya wale waliolaaniwa..
Lakini mkuu kuna kila dalili ya laana hii.Kama umekuwa ukiangalia picha za nyakati za uhuru Kuna mganga mmoja anaonekana akiwa amevalia kiganga wakati wa kuapishwa kwa Mwalimu.Hata ngozi ya chui aliyo vaa mwalimu wakati wa kuachanganywa udongo wa Zanzibar na Tanganyika ni vitu vyenye ishara hizo hizo.Kwa watu mnao soma biblia mnajua tukio la nchi kupata uhuru halikumfurahisha Mungu kabisa jinsi lilivyo fanyika hata Mganga kuwa kama mgeni Rasimi,Aliitwa Chifu Matunge kitu kama hicho.
 
Watu pekee wanaoweza kuliweka Taifa hili katika misukosuko ya Udini ni hawa wachungaji na Masheikh kwa sababu kiongozi wa dini huwezi kutumikia chama bali kazi yako ni kuwahubiri neno la Mungu. Laana za Mwenyezi Mungu azijue nani? sisi kina nani wa kuhukumu watu wa Taifa zima wakati wewe unaishi humo humo. Kama kweli huyu Mchungaji ameweza kuoteshwa basi bora akimbie haraka asije kuwa kati ya wale waliolaaniwa..
Swadakta.. yeye kama mtumishi wa mungu amefanya nn kulisaidia taifa laaniwa? Au ndo mmoja wa "wasakatonge"?
 
Inawezekana watanzania tukaonekana tumerogwa na huo uchawi,je wamarekani wamerogwa na nani? Nchi yao ilianzishwa katika misingi ya dini tena ya kikristo,lakini sasa majimbo yote wameruhusu ndoa za jinsia moja!! Hivi wao na sisi nani karogwa zaidi?
 
Maaskofu wote waafrika washukuru sana mizimu iliyoleta uhuru kwa sababu iliwafukuza wazungu wote wakiwemo wazungu maaskofu ili waswahili ngozi nyeusi washike uaskofu kwenye makanisa yote .

Isingekuwa hiyo mizimu kufukuza wazungu huyo askofu mswahili angekuwa anaswalishwa na Askofu mzungu na angekuwa kazi yake kushika gauni la askofu mzungu kwenye altare.

Mizimu ndiyo imweezesha yeye kuwa askofu.Maaskofu wazungu waliondoka wakilia walipoambiwa fungeni virago muachie waswahili washike serikali,njia za uchumi na uongozi wa dini.
 
Halafu mkulu aliyepo akajazia na kitengo cha ulinzi wa majini ikulu chini ya marehemu. Bado kidogo tu tutaanza kusikia ya ikulu ya Malawi hapa Bongo. Bakora zitaanza kutembea magogoni.
 
Back
Top Bottom