Elections 2010 Askofu Mokiwa akataa rushwa ya Sh11 milioni!

Hao nao mbona izo fedha ni chache kumhonga askofu,wangeenda na Billioni ama kweli chama kimeishiwa hasa baada ya kufuja mali
 
watu wana pesa mazee, yani mtu anatembea na mill. 10 kirahisi hivyo?? Wanazitoa wapi aisee.
 
Bravo Dr. Mokiwa!!!!! Ila najiuliza nani mwenye jeuri ya kumpelekea Dr. Mokiwa rushwa kama sio hawahawa wanamtandao?
 
Kwa nchi kweli zinazofuata utawala wa sheria vyombo husika vilitakiwa vimuhoji mokiwa ili jamii iwajue wahusika. Na ikiwezekana wachukuliwe hatua.

Kwa mtu wa level ya uelewa na elimu ya Askofu mokiwa alitakiwa a deal na hii issue tofauti na alivyofanya.

Lakini hakuna kilichoharibika sasa vyombo husika TAKUKURU ,POLISI wanaweza kuendelea.
 
angezichukua,angewaita waandishi wa habari na kisha kuzipeleka kituo cha watoto yatima,kuwarudishia hizo pesa wahusika ni kuwajengea mazingira ya kumtafuta mtu mwigine wa kumpa hizo pesa ambazo ni haki yetu,
Huo ulikuwa mtego mzee fungua macho kabla hajaita wana habari au hajazikabidhi kwa watoto yatima, ilikuwa aanikwe na kuvishwa pingu! so jaribuni kufikiria! hapo ilikuwa ni kutegua maono yake maana walikuwa wanajua anachosimamia yaani "pokea halafu usipige kura"!
 
Angepelekewa malaria sugu, nadhani angeliangua kicheko. Hongera sana mtumishi.
 
Kauli za kisaniisanii tu..kama yeye Mokiwa ni mkweli na hana cha kuficha kwanini asiweke vitu hadharani bila chenga?
 
Dr Slaa AKUMBUKE kutamka wazi kuwa anawapenda wana CCM na aendee kuziomba kura zao kama alivyofanya mwanzoni. Hata wana ccm wenyewe wameishamchoka Kikwete. Asisitize kuwa wana CCM wengi wana mapenzi mema na nchi yao, na hata yeye anawapenda. Isipokuwa CCM imekuwa ya mafisadi wachache, ndio wanaofaidi. Wana CCM wengi waliobaki, pamoja na ushabiki hawana wanachokifaidi ndani ya Chama chao. Asisitize kuwa yeye ndiye mkombozi wa wote na hasa wana CCM!

Kauli kama hii yaweza kuvuta hisia na kubadili mawazo ya watu kwa haraka sana. Dr Slaa ukumbuke ulivyomsema vizuri Mwakyembe ulikuwa kivutio, ukabadili hisia za watu na kusababisha wana CCM wote wakukubali. Dr Slaa sasa wasifie wana CCM. Toa kauli nzuri kwamba wewe ni mkombozi wa Wana CCM. Adui mkubwa wa CHADEMA ni mafisadi na sio wana CCM. Tafadhali Dr Slaa usisitize jambo hili.

Maana watu wasio na uelewa wanakatana mapanga wakidhani wewe utakuwa rais wa wana CHADEMA na hivi kuwatelekeza wao.

Valid piece
 
Sasa subirini watakavyomgeuzia kibao na kumshambulia kama yule Askofu mwingine pale Mwenge.

Angalau tuna viongozi wachache wa dini wenye kujua kusema ukweli bila kuogopa.
 
Hilo ni somo zuri na tosha kwa mawakala wa vyama hasa vya upinzani katika kukataa hongo kwa ajili ya kubadilisha matokeo!!
 
angezichukua,angewaita waandishi wa habari na kisha kuzipeleka kituo cha watoto yatima,kuwarudishia hizo pesa wahusika ni kuwajengea mazingira ya kumtafuta mtu mwigine wa kumpa hizo pesa ambazo ni haki yetu,
nakubaliana na wewe, then angewakabidhisha hao watu kwa TAKUKURU...japo hawatafanywa kitu kama tulivyozoea, lakini angekuwa amefanya jambo jema zaidi!
 
angezichukua,angewaita waandishi wa habari na kisha kuzipeleka kituo cha watoto yatima,kuwarudishia hizo pesa wahusika ni kuwajengea mazingira ya kumtafuta mtu mwigine wa kumpa hizo pesa ambazo ni haki yetu,

wewe aliyekuambia hizo habari za askofu ni za kweli ni nani?
 
Back
Top Bottom