Kanisa la KKKT halitakuwa salama kama litaendelea kuwavumilia viongozi wa kanisa na watendaji ambao wanatuhuma zisizovumilika ambazo haziendi sambamba na taratibu za Mungu . Moja ya viongozi wa Kanisa ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakituhumiwa na mambo yanayochafua huduma ya Bwana ni Askofu Mdegela ambaye ndiye Askofu wa Dayosisi ya Iringa. Pamoja na tuhuma zake kuwa za muda mrefu lakini uongozi wa KKKT umekuwa hauna la kufanya dhidi ya viongozi wa Dayosisi kutokana na udhaifu wa katiba ya KKKT ambayo pamoja na mapungufu mengi ya kimuundo lakini imeshindwa kurekebisha mapungufu hayo kiasi kuwa kwa muundo ulivyo wa KKKT Askofu Mkuu hana nguvu ya kumuwajibisha Askofu wa Dayosisi yoyote hata anapofanya makosa ya wazi ambayo yangehitaji kiongozi wa juu kuchukuwa hatua za kinidhamu kwa haraka.
Kwa mujibu wa gazeti la leo la Mwana halisi imeelezwa kuwa Askofu huyu ameundiwa Tume ya kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo kwa sisi tunaomfahamu Askofu huyu niza kweli na za muda mrefu lakini uongozi wa KKKT haukuwa na lakufanya kutokana na ukweli kuwa katiba ya KKKT haina kipengere kinachoeleza hatua kuchukuliwa kwa Askofu anayekwenda kinyume na taratibu za kanisa. Kinachofanyika sasa hivi ni mpaka waumini waanzishe chokochoko na vurugu ndipo KKKT hufanya mlolongo wa kuunda tume na baadaye kuitishwa kwa mkutano mkuu ili kujadili jambo husika na hatua kuchukuliwa. Askofu mdegela kwa muda mrefu amekuwa akituhumiwa kwa vitendo vya uzinzi, ufisadi na kutumia madaraka yake vibaya lakini bado aliendelea kuvumiliwa.
Kwa mujibu wa gazeti la mwanahalisi ambalo lilifuatilia sakata hili kwa karibu, askofu huyu ameundiwa tume inayoongozwa na Askofu Hance Mwakabana (Dayosisi ya kusini kati-makete), Askofu Dk. Martin shao - Dayosisi ya Kaskazini - Moshi) na Askofu Elisa Buberwa - Dayosisi ya Kaskazini Magharibi. Miongoni mwa tuhuma zinazomkabilia Askofu Mdegella ni Kushinikiza kulipwa mishahara miwili yaani kulipwa kama Askofu wakati huohuo kulipwa na Chuo kikuu cha Tumaini, kashfa nyingine ni kufisidi fedha za Dayosisi yake pamoja na za Chuo Kikuu cha Tumaini, makosa mengine ni kujihusisha na vitendo vya uzinzi kwani imeelezwa kuwa kwenye moja za ofisi yake kunakitanda ambacho inasadikiwa kuwa hukitumia kujipumzisha na baadhi ya kondoo zake, aidha miezi kadhaa iliyopita ilisikika kuwa alifanya jaribio la kumbaka mmoja wa wanachuo cha Tumaini - Iringa. Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi wajumbe wa tume hiyo walifukuzwa na Askofu Mdegella na ametishia kuondoa Dayosisi ya Iringa kwenye mfumo wa KKKT kama wataendelea kumfuatia nyendo zake.
Hata hivyo naamini uongozi wa KKKT ukiongozwa na Askofu Dk. Alex Malasusa utahakikisha kuwa wembe uliomnyoa aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki ya Pwani Jerry Ng'wamba unatumika vilivyo kumnyoa Askofu Mdegella ili iwe fundisho kwa wale wote wanao chezea kazi ya Mungu.