Askofu Mwamakula: Wanapanga kunifungulia kesi ya uhaini/ ugaidi

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,700
Reaction score
103,703
‼️TAARIFA KWA UMMA; NIMEANDALIWA KESI NA UTAWALA WA SAMIA SULULUH, ILA SIOGOPI KUBAMBIKWA KESI NGUMU YOYOTE MTAKATOIANDAA KWASABABU MIMI SINA HATIA‼️

#Ndugu_Watanzania!🇹🇿
Nimepata taarifa zisizotiliwa shaka kuwa watu walio karibu na watawala wananijadili mimi na baadhi ya viongozi wa dini na kuwa wamefikia uamuazi kuwa tukamatwe na nifunguliwe kesi ngumu (uhaini au ugaidi) ili kuninyamazisha.

Lakini kwa upande wangu, nimejulishwa kuwa wamefikia uamuzi ili baada ya Tume ya Jaji Lila nikamatwe nifunguliwe kesi ngumu. Taarifa zilizonifikia zinatoka katika vyanzo vikuu vitatu ambavyo ni:

1. Watu wa usalama walio ndani ya mfumo na ambao hawakubaliani na jinsi namna ambavyo Serikali ya Rais Samia inavyoendesha mambo yake hasa baada ya mauaji ya 29 Oktoba 2025, kuondoshwa kwa Dkt. Emmanuel Nchimbi na kutekwa na kupotezwa kwa Balozi Humphrey Polepole.

2. Watu walio karibu na Ofisi za Ubalozi mmoja kutoka nchi za Magharibi ambazo zimekuwa zikiipigia kelele Serikali ya Rais Samia kuhusu masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu na hasa tangu mauaji ya 29 Oktoba 2025. Wao pia wana idara zao za kufuatilia mambo nchini.

3. Na kauli ya mwanaharakati wa Kitanzania, Mange Kimambi anayeishi Marekani ambaye amekuwa mpiga miluzi (whistle blower) juu ya masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania. Huyu naye pia hupewa taarifa kutoka ndani ya watu wa Serikali wasioyaunga mkono matendo ya ukiukwaji haki za watu.

Taarifa za vyanzo vingine pia zipo lakini hazifai kuelezwa katika hatua hii kwa sasa. Lakini kwa kuwa taarifa kutoka katika vyanzo vyote hivyo zinaoana imekuwa vigumu sana kwangu kukaa kimya pasipo kuujulisha umma.

Inaelezwa kuwa watawala wanafanya juhudi za makusudi kutaka kutunyamazisha baadhi ya watu hasa viongozi wa dini tunaoipigia kelele kuhusiana na masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.

Kwa upande wangu, kuna mambo makuu 4 ambayo yamewafanya watawala washauriwe kuchukua uamuzi huo wa kunibambika kesi:

1. Nimekuwa mstari wa mbele kumtetea Lissu ikiwemo kutoa maandiko na kauli zinazofunua uelewa wa watu nchini na nje ya nchi.

2. Nilipiga sana kelele na bado pia ninaendelea kupiga kelele juu ya kupotezwa kwa Mhe Balozi Humphrey Polepole.

3. Nilipiga sana kelele na pia bado ninaendelea kupiga kelele kutaka pia aliyekuwa Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi awe huru maana kuna hisia kuwa amewekwa chini ya ulinzi au kizuizini. Tangu taifa litangaziwe ya kuwa amejiuzulu, Mhe. Nchimbi hajaonekana hadharani ikiwemo pia katika nyumba za ibada.

4. Nilipiga sana kelele na bado pia ninaendelea kupiga kelele juu ya mauaji ya 29 Oktoba 2025 ambapo nimekuwa nikiihusisha moja kwa moja Serikali kuhusika na mauaji hayo. Lakini katika hili mimi nimeonyesha wazi msimamo wangu wa kutounga mkono kitendo cha Rais Samia kuunda Tume za Uchunguzi kwa kuwa yeye na Serikali yake ni sehemu ya watuhumiwa.

