Askofu Kilaini: Nitazirejesha fedha za Rugemalira

Askofu Kilaini: Nitazirejesha fedha za Rugemalira

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,492
Reaction score
39,970
"Kwa kweli sikujua kama hizi fedha zina wingu zito juu yake. Mimi nilipokea nikiamini kuwa ni msaada kwa kanisa kama ilivyo misaada mingine kutoka kwa waumini wenye nia ya kuliendeleza kanisa.Kutokana na hali halisi iliyojitokeza, naahidi kuzirejesha maana si fedha halali"

Hayo ni maneno ya Askofu Methodius Kilaini aliyoyatoa jana kwa wanahabari wa gazeti la MTANZANIA JUMAPILI.

Askofu huyo ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa waliolamba mgao wa James Rugemalira ambapo yeye alipewa shilingi za kitanzania milioni themanini, ameahidi kuzirudisha kwa mwenyewe huku akidai kukwazwa kupita kiasi na jambo hilo.
 
Tutaaminije kuwa amezirudisha.?
 
Mbona imemchukua muda mrefu kuelewa huo ukweli? Na hawa ndio viongozi wetu wasomi.
 
Askofu muhimu ni kuwajibika tu kama wenzako..

mambo ya kurusisha pesa sio muhimu..

Kanisa na waumini wake hawana imani na wewe tena.. wanaogopa kutoa sadaka kanisani maana maaskofu wachafu
 
"Kwa kweli sikujua kama hizi fedha zina wingu zito juu yake. Mimi nilipokea nikiamini kuwa ni msaada kwa kanisa kama ilivyo misaada mingine kutoka kwa waumini wenye nia ya kuliendeleza kanisa.Kutokana na hali halisi iliyojitokeza, naahidi kuzirejesha maana si fedha halali"

Hayo ni maneno ya Askofu Methodius Kilaini aliyoyatoa jana kwa wanahabari wa gazeti la MTANZANIA JUMAPILI.

Askofu huyo ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa waliolamba mgao wa James Rugemalira ambapo yeye alipewa shilingi za kitanzania milioni themanini, ameahidi kuzirudisha kwa mwenyewe huku akidai kukwazwa kupita kiasi na jambo hilo.

Kilaini mwongo, sekeseke za Ruge na IPTL, Serikali na Escrow zilikuwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu Sana kabla ya Escrow kuvunjwa na wao kugawiwa pesa hizi, alikuwa na fursa ya kujiridhisha kuhusu source ya hiyo "Sadaka"; asitwambie hakujua, akiri aliingia tamaa ya mshiko. Askofu #bringbackourmoneykilaini .
 
Askofu Kilaini. Pole sana kwa kuweweseka Baba. Jamii ya Kitanzania inataka tu kujua usafi wako. Kama kweli ni sadaka kwa kanisa, hakuna haja ya kurudisha fedha kwa Ruge. Lakini kama ulipewa kwa sababu wewe una mamlaka pale Mkombozi Bank ili kwa namna yoyote usiwe kiwingu katika mchakato wa kutakatisha fedha, Baba hapo uaskofu wako upo mashakani. Umeingia kwenye listi ya maaskofu wachafu wanaoliharibu kanisa takatifu la roma. Katika hili kurudisha si hoja. Tunakuomba wewe mwenyewe kama kiongozi wa kidini, uwaite wana wa TAKUKURU, wakuchunguze ili wao watuambie kama kuna usafi. Vinginevyo utabaki na dhambi moyoni mwako, na uhalali wako wa kubariki na kitakasa wana wa mungu utakuwa haupo, bali utakuwa unafanya viini macho. Kubali kuwajibika ili usamehewe na Bwana. Maana alisema hata dhambi zikiwa nyekundu kama damu, aweza kuzisamehe. Usichelewe Baba.
 
Aache unafiki sadaka au michango ya kanisa itapitiaje kwenye acc yake binafsi?

Kachemsha awadanganye wajinga...
Brother kama hulielewi kanisa katoliki nyamaza. Mapadri wanaruhusiwa kuwa na account binafsi ambayo kupitia account hizo hupata misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nye ya nchi. Ndio maana unakuta kuna baadhi ya mapadri wanaongoza kwa kuleta maendeleo hata wakiamishiwa sehimu ngumu kiasi gani. Hii inatokana na wafadhili wake binafsi wa nje na ndani.
 
Askofu muhimu ni kuwajibika tu kama wenzako..

mambo ya kurusisha pesa sio muhimu..

Kanisa na waumini wake hawana imani na wewe tena.. wanaogopa kutoa sadaka kanisani maana maaskofu wachafu

Au arudishe hela na ajiuzulu. Na hizo hela ili zionakane zimerudi asizirudishe kwa Ruge maana Ruge anazo nyingi sana na ndiyo maana aliamua kuzigawa kama njugu mawe, azipeleke kama msaada kwenye vituo kadhaa vya kulelea watoto yatima ili na wao wapate raha ya hela za nchi yao.
 
Hili suala tayari limeshamfikia Balozi wa Papa hapa nchini.

Ninavyofahamu jinsi wawakilishi wa papa wanavyofanya kazi, hili suala sasa hivi litakuwa kwenye meza ya Papa Francis kule Vatican City.

Subiri tu Methodius Kilaini uitwe Vatican, nakushauri anza kufunga na kufanya maombi.
 
Back
Top Bottom