Elections 2010 Askofu Mokiwa akataa rushwa ya Sh11 milioni!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,060
22,755
Friday, 15 October 2010
Na Hussein Kauli


SIKU 16 kabla ya kufanyika wananchi kupiga kura, askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dk Valentino Mokiwa amedai kuwa hivi karibuni alipelekewa rushwa ya Sh11 milioni na mtu asiyemfahamu ili asizungumze masuala ya uchaguzi.

Dk Mokiwa alisema hayo kwenye tamasha la kuombea uchaguzi mkuu lililoandaliwa na Usharika wa Yombo wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT) Dar es Salaam jana.


Alisema tukio hilo lilitokea siku moja baada ya watu wawili mmoja akiwa anamjua kwenda nyumbani kwake kwa lengo la kumsalimia ambapo alizungumza nao kisha wakaondoka.


"Siku moja baadaye, mlinzi alinipigia simu akaniambia yule mgeni wa jana ameleta ….nikamwambia kwa nini ulichukua? sina ahadi na mtu yeyote kuniletea mzigo," alisema Dk Mokiwa.


Alifafanua kuwa taarifa hizo zilimlazimu aende nyumbani kwake ili kujua nini kimeletwa... na alipofungua alikuta fedha taslimu Sh11 milioni ambazo zilimtia wasiwasi.


"Nikampigia yule ninayemfahamu nikamwambia njoo uchukue fedha za jamaa yake, akaniambia 'usiwe na wasiwasi', nikamwambia haiwezekani njoo akaja akachukua zile fedha," alisema.



Aliongeza kuwa alikumbuka maneno ya mtu yule wakati walipokwenda nyumbani kwake kuwa nyinyi (viongozi wa dini) mkizungumza nchi inatikisika, akaona ile ilikuwa ni rushwa ili anyamaze kuzungumzia masuala ya uchaguzi mkuu ujao.


Alisema aliamua kukataa fedha hizo kwa sababu alikuwa na wasiwasi asije baadaye akaambiwa na yeye alipewa fedha za rushwa na kumalizia nyumba yake kwani ile kwake ilikuwa ni rushwa ili anyamaze.


Akizungumzia hoja yake iliyopingwa na taasisi za serikali zinazohusiana na rushwa na uchaguzi kwa madai kuwa anahamasisha watu kupokea rushwa, Dk Mokiwa alisema:


"Mimi sikuhamasisha rushwa ila nilikuwa nawapinga viongozi wabaya wanaotoa rushwa kwa wapiga kura. Sheria ya Gharama za Uchaguzi si mbaya, lakini wasimamizi wa sheria hiyo ndio wabaya," alisema Dk Mokiwa.


Alidai kuwa atafanya awezalo kuhakikisha kuwa viongozi wala rushwa hawaiongozi nchi hii kwa sababu mwaka huu rushwa imeenea na wakati huu wa kampeni rushwa ndio inaliwa sana na viongozi wasiokubalika ndio watoa rushwa.


"Tunamuomba Mungu leo, tupate viongozi ambao hawajawahi kutuongoza nchi hii; viongozi watakaotuletea amani bila ya kuwepo polisi shirikishi kwa kuwa hapa tulipofika ni matokeo ya kuwapa ushirikiano viongozi wabovu," alisema.


Akizungumzia kauli ya vyombo vya usalama juu ya amani kulekea kwenye uchaguzi, Dk Mokiwa alisema ili kulinda amani iliyopo hakuna budi vyombo hivyo vikatenda kazi yake bila ya upendeleo katika kusimamia uchaguzi.


"Nani alisema hakuna amani, tatizo ni vyombo hivi vinataka kuwalinda watu waendelee kuongoza wakati wananchi wamewachoka. Wanatakaiwa wawe fair katika usimamizi," alisema.


Source: Askofu Mokiwa akataa rushwa ya Sh11 milioni

My take:
Si vigumu kukisia wahusika wanatoka chama gani.
 
angezichukua,angewaita waandishi wa habari na kisha kuzipeleka kituo cha watoto yatima,kuwarudishia hizo pesa wahusika ni kuwajengea mazingira ya kumtafuta mtu mwigine wa kumpa hizo pesa ambazo ni haki yetu,
 
Wazalendo bado wapo nchi hiii! MUNGU AKULINDE DK MOKIWA!
 