5. Nilipiga sana kelele na pia naendelea kupiga kelele kutaka kujua walipo watu waliotekwa na kupotezwa kama vile Mdude Mpaluka Nyagali, Dioniz Kipanya, Juma Kaswahili, Deusdedith Soka, Chaula, Mlay, Mbise, nk. Hawa wakitekwa kwa sababu walikuwa wanaikosoa Serikali ya Rais Samia.

6. Nilipiga kelele na pia bado naendelea kupiga kelele kuhusu hali ya usalama wa Watanzania ambao wameikimbia nchi baada ya mauaji ya 29 Oktoba 2025.

Kutaka kuninyamazisha mimi pia ni sehemu ya mkakati wa watawala unaokwenda sambamba na kutaka kunyamazisha sauti mbadala kama za Rais wa TLS, Boniface Anyisile Mwabukusi, wakili Peter Madeleka, Padri Charles Kitima, Askofu Josephat Gwajima, Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza, nk.

Lengo la kutaka kutunyamazisha sisi ni kutaka kupunguza kelele za kuwapigania viongozi wa CHADEMA ambao wanawindwa nchi nzima na kukamatwa na kubambikwa kesi za ugaidi na hata uhaini.

Lakini kinachotushangaza ni kuwa watu ambao wanapanga mkakati huo wanataka pia kuitumia Tume ya Jaji Lila kuwa ndiyo iliyotukuta sisi na hatia kuhusiana na mauaji ya 29 Oktoba 2025. Inashangaza kuona watu hao wamekuja kabisa na verdicts (maamuzi) wakati Tume ya Jaji Lila bado kuhitimisha 'mambo yao'!

Wakati ukifika, jumuiya ya kimataifa itajulishwa kuhusu mpango huo wa kutaka kunibambika kesi ngumu. Lakini hata kama watanikamata muda huu, hiyo haitaondoa adhma hiyo. Lakini na ijulikane kuwa Mungu wangu atanipigania na Watanzania watasimama na mimi kwa kuwa nilisimama kwa ajili ya kutetea na kuwasemea watu wasiokuwa na sauti. Kikubwa, nilitimiza wajibu wangu wa kikuhani (Ezekieli 33:1-20).

Kwa neema ya Mungu, nitatunzwa na siku moja nitakuja kuwa sauti pekee ya kuwatetea ambao leo wanapanga hila za kunikamata na kutaka kunibambika kesi ngumu (kesi ya haini au kesi ya ugaidi).
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 21 Oktoba 2026; Saa 9:20 alasiri.
 
Askofu usiye na waumini tulizana,hakuna mwenye habari na wewe!,ungelikuwa mtu muhimu sana au hatari ungelisha kamatwa kitambo sana,unajulika sana ya kwamba unasumbuliwa na njaa tu.
 
Yes,
si inafahamika huyo askofu wa mchongo ni mchochezi wa muda mrefu sana ndani ya Chadema Church, ambayo nadhani ndio daima kanisa analotumia kuongoza ibada zake za fujo na ghasia.

ni muhimu akatiwa mbaroni na akawajibishwa kwa mujibu wa sheria za nchi ili iwe fundisho kwa maaskofu wa mchongo kama huyo :NoGodNo:
 
Askofu usiye na waumini tulizana,hakuna mwenye habari na wewe!,ungelikuwa mtu muhimu sana au hatari ungelisha kamatwa kitambo sana,unajulika sana ya kwamba unasumbuliwa na njaa tu.
Kuna wachangiaji ambao wakichangia hata kama wana point wadau huwa wanawapuuza. Mfano wewe, Tlaatlaa, Lucas, Voice na the likes.
 
Na ndio maana dini ya kiislam inaonekana ya hovyo kwa watu kama wewe kuwa na ubaguzi wa kijinga kuhusu imani ya mtu.
 
