Askofu O.Mdegella kuwepo kwake KKKT ni Kumtukana Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu O.Mdegella kuwepo kwake KKKT ni Kumtukana Mungu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, May 25, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kanisa la KKKT halitakuwa salama kama litaendelea kuwavumilia viongozi wa kanisa na watendaji ambao wanatuhuma zisizovumilika ambazo haziendi sambamba na taratibu za Mungu . Moja ya viongozi wa Kanisa ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakituhumiwa na mambo yanayochafua huduma ya Bwana ni Askofu Mdegela ambaye ndiye Askofu wa Dayosisi ya Iringa. Pamoja na tuhuma zake kuwa za muda mrefu lakini uongozi wa KKKT umekuwa hauna la kufanya dhidi ya viongozi wa Dayosisi kutokana na udhaifu wa katiba ya KKKT ambayo pamoja na mapungufu mengi ya kimuundo lakini imeshindwa kurekebisha mapungufu hayo kiasi kuwa kwa muundo ulivyo wa KKKT Askofu Mkuu hana nguvu ya kumuwajibisha Askofu wa Dayosisi yoyote hata anapofanya makosa ya wazi ambayo yangehitaji kiongozi wa juu kuchukuwa hatua za kinidhamu kwa haraka.

  Kwa mujibu wa gazeti la leo la Mwana halisi imeelezwa kuwa Askofu huyu ameundiwa Tume ya kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo kwa sisi tunaomfahamu Askofu huyu niza kweli na za muda mrefu lakini uongozi wa KKKT haukuwa na lakufanya kutokana na ukweli kuwa katiba ya KKKT haina kipengere kinachoeleza hatua kuchukuliwa kwa Askofu anayekwenda kinyume na taratibu za kanisa. Kinachofanyika sasa hivi ni mpaka waumini waanzishe chokochoko na vurugu ndipo KKKT hufanya mlolongo wa kuunda tume na baadaye kuitishwa kwa mkutano mkuu ili kujadili jambo husika na hatua kuchukuliwa. Askofu mdegela kwa muda mrefu amekuwa akituhumiwa kwa vitendo vya uzinzi, ufisadi na kutumia madaraka yake vibaya lakini bado aliendelea kuvumiliwa.

  Kwa mujibu wa gazeti la mwanahalisi ambalo lilifuatilia sakata hili kwa karibu, askofu huyu ameundiwa tume inayoongozwa na Askofu Hance Mwakabana (Dayosisi ya kusini kati-makete), Askofu Dk. Martin shao - Dayosisi ya Kaskazini - Moshi) na Askofu Elisa Buberwa - Dayosisi ya Kaskazini Magharibi. Miongoni mwa tuhuma zinazomkabilia Askofu Mdegella ni Kushinikiza kulipwa mishahara miwili yaani kulipwa kama Askofu wakati huohuo kulipwa na Chuo kikuu cha Tumaini, kashfa nyingine ni kufisidi fedha za Dayosisi yake pamoja na za Chuo Kikuu cha Tumaini, makosa mengine ni kujihusisha na vitendo vya uzinzi kwani imeelezwa kuwa kwenye moja za ofisi yake kunakitanda ambacho inasadikiwa kuwa hukitumia kujipumzisha na baadhi ya kondoo zake, aidha miezi kadhaa iliyopita ilisikika kuwa alifanya jaribio la kumbaka mmoja wa wanachuo cha Tumaini - Iringa. Hata hivyo kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi wajumbe wa tume hiyo walifukuzwa na Askofu Mdegella na ametishia kuondoa Dayosisi ya Iringa kwenye mfumo wa KKKT kama wataendelea kumfuatia nyendo zake.

  Hata hivyo naamini uongozi wa KKKT ukiongozwa na Askofu Dk. Alex Malasusa utahakikisha kuwa wembe uliomnyoa aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki ya Pwani Jerry Ng'wamba unatumika vilivyo kumnyoa Askofu Mdegella ili iwe fundisho kwa wale wote wanao chezea kazi ya Mungu.
   
 2. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima kwako bwana Anold ( Nadhani ni bwana kama siyo samahani)
  Tafadhali naomba hiyo link ya mwanahalisi. Nimejaribu google search napata magazeti ya zamani.
  Natanguliza shukrani.
   
 3. A

  Anold JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Fanya mpango upate gazeti la Mwanahalisi toleo na. 243 la tarehe 25/5/2011 habari hiyo imeeleza kwa kina.
   
 4. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mkuu habari naona hawajaiweka kwenye mtandao.
   
 5. C

  Calist Senior Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaaa Mdegera ni muhuni kuliko hata wahuni wa mitaani, kwa uzinzi ndio hana kipimo binafsi nimegongana naye tukiwa tunamfukuzia kimwana mmoja, historia yake ni mbovu sana hafai hata kuwa mchungaji wa fisi.
   
 6. t

  titomganwa Senior Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acheni hizo Jamani. Msimhukumu mtu kabla hamjamsikiliza. Tena mnapomzungumzia mtumishi wa Bwana, aliyepakwa mafuta kuweni Makini sana. Kama huyu anayesema alikutana naye wakifukuzia kimwana mmoja! sasa tunajuaje kama amezungumza au kuzuusha habari hizi kwa chuki zake binafsi? Chunguzeni kabla ya kusema, shetani asije akawatumia kuliharibu kanisa la Bwana.

   
 7. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ha ha ha Tito, kweli busara zimekujaa. Tunahitaji kuchunguza hata kwa yaliyo wazi ili kupata ukweli uliofichika. Mkwawa wanasemaje lakini?
   
Loading...