DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael George Mabuga Msonganzila, amewataka waumini na viongozi wa dini nchini kutokubeba jazba wala kujiingiza katika mijadala ya matusi, lawama na kejeli inayoibuka mitandaoni na kwenye mikutano ya kijamii, akisema kuwa njia ya Kristo ni ya upole, uvumilivu, huruma na kutanguliza haki.
Akizungumza kufuatia mfululizo wa matamko kutoka taasisi kadhaa za Kikristo na Kiislamu kuhusu matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu, huku baadhi ya kauli zikiishambulia Kanisa Katoliki kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uchochezi dhidi ya amani ya nchi, Askofu Msonganzila amesema kuwa migogoro na kejeli haviwezi kuizima nguvu ya ukweli.
“Hamna sababu ya kuijibu, ni kuinyamazia tu wakati mwingine watu wakisema sisi tumeenda shule sio zamani, kwani kwenda shule ni shida? Shida ni kusoma, shida ni kuelimika, sasa kuzozanazozana katika misingi hiyo haina haja- ni kunyamaza kama Kristo aliyedhihakiwa: Wewe si ni mwana wa Mungu Jiokoe basi nafsi yako, Nyamaza kimya endelea kusali”, amesema.
Askofu Msonganzila amesisitiza kuwa nguvu ya maneno ya kupotosha haiwezi kuzidi uzito wa maadili, utu, na dhamira njema ya Kanisa, akionya kuwa matusi na vitisho ambavyo vimekuwa vikitolewa haviwezi kubadilisha msingi wa imani wala wajibu wa viongozi wa dini kusimama katika kweli.
“Mahangaiko yakitokea ndugu zangu tusiogope kwa sababu ndio Kristo amepitia njia hiyo, Kanisa Katoliki linaweza likateseka kwa njia za namna hiyohiyo na matishio mbalimbali: umemwaga ugali tutamwaga mchuzi, tutawakatakata- tusiogope Mungu yupo”, ameeleza.
Kauli ya Askofu Msonganzila imekuja wakati ambapo mjadala kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kueleza ukweli wa kijamii na kisiasa umeendelea kushika kasi, huku baadhi ya taasisi za kiimani zikitoa matamko yanayopingana kuhusu misimamo ya Kanisa Katoliki na makundi mengine ya kijamii kuhusu mwenendo wa uchaguzi na matukio yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.