Kama risasi, utekaji, kesi za kubumba zingekua zinaua upinzani basi watanzania wangekua kimya sasa wanaimba mapambio kama enzi za Moi na kumwita Samuya mtukufu.

Ila ndio kwanza upinzani mkali na chuki dhidi yake umeongezeka maradufu.
 
‼️TAARIFA KWA UMMA; NIMEANDALIWA KESI NA UTAWALA WA SAMIA SULULUH, ILA SIOGOPI KUBAMBIKWA KESI NGUMU YOYOTE MTAKATOIANDAA KWASABABU MIMI SINA HATIA‼️

#Ndugu_Watanzania!🇹🇿
Nimepata taarifa zisizotiliwa shaka kuwa watu walio karibu na watawala wananijadili mimi na baadhi ya viongozi wa dini na kuwa wamefikia uamuazi kuwa tukamatwe na nifunguliwe kesi ngumu (uhaini au ugaidi) ili kuninyamazisha.

Lakini kwa upande wangu, nimejulishwa kuwa wamefikia uamuzi ili baada ya Tume ya Jaji Lila nikamatwe nifunguliwe kesi ngumu. Taarifa zilizonifikia zinatoka katika vyanzo vikuu vitatu ambavyo ni:

1. Watu wa usalama walio ndani ya mfumo na ambao hawakubaliani na jinsi namna ambavyo Serikali ya Rais Samia inavyoendesha mambo yake hasa baada ya mauaji ya 29 Oktoba 2025, kuondoshwa kwa Dkt. Emmanuel Nchimbi na kutekwa na kupotezwa kwa Balozi Humphrey Polepole.

2. Watu walio karibu na Ofisi za Ubalozi mmoja kutoka nchi za Magharibi ambazo zimekuwa zikiipigia kelele Serikali ya Rais Samia kuhusu masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu na hasa tangu mauaji ya 29 Oktoba 2025. Wao pia wana idara zao za kufuatilia mambo nchini.

3. Na kauli ya mwanaharakati wa Kitanzania, Mange Kimambi anayeishi Marekani ambaye amekuwa mpiga miluzi (whistle blower) juu ya masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania. Huyu naye pia hupewa taarifa kutoka ndani ya watu wa Serikali wasioyaunga mkono matendo ya ukiukwaji haki za watu.

Taarifa za vyanzo vingine pia zipo lakini hazifai kuelezwa katika hatua hii kwa sasa. Lakini kwa kuwa taarifa kutoka katika vyanzo vyote hivyo zinaoana imekuwa vigumu sana kwangu kukaa kimya pasipo kuujulisha umma.

Inaelezwa kuwa watawala wanafanya juhudi za makusudi kutaka kutunyamazisha baadhi ya watu hasa viongozi wa dini tunaoipigia kelele kuhusiana na masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.

Kwa upande wangu, kuna mambo makuu 4 ambayo yamewafanya watawala washauriwe kuchukua uamuzi huo wa kunibambika kesi:

1. Nimekuwa mstari wa mbele kumtetea Lissu ikiwemo kutoa maandiko na kauli zinazofunua uelewa wa watu nchini na nje ya nchi.

2. Nilipiga sana kelele na bado pia ninaendelea kupiga kelele juu ya kupotezwa kwa Mhe Balozi Humphrey Polepole.

3. Nilipiga sana kelele na pia bado ninaendelea kupiga kelele kutaka pia aliyekuwa Makamu wa Rais, Mhe. Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi awe huru maana kuna hisia kuwa amewekwa chini ya ulinzi au kizuizini. Tangu taifa litangaziwe ya kuwa amejiuzulu, Mhe. Nchimbi hajaonekana hadharani ikiwemo pia katika nyumba za ibada.

