Askofu Kilaini kahamishwa kisiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Kilaini kahamishwa kisiasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Dec 14, 2009.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,124
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  NOVEMBA 6, 2009 yaani wiki tano zilizopita, Papa Benedict XVI amewateua mapadri wawili kwa wakati mmoja kuwa maaskofu wasaidizi (Auxiliary Bishops) wa jimbo la Toronto nchini Canada na kufanya Toronto iwe na maaskofu wasaidizi wanne.

  Askofu Michael Lacey alikuwa askofu msaidizi wa jimbo hili tangu Mei 3, 1979 hadi alipostaafu Mei 31 1993. Hivyo amekuwa askofu msaidizi kwa zaidi ya miaka 14.

  Wakati Askofu George Gottwald alikuwa askofu msaidizi wa Jimbo la Saint Louis nchini Marekani kwa miaka 27 tangu Juni 23, 1961 hadi Agosti 2, 1988 alipostaafu.

  Askofu Camillo Ruini amekuwa askofu msaidizi wa Jimbo la Reggio Emilia-Guastalla nchini Italia tangu Mei 16, 1983. Januari 17, 1991 Papa John Paul II alimhamisha ili awe Askofu Msaidizi wa Jimbo la Roma.

  Licha ya kuwa askofu msaidizi , Papa John Paul II alimteua Askofu Ruini kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu la nchi ya Italia (Conferenza Episcopale Italiana), jukumu alilotumikia tangu mwaka 1991 hadi 2007. Italia ni nchi pekee ambayo rais wa baraza la maaskofu huchaguliwa na Papa.

  Mwaka huo huo (1991) Askofu Ruini alipewa ukardinali. Kilichoongezeka hapo ni kuanza kuitwa Kardinali Camillo Ruini kwani uaskofu-msaidizi na urais wa baraza la maaskofu vikabaki vilevile.

  Sipendi kujadili wadhifa mwingine aliopewa unaojulikana kama Archpriest (Padri Mkuu). Naamini wapo watakaouona kuwa ni wadhifa mpya, kama waraka ulivyoonekana jambo jipya, na kama uhamisho wa askofu Kilaini unavyoonekana jambo jipya.

  Sifa moja ya huyu askofu msaidizi wa Roma (Kardinali Ruini) ni kwamba ndiye askofu aliyetokea sana kwenye vyombo vya habari nchini Italia. Italia ina maaskofu wengi na makardinali wengi. Lakini bado ndiye aliyeongoza kuwa chanzo cha habari. Ni halali kusema alikuwa msemaji wa kanisa nchini Italia. Amestaafu Juni 27, 2008 na hivyo kutumikia kama Askofu Msaidizi kwa zaidi ya miaka 25 katika majimbo mawili.

  Maaskofu hawa watatu (Lacey, Gottwald na Ruini) wanatuthibitishia kwamba uaskofu-msaidizi si kituo cha kusubiri kupewa jimbo baadaye. Askofu anaweza kuhama majimbo huku akidumu na uaskofu-msaidizi kila anapoenda kama tulivyoona kwa Kardinali Ruini.

  Wote hao watatu, nchini mwao (Canada na Italia), wameshuhudia majimbo mengi yanajazwa na maaskofu wapya huku wao wakidumu kwenye nafasi zao za uaskofu msaidizi hadi walipostaafu.

  Ingekuwa kupata jimbo ni kupanda hadhi (promotion) basi tungesema hawa watatu hawakuwahi kupandishwa hadhi hadi wamestaafu.

  Uaskofu ni sehemu ya kuhudumia. Maaskofu wote duniani wako sawa. Kwani wamekamilisha ngazi zote tatu za sakramenti ya Daraja Takatifu (Holy Orders). Askofu aweza kuitwa vyovyote kama vile askofu msaidizi, askofu wa jimbo, askofu mwandamizi, askofu mkuu, Vicar Apostolic, Titular Bishop na kuendelea.

  Yote yale yanaonyesha majukumu yao kwenye muundo kanisa. Majukumu ambayo askofu anaweza kubadilishwa toka jukumu moja kwenda jingine.

