Askofu Mokiwa: UCHAGUZI 2010 UTAKUWA MGUMU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Mokiwa: UCHAGUZI 2010 UTAKUWA MGUMU

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Teamo, Jul 19, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  askofU mukiwa anasema leo wazi wazi kwamba uchaguzi wa 2010 utakuwa mgumu sana kwa wanasiasa wengi kwa sababu wananchi wengi wameshajua haki zao ni zipi!.

  .''....wanasiasa waongo hawana nafasi,wananchi wengi wameshajua haki zao,kanisa la kianglikana limejiandaa kwa dhati kabisa kuwaelimisha waumini wake namna na vigezo vya kumchagua kiongozi bora!.....''

  HAYA SASA JAMANI!kazi mnayo wakina masatu,wakina GT,na wengine ,na kwa yoyote anayehusika
   
 2. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Moto juu ya moto yaani watu wapakua na kubandika moto mwingine .Nape endelea kulia lia kwenye TV .
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Nnauye kwenye siasa za kizazi hichi ATACHEMKA,HATAFURUKUTA!kama kweli ni mjanja basi anapaswa kusoma alama za nyakati!

  WATU WAMEAMKA SASA!
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Niulize jamani, huyu Mokiwa ni kiongozi wa chama gani ehhh???
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahahahahahah!mkuu huyu ni askofu mkuu wa kanisa la anglikana!kama mchungaji AMETIMIZA WAJIBU WAKE KWA KONDOO WAKE!I BELIEVE THAT
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu najua kama Mokiwa ni askofu ila siku hizi namsikia sana katika Majukwaa ya kisiasa, ndiyo nikauliza hivyo.
   
 7. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wewe ni Kiongozi wa chama chochote cha siasa? Maana unaonekana sana kwenye Jukwa la siasa hapa JF.
  Nadhani ni haki ya kila Mtanzania kuzungumzia mstakabari wa nchi yake? au katiba imetenga wananchi wa makanisni na misikitini wasingumzie kabisa masuala ya nchi yao??? Nadhani ni kiongozi wa kundi kubwa la watu mimi watu kama hawa nawaheshimu sana, wanaushwishi mkubwa sana sawa na Krdinali pengo, Sheikh Simba, Ni sehemu ya jamii, wanafeelinga, na walionja joto la jiwe kama wengine wote. Kwa kfupi Dini ya Kikristo inasisitiza Viongozi wake kama mitume wa Mungu kuwakemea Viongozi wa serikali wanapoenda tofauti. Hajakosea kama raia, hajakosea kama kiongozi wa kidini.
   
 8. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mkuu Heshima Mbele.
  Kabla hawa uliwaambia wanakazi labda nikuombe kuwa siku nyingine ulete thread iliyokamilika.
  1. alikuwa naongea wapi?
  2. Aliongea na akina nani
  3. Nini Kimemfanya aongee hayo?
  4. Umeipata wapi habri hii (source mkuu wangu ni muhimu, watu makini hatujadili mada kama the credibility of its source is questionable suipojibu hayo maswali kiufasaha ndio kwa heri kwenye hii thread yako hunikuti enedelea na hao wababishaji wengine)
   
 9. S

  Sebere Member

  #9
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 16, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera Mh Mokiwa,tunaomba viongozi wengine wa Kikristo na Kiislamu mfuate nyayo kukemea ufisadi na mambo mengine maovu yanayofanyika katika nchi hii.
   
 10. b

  bangusule Senior Member

  #10
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  sebere,
  wewe mwenzetu ni wa monduli juu?
   
 11. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,966
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Hawa maaskofu wamechoka amani.Bado hawajastuka jinsi watu waa mbeya walivo BIP huko tunduma na kyela.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wabongo wamelala kuna haja ya kuwaamsha by anymeans ili wawe serious na mustakabali wa nchi yao kitu amabcho CCM wanakiogopa.
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  .........NA SAFARI HII WATAAMKA!hakika wataamka
   
 14. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Askofu Mukiwa aende akawaelimishe Waumini wake kwanza ndio aje kutuambia iwapo wameshaelimika au bado na kama bado ni vipi amejizatiti kufikia lengo. Sio anakuja kutueleza "ndoto zake za kwenda" kuwaelisha halafu wakati huo huo anaweka hitimisho kuwa wananchi wameshaelewa namna ya kuchagua viongozi bora.

  Mimi nasema bado wananchi hawajaelewa; hizi ni fikra za kujazana ujasiri potofu hazitasaidia demokrasia ya Tanzania hata kidogo.
   
 15. B

  Bobby JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Junius basi hivi ndivyo viongozi wa dini wanapaswa kuwa. Hope unajuwa kwamba we are all political animals whether we like it or not. Na neno la Mungu linalotenga mwili na roho limepitwa na wakati. Mungu hakuumba roho peke yake aliumba na mwili pia. Na it's a well known fact kwetu sote kwamba miili yetu inaathiriwa kwa kiwango kikubwa na maamuzi ya kisiasa. Kifupi nawapongeza sana Roman Catholic na Anglican kwa kuamuka-this is really good.
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hata mimi nawapongeza zaidi,THEY ARE PLAYING THEIR ROLE TO THE COMMUNITY!kinyume na hilo watakuwa hawatufai kabisa
   
 17. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Haya jamani tuwe mashahidi sote humu JF kuwa kama RC na Anglikana wanafanya wajibu wao na wengine kufuatia RUKSA eeeh!
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu, sheria zetu zinakataza kutumia majukwaa ya dini kwa mambo ya kisiasa na kinyume chake. Si tatizo Asokofu Mokiwa kama watanzania wengine kuzunguzia mambo ya nchi yake lakini je katika jukwaa lipi???
  Maana tumeona kule Spika anakataza wenzake kuleta udini udini katika bunge lakini wakati huo huo anapongeza waraka wa kiaskofu, kana kwamba chombo anachokiongoza hakina wala hakijatunga sheria zinazoongoza wananchi kuchagua viongozi bora. Naye(sitta) pia nauliza ni askofu wa jimbo gani?
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  "Mind once stretched, will never regain its originl shape"
   
 20. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ndio maana niliuliza alikuwa akiongea wapi? na nani? kwasababu gani? kama alikuwa nafungua chuo cha kanisa cha uongozi bora asiseme maneno kama hay? kama alikuwa nafanyiwa interview na waandishi asiseme? Hoja yenyewe imeletwa haijakamilika.

  Tumelishwa kasumba mbovu na CCM kuwa viongozi wa Dini wasituambie maovu ya wanasiasa. Hata Mfalme Daudi alimpofanya dhambi ya kumchukua Mke wa Uria, Mungu alimtuma Nabii Nathan akamwonye na Kumkemea, alipotoza kodi na wakusanya kodi wakawa wanakula hizo pesa za walalahoi (ufisadi) watumishi wa Mungu walimkemea kwa nguvu na kodi ikafutwa (Hizi zipo kwenye biblia na hadith) sasa sijui kama maandiko haya siku hizi sio valid tena?
   
Loading...