4. Nilipiga sana kelele na bado pia ninaendelea kupiga kelele juu ya mauaji ya 29 Oktoba 2025 ambapo nimekuwa nikiihusisha moja kwa moja Serikali kuhusika na mauaji hayo. Lakini katika hili mimi nimeonyesha wazi msimamo wangu wa kutounga mkono kitendo cha Rais Samia kuunda Tume za Uchunguzi kwa kuwa yeye na Serikali yake ni sehemu ya watuhumiwa.

5. Nilipiga sana kelele na pia naendelea kupiga kelele kutaka kujua walipo watu waliotekwa na kupotezwa kama vile Mdude Mpaluka Nyagali, Dioniz Kipanya, Juma Kaswahili, Deusdedith Soka, Chaula, Mlay, Mbise, nk. Hawa wakitekwa kwa sababu walikuwa wanaikosoa Serikali ya Rais Samia.

6. Nilipiga kelele na pia bado naendelea kupiga kelele kuhusu hali ya usalama wa Watanzania ambao wameikimbia nchi baada ya mauaji ya 29 Oktoba 2025.

Kutaka kuninyamazisha mimi pia ni sehemu ya mkakati wa watawala unaokwenda sambamba na kutaka kunyamazisha sauti mbadala kama za Rais wa TLS, Boniface Anyisile Mwabukusi, wakili Peter Madeleka, Padri Charles Kitima, Askofu Josephat Gwajima, Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza, nk.

Lengo la kutaka kutunyamazisha sisi ni kutaka kupunguza kelele za kuwapigania viongozi wa CHADEMA ambao wanawindwa nchi nzima na kukamatwa na kubambikwa kesi za ugaidi na hata uhaini.

Lakini kinachotushangaza ni kuwa watu ambao wanapanga mkakati huo wanataka pia kuitumia Tume ya Jaji Lila kuwa ndiyo iliyotukuta sisi na hatia kuhusiana na mauaji ya 29 Oktoba 2025. Inashangaza kuona watu hao wamekuja kabisa na verdicts (maamuzi) wakati Tume ya Jaji Lila bado kuhitimisha 'mambo yao'!

Wakati ukifika, jumuiya ya kimataifa itajulishwa kuhusu mpango huo wa kutaka kunibambika kesi ngumu. Lakini hata kama watanikamata muda huu, hiyo haitaondoa adhma hiyo. Lakini na ijulikane kuwa Mungu wangu atanipigania na Watanzania watasimama na mimi kwa kuwa nilisimama kwa ajili ya kutetea na kuwasemea watu wasiokuwa na sauti. Kikubwa, nilitimiza wajibu wangu wa kikuhani (Ezekieli 33:1-20).

Kwa neema ya Mungu, nitatunzwa na siku moja nitakuja kuwa sauti pekee ya kuwatetea ambao leo wanapanga hila za kunikamata na kutaka kunibambika kesi ngumu (kesi ya haini au kesi ya ugaidi).
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 21 Oktoba 2026; Saa 9:20 alasiri.
Kristo alilia kwa maumivu makuu pale msalabani, Mungo wangu Mungu wangu mbona umeniacha? Kisha akasema yametimia na kukata roho.

Maumivu ya wapigania haki no yenye uzito mkubwa sana. kila pale wanapohisi kuwa wameachwa wapweke, ndipo mkono wenye nfuvu wa Mungu mwenye haki hudhihirika.

CCM, CCM, CCM, your days are numbered.
 
Siasa za Africa ni ngumu sana ni Bora hata ukae kimya .
1792650629920.jpg
 
Aache kukimbia Kivuli chake atubu kwa mchango wake kwenye machafuko ya October 29
 
Kuna wachangiaji ambao wakichangia hata kama wana point wadau huwa wanawapuuza. Mfano wewe, Tlaatlaa, Lucas, Voice na the likes.

Hao Tlaatlah, Mwashambwa, Dr wa Manesi, Chrocodiletooth, unapozungumzia akili, kwa kweli, hizo ni takataka. Ukiona tu majina yao unajua hakuna lolote la maana.
 
Back
Top Bottom