  Niliwahi kuandika makala nikifafanua majukumu hayo. Wakati huo mjadala mwingine ulikuwa ukiendelea kutokana na Papa Benedict XVI kufanya mabadiliko kwenye Jimbo la Same.

  Tulijadili pia maaskofu ambao majukumu yao si lazima wakabidhiwe jimbo lenye waumini. Aina hii tulisema huitwa Titular Bishop. Kwamba askofu msaidizi kama Method Kilaini ni askofu wa aina hii.

  Tuliona kila Titular Bishop hupewa jimbo linaloitwa Titular See na kwamba la askofu Kilaini linaitwa Strumnitza. Hivyo unaweza kumuita "Askofu wa Strumnitza" au "Titular Bishop of Strumnitza". Ilikuwa ni makala ndefu inatosha kuikumbusha kwa ufupi huo. Tuendelee na hoja yetu kuhusu Askofu Method Kilaini aliyehamishiwa Bukoba.

  Tunaambiwa na baadhi kuwa hii ni mara ya kwanza kwa nafasi ya askofu msaidizi kwenda nje ya D'Salaam. Je, ni kweli?

  Hayati Renatus Butibubage alikuwa Askofu Msaidizi wa jimbo la Mwanza tangu Desemba 19, 1959 hadi Januari 15, 1966 alipoteuliwa kuwa askofu wa jimbo hilo hadi alipostaafu Novemba 18, 1987.

  Hayati James Joseph Komba alikuwa Askofu Msaidizi wa Peramiho tangu Desemba 22, 1961 hadi Feb 6, 1969 siku ambayo Peramiho ilibadilishwa jina kuwa jimbo la Songea na yeye akateuliwa kuwa askofu wa jimbo hilo hadi alipofariki Februari 01, 1992.

  Hayati Bernard Mabula alikuwa Askofu Msaidizi wa Tabora tangu Januari 09, 1969 hadi Machi 25, 1972 alipoteuliwa na kuwa askofu wa Singida hadi alipostaafu Aprili 19, 1999.

  Hayati Elias Mchonde alikuwa Askofu Msaidizi wa D'Salaam tangu Machi 24, 1956 hadi Aprili 21, 1964 alipoteuliwa na kuwa askofu wa Mahenge hadi alipofariki dunia Juni 13, 1969.

  Placidus Nkalanga alikuwa Askofu Msaidizi wa Bukoba tangu Aprili 18, 1961 hadi Machi 06, 1969 alipoteuliwa na kuwa askofu wa jimbo hilo hadi alipostaafu Novemba 26 1973.

  Hayati Christopher Mwoleka amekuwa Askofu Msaidizi wa Rulenge tangu Machi 06, 1969 hadi Juni 26, 1969 alipoteuliwa na kuwa askofu wa jimbo hilo hadi alipostaafu Novemba 08, 1996.

  Padri Method Kilaini aliteuliwa kuwa askofu msaidizi wa D'Salaam Desemba 22, 1999. Siku hiyo inatukumbusha nini? Moja ni kwamba Method Kilaini anakuwa mzalendo wa saba kuwa askofu-msaidizi hapa nchini. Pili, ni kama kwamba amerudisha wadhifa wa uaskofu msaidizi ulioikimbia Tanzania kwa miaka 18.

  Pia kuna uaskofu-mwandamizi (Coadjutor bishop) ambao majukumu yake hufanana sana na uaskofu msaidizi. Tofauti kubwa kati yao ni kwamba mwandamizi ana haki ya kurithi jimbo wakati msaidizi hana haki hiyo (Rejea: Sheria za Kanisa, Can. 403).

  Maaskofu waandamizi (Coadjutor Bishop) waliowahi kurithi jimbo ni askofu Polycarp Pengo, aliyerithi Jimbo la D'Salaam mwaka 1992 siku alipostaafu Kardinali Laurian Rugambwa. Askofu Castor Msemwa alirithi Jimbo la Tunduru-Masasi mnamo Agosti 5, 2005 siku alipostaafu askofu Magnus Mwalunyungu. Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa hakurithi Jimbo la Sumbawanga, alipata uhamisho wa kwenda Iringa ambako ni askofu wa jimbo hilo hadi leo.