Dr Slaa AKUMBUKE kutamka wazi kuwa anawapenda wana CCM na aendee kuziomba kura zao kama alivyofanya mwanzoni. Hata wana ccm wenyewe wameishamchoka Kikwete. Asisitize kuwa wana CCM wengi wana mapenzi mema na nchi yao, na hata yeye anawapenda. Isipokuwa CCM imekuwa ya mafisadi wachache, ndio wanaofaidi. Wana CCM wengi waliobaki, pamoja na ushabiki hawana wanachokifaidi ndani ya Chama chao. Asisitize kuwa yeye ndiye mkombozi wa wote na hasa wana CCM!

Kauli kama hii yaweza kuvuta hisia na kubadili mawazo ya watu kwa haraka sana. Dr Slaa ukumbuke ulivyomsema vizuri Mwakyembe ulikuwa kivutio, ukabadili hisia za watu na kusababisha wana CCM wote wakukubali. Dr Slaa sasa wasifie wana CCM. Toa kauli nzuri kwamba wewe ni mkombozi wa Wana CCM. Adui mkubwa wa CHADEMA ni mafisadi na sio wana CCM. Tafadhali Dr Slaa usisitize jambo hili.

Maana watu wasio na uelewa wanakatana mapanga wakidhani wewe utakuwa rais wa wana CHADEMA na hivi kuwatelekeza wao.
 
Ndugu zangu hebu tujiulize mtu anaye toa rushwa ili mtumishi wa mungu asiseme mambo yanayo wafungua wasio jua kweli huyu ana mapenzi na nchi yetu?
 
"Tunamuomba Mungu leo, tupate viongozi ambao hawajawahi kutuongoza nchi hii; viongozi watakaotuletea amani bila ya kuwepo polisi shirikishi kwa kuwa hapa tulipofika ni matokeo ya kuwapa ushirikiano viongozi wabovu," alisema.


CCM mwaka huu watafulia, hizi ni kampeni makanisani...tatizo letu Watz tunajidai hatuna udini kumbe ndo namba moja!!!
 
angezichukua,angewaita waandishi wa habari na kisha kuzipeleka kituo cha watoto yatima,kuwarudishia hizo pesa wahusika ni kuwajengea mazingira ya kumtafuta mtu mwigine wa kumpa hizo pesa ambazo ni haki yetu,
Hapa umesema mkuu
 
Mmmmh!!! hapo najiuliza maswali na sipati majibu, kama SIJAKOSEA NAZANI KATI YA VIONGOZI WA DINI WALIOONGEA LAST WEEK NI MOKIWA ALIESEMA "HELA ZAO TULE LAKINI TUSIWAPE WATOA HELA KURA" sasa yeye angechukua alafu atoe mbele ya kanisa wakati alipokua akielezea hao waliomletea ilo donge NONO..

ILA BIG UP KWA MOKIWA


:A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 
Jamani nikumbusheni, ni kiongozi gani wa dini aliyewaambia waumini siku chache zilizopita kuwa " Pesa chukueni lakini msiwachague"
 
Hapo Mokiwa umefanya kazi njema machoni pa Bwana na kati ya Waana wa Taifa hili...

Swali: Je Mtuhumiwa sio kuwa anatajwa? Maana hajakiri mwenyewe kama kaungama ndio ungesamehe, lakini hajaungama, mbona usimtaje? Na kama walitaka baada ya muda si mrefu wakuunganishie kwa 'Takukuru yao feki' huoni hiyo ingekuwa mlipuko wa bomu kwa jamii yote na hasa viongozi wa dini kudakwa na rushwa??

Jamaa hao Watajwe, wakamatwe!!
 
Askofu Mokiwa, Angetusaidia sana kwa kuwanasa hao wafuasi wa Mafisadi kwa kuwataja majina, ili wawateje walio watuma. Kwa kuwarejeshea pesa zao, Askofu ameteleza, amewachia memo mbwa mwitu waendele kuwatafuna kondoo wa bwana. Kwani watawafuata maskofu wengine na kuwanyamazisha kwa vijisenti.

Simskii Nabii Mwingira na cheche zake. Unaweza kuta wamemnyamazisha
 
Mmhhh, yaogopesha! naamini vingozi wapo for their personal interest, not for people.
 
Back
Top Bottom