Askofu Msonganzila: Imefika wakati tufanye mabadiliko ndani ya jeshi la Polisi

Askofu Msonganzila: Imefika wakati tufanye mabadiliko ndani ya jeshi la Polisi

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
638
Reaction score
1,771
Askofu Michael Msonganzila ametoa pendekezo hilo wakati akizungumzia kitendo cha jeshi polisi kuwashambulia bawacha eneo la kanisani

---
Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael Msonganzila amelaani tukio la Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama, wafuasi na viongozi Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) katika eneo la Kanisa Kuu la jimbo hilo mjini Musoma, akisema kitendo hicho kinazidisha chuki kwa jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma leo Jumanne Machi 10, 2026, Askofu Msonganzila amesema Jeshi la Polisi lilipaswa kutumia busara na hekima badala ya kutumia nguvu kuwatawanya watu hao, ambao hawakuwa na aina yoyote ya silaha.
 
.
 
Attachments

  • downloadfile-15.jpg
    downloadfile-15.jpg
    135.1 KB · Views: 4
Askofu Michael Msonganzila ametoa pendekezo hilo wakati akizungumzia kitendo cha jeshi polisi kuwashambulia bawacha eneo la kanisani

View attachment 3556171

---
Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael Msonganzila amelaani tukio la Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama, wafuasi na viongozi Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) katika eneo la Kanisa Kuu la jimbo hilo mjini Musoma, akisema kitendo hicho kinazidisha chuki kwa jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma leo Jumanne Machi 10, 2026, Askofu Msonganzila amesema Jeshi la Polisi lilipaswa kutumia busara na hekima badala ya kutumia nguvu kuwatawanya watu hao, ambao hawakuwa na aina yoyote ya silaha.
Duh.
 
Sifa kubwa ya kuwa plsi wa Tz, ni uwe huna akili yà juu. Simbachawene alisema kuwa sababu ya kuwaajiri wenye akili ndogo kuwa polsi ni kwa sababu wenye akili timamu hawawezi kukubali kufanya kazi ya kulinda benki.
 
Kwanza ieleweke Tanzania hatuna kitu kinaitwa "Jeshi la Polisi",Ni wahuni tu ambao ni Darasa la Saba na Form 4 Failure waliamua kukaa huko Bungeni na kutunga sheria za kiduanzi ili Iliyopaswa kuitwa "IDARA YA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO" kuipa jina la "JESHI"

JESHI ni ARMY,Tanzania tunalo Jeshi moja tu ambalo ni Jeshi la Wananchi,Ila kwakuwa wapuuzi kadhaa walitunga na kupitisha sheria za kiduanzi ndiyo maana Iliyopaswa kuitwa "IDARA YA USALAMA" inaitwa "JESHI LA POLISI"

Hata hapo Uingereza ambapo sheria zetu nyingi tumerithi kutoka kwao bado polisi hawaitwi"JESHI"

Anyway

Nilikuwa nawaelewesha wajinga kadhaa!

MAONI YANGU

Jeshi la Polisi nchi hii halihitaji mabadiliko,Mabadiliko yapi utayafanya ndani ya Jeshi ambalo lipo kutekeleza matakwa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Badala ya kufuata na kusimamia sheria kwa mujibu wa Sheria na Katiba!?

Ok,Tuseme umefanya mabadiliko! ,Je CCM haipo Madarakani?,Kama CCM ipo Madarakani endeleeni kusahau Jeshi lenu la Polisi kujifungamanisha na CCM!

Hebu fikiria tu suala dogo kama la BAWACHA na siku ya wanawake!

Polisi hawa Wajinga ambao walipaswa kusimamia sheria wao ndiyo wamegeuka wanasiasa mbadala wa CCM na kuwananga wanawake wa CHADEMA!

UKITAKA KUFANYA MABADILIKO KWENYE IDARA YA POLISI (JESHI LA POLISI) HAKIKISHA CCM HAWAPO MADARAKANI!,TOFAUTI NA HAPO MTAKUWA MNAJAZA MAJI KWENYE TENGA!
 
Back
Top Bottom