  Hivyo, si rahisi kusema askofu Method Kilaini atarithi Jimbo la Bukoba kwa sababu Askofu Nestorius Timanywa anafikisha miaka 75 Mei 07, 2012 na hivyo kutakiwa kuomba kustaafu {Rejea: Sheria za Kanisa, Can. 401(1)}. Tungesema hivyo kama angepelekwa huko kama askofu mwandamizi.

  Sasa tujadili baadhi ya hoja zinazojitokeza kwenye mijadala kuhusu Askofu Kilaini. Kuna dhana kuwa yale majimbo makuu (archdiocese) yana hadhi tofauti na yale majimbo mengine. Ni yale ambayo pia huitwa "majimbo" na wengine huridhika kuyaita "majimbo madogo". Kwa Kiingereza huitwa (suffragan diocese).

  Ukikubali neno "majimbo madogo" basi utakubali kuwa Method Kilaini anatoka D'Salaam ambalo ni jimbo kuu (archdiocese) anakwenda Bukoba ambalo ni "jimbo dogo".

  Historia kuhusu majimbo makuu (archdiocese) ni makala ndefu inayojitosheleza. Yatosha kusema ni vizuri kusoma kanuni nne za Sheria za Kanisa yaani 435 hadi 438 (au Can. 435-43).

  Leo hii Jimbo la Bukoba likitangazwa kuwa jimbo kuu (Archdiocese of Bukoba), mabadiliko hayo yatamgusa Askofu Nestory Timanywa tu ambaye sasa atakuwa askofu mkuu (archbishop).

  Askofu Kilani yaani askofu Msaidizi ataendelea kuwa hivyohivyo, yaani Auxiliary Bishop of Bukoba. Tahadhari! Askofu Mwandamizi, yeye atabadilika na kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Bukoba (Coadjutor Archbishop of Bukoba).

  Hivyo hata ile dhana ya kupanda (promotion) ingekuwa kweli askofu msaidizi anabaki hivyohivyo hata ahamie Jimbo la Roma kwa wadhifa huohuo. Kwa Kiingereza, mara nyingi neno "See" hutumika badala ya neno diocese (jimbo) au archdiocese (jimbo kuu).

  Kuna swali linaulizwa kuwa ni askofu gani mpya atakayeziba nafasi ya Method Kilaini pale Dar? Mwenye swali akisoma makala hii aweza kulibadili na kuuliza, kwa nini maaskofu wasaidizi nafasi zao hazizibwi?

  Sheria ya Kanisa {Can. 406(2)} inamtaka askofu wa jimbo kumpa Askofu Msaidizi jukumu linaloitwa Vicar General au umakamu wa askofu. Katika mazingira hayo ni rahisi kudhani kwamba D'Salaam haikuwa na Vicar General kipindi chote cha uaskofu wa Kilaini.

  Haitashangaza hali hiyo kuhamia Bukoba alikoenda Method Kilaini. Vilevile haitashangaza kwa D'Salaam kumtangaza padri mmoja kuwa Vicar General au makamu wa askofu.

  Hoja yangu ya mwisho kuijadili leo ni dhana kwamba Askofu Kilaini amemzidi Kardinali Polycarp Pengo kutokea sana kwenye vyombo vya habari. Je, tumetafiti chanzo cha hali hii kama ni kweli? Mimi naitafakari kama ifuatavyo:

  Nimeanza makala hii nikimtaja makusudi Kardinali Camillo Ruini aliyekuwa askofu msaidizi wa Jimbo la Roma.

  Isingekuwa umaarufu wa Papa duniani basi huenda angemzidi hata Papa, kwa kuwa chanzo cha habari licha ya kwamba wote wako jimbo la Roma lililoko nchini Italia.

  Je, Kardinali Polycarp Pengo anaijua hali hiyo, kwamba moto wa yeye kuwa chanzo cha habari si mkubwa kiasi kile? Kama anaijua, ni nini maoni yake kuhusu hali hiyo?

  Tuyaone maoni yake (Pengo) alipojibu swali aliloulizwa na jopo la Padri Stephano Kaombe na Ndg. Paschal Maziku. Hawa wawili walimuhoji Kardinali Pengo maswali kumi na nane wakayakusanya kwenye kitabu kidogo kilichoitwa KUISHI KWANGU NI KRISTO. Kitabu hicho kilitolewa rasmi kwa ajili ya kumbukumbu ya jubilei ya fedha ya uaskofu wa Mwadhama Polycarp Pengo.

  Swali la 15 lililoko ukurasa wa 22 anaulizwa hivi: "Kuna tetesi kwamba umeanza kupunguza moto katika kukemea mapungufu, hasa katika masuala ya kitaifa, je, ni kweli?"

  Mwadhama Pengo aligawanya jibu lake katika aya tatu. Aya ya kwanza alikiri kusikia madai hayo. Lakini akaeleza pia hushtuka kusikia wanaosema wamehojiana naye wakati hata sura zao hazijui.

  Aya ya pili ameeleza hana uhakika kama kweli amepunguza "Sauti yake ya unabii", lakini pia akataja majukumu yanayomtinga ambayo ni kuongoza jimbo, urais wa SECAM, na ujumbe wa idara tatu za Vatican.

  Aya ya tatu ameeleza kwamba anaona kama maoni ya taifa yako mikononi mwa vyombo vya habari. Kwamba vyombo vya habari vinaandika habari zile ambazo wanazipenda.

  Ni kitabu kizuri chenye utangulizi wa Katibu wa Baraza la Maskofu, Padri Anthony Makunde, kinapatikana kwenye duka liitwalo Paulines Media lililoko kwenye Kanisa Kuu la St. Joseph jijini D'Salaam.

  Je, kwa hali hiyo tumtegemee vipi kila mara awe na waandishi wakati mwenyewe anakiri wingi wa kazi alio nao?

  Kwa hali hiyo, kwenye jimbo lenye askofu msaidizi, na kinachotafutwa ni kauli ya kanisa jimboni, kuna sababu gani zinazozuia asitafutwe Askofu Method Kilaini kufafanua? Ni mara ngapi Askofu Kilaini ameitisha mkutano wa waandishi wa habari (press conference) ili kueleza masuala ya kanisa au mengine?

  Kama Askofu Kilaini anapatikana, je, kuna chochote kinachokwamisha kuwapata Askofu Ngonyani wa Lindi, Askofu Maluma wa Njombe, Askofu Minde wa Kahama, Askofu Kinyaia wa Mbulu au Askofu Dalu wa Geita?

  Je, hao maaskofu watano niliowataja, tumewatumia vipi kama chanzo cha habari kama alivyotumika Askofu Kilaini?

  Kama mtu ulikuwa nje ya nchi na husomi magazeti ya hapa, halafu siku ya kurudi usimuliwe mjadala wa waraka ulivyokuwa, kisha uambiwe idara anayoongoza Askofu Paul Ruzoka kwenye Baraza la Maaskofu, Basi haishangazi iwapo utafikiri kwamba Jimbo la Tabora aliko Askofu Ruzoka liliongoza kuwa chanzo cha habari kipindi chote cha waraka. Kwamba hata angezima simu ingeripotiwa kwamba "simu ya askofu imetafutwa bila mafanikio".

  Je, tunaonaje tunapokuta tumelifanya jimbo moja au askofu mmoja kama chanzo cha habari? Je, huu si mwanzo wa kukosa tunu zilizojaa kwenye majimbo mengine?

  Sasa Askofu Kilaini anaenda Bukoba, hivi kama ni kweli ndiyo tabia yake kuwasiliana halafu anasikika, je, hilo litamshinda akiwa hukohuko Bukoba? Ni mawasiliano gani ambayo hayafiki au hayasikiki Bukoba?

  Tembelea mwenyewe tovuti ifuatayo (http://kiongozi.tripod.com). Utaona maneno yameandikwa (Last Updated on July 12, 2000 by Norbert Kija and Method Kilaini with help from Miss. Christina Nyambo).

  Dalili kwamba ujuzi wa kutunza taarifa kwenye mtandao au kucheza na mitandao anao hata hajawa askofu. Dalili pia kwamba tangu ajikite na shughuli za uaskofu jimboni D'Salaam basi tovuti ile ikapunguza kasi ya kutunza habari mpya.

  Chanzo: Tanzania Daima
   
 2. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sina muda wa kusoma habari za Tanzania daima,gazeti limekaa kiudaku kuliko gazeti la Ijumaa na Risasi.
   
 3. K

  Kieleweke Member

  #3
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana mwenzetu ulifundishwa kwamba research ndiyo udaku na udaku ndiyo research?
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hizi ni speculation tu za kigazeti hiki lakini hakuna lolote lenye ukweli. Askofu kilaini mwenyewe alishaomba kuhamia bukoba alikuwa akisubiri ruhusa ya baba mtakatifu.
   
 5. K

  Kieleweke Member

  #5
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni udaku gani ambao wewe huupendi maana huu mwekundu ni udaku pia?Ni speculation zipi ambao wewe huzipendi maana hii ya kijani ni speculation pia? Fafanua.
   
 6. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #6
  Dec 14, 2009
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Mtapoteza muda wenu buree,uteuzi wa ki kanisa ni tofaut na wa kisiasa kabsaaaaa
  Achen kanisa lifanye mambo yake
   
 7. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Novemba 6, 2009 yaani wiki tano zilizopita, Papa Benedict XVI amewateua mapadri wawili kwa mpigo kuwa maaskofu wasaidizi (Auxiliary Bishops) wa jimbo la Toronto nchini Kanada na kufanya Toronto iwe na maaskofu wasaidizi wanne.

  Askofu Michael Lacey allikuwa askofu msaidizi wa jimbo hili tangu Mei 3, 1979 hadi alipostaafu Mei 31 1993. Hivyo amekuwa askofu msaidizi kwa zaidi ya miaka 14.

  Wakati Askofu George Gottwald alikuwa askofu msaidizi wa jimbo la Saint Louis nchini Marekani kwa miaka 27 tangu Juni 23, 1961 hadi Agosti 2, 1988 alipostaafu.

  Askofu Camillo Ruini amekuwa askofu msaidizi wa jimbo la Reggio Emilia-Guastalla nchini Italia tangu Mei 16, 1983. Januari 17, 1991 Papa John Paul II alimhamisha ili awe Askofu Msaidizi wa jimbo la Roma.

  Licha yakuwa askofu msaidizi , Papa John Paul II alimteua Askofu Ruini kuwa Rais wa Baraza la maaskofu la nchi ya Italia (Conferenza Episcopale Italiana), jukumu alilotumikia tangu mwaka 1991 hadi 2007. Italia ni nchi pekee ambayo rais wa baraza la maaskofu huchaguliwa na Papa.

  Mwaka huohuo (1991) Askofu Ruini alipewa ukadinali. Kilichoongezeka hapo ni kuaza kuitwa Kadinali Camillo Ruini kwani uaskofu-Msaidizi na urais wa baraza la maaskofu vikabaki vilevile.

  Sipendi kujadili wadhifa mwingine aliopewa unaojulikana kama Archpriest (Padri Mkuu). Naamini wapo watakaouona kuwa ni wadhifa mpya, kama waraka ulivyoonekana jambo jipya, na kama uhamisho wa askofu Kilaini unavyoonekana jambo jipya.

  Sifa moja ya huyu askofu msaidizi wa Roma (Kadinali Ruini) ni kwamba ndiye askofu aliyetokea sana kwenye vyombo vya habari nchini Italia. Italia ina maaskofu wengi na makadinali wengi. Lakini bado ndiye aliyeongoza kuwa chanzo cha habari. Ni halali kusema alikuwa msemaji wa kanisa nchini Italia. Amestaafu Juni 27 2008 na hivyo kutumikia kama Askofu Msaidizi kwa zaidi ya miaka 25 katika majimbo mawili.

  Maaskofu hawa watatu (Lacey, Gottwald na Ruini) wanatuthibitishia kwamba uaskofu-msaidizi si kituo cha kusubiri kupewa jimbo baadaye. Askofu anaweza kuhama majimbo huku akidumu na uaskofu-msaidizi kila anapoenda kama tulivyoona kwa Kadinali Ruini.

  Wote hao watatu, nchini mwao (Kanada na Italia), wameshuhudia