upupu255
JF-Expert Member
- Sep 4, 2024
- 341
- 476
Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Lameck Musomba, amesema Taifa limepitia mwaka wenye majonzi makubwa uliodhihirisha kupotea kwa mwelekeo wa maadili na mshikamano wa kijamii, akisisitiza umuhimu wa Watanzania kurejea kwa Mungu, haki na kuheshimiana ili kulinda amani ya nchi.
Askofu Musomba ameyasema hayo wakati wa Misa Takatifu ya Mkesha wa Kuukaribisha Mwaka Mpya 2026 iliyofanyika katika Parokia ya Mwenyeheri Isidori Bakanja, Boko, Jimbo Katoliki la Bagamoyo. Akirejea tukio la Oktoba 29, Askofu Musomba amesema taifa lilikumbwa na janga kubwa lililosababisha vifo vya watu wengi, tukio alilosema halijawahi kuwa la kawaida katika historia ya Tanzania, hata wakati wa janga la UVIKO-19.
Amesema tukio hilo lilizua mshangao, hofu na maswali mengi kwa Watanzania, huku likiwaacha wengi wakitafakari mwenendo wa taifa na uhusiano wake na Mungu, akisisitiza kuwa janga hilo lilipaswa kuwa funzo la kitaifa.
Askofu Musomba amesema kiburi, kutosikilizana, kukosa ushauriano na kuachana na misingi ya uongozi bora ni miongoni mwa sababu zilizosababisha taifa kupoteza mwelekeo, hali iliyochochea migogoro, machafuko na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wananchi.
Askofu Musomba amesema mbali na kumshukuru Mungu kwa amani, amani inapaswa kwenda sambamba na kuhakikisha haki, heshima, uhuru wa maoni na usikivu vinazingatiwa katika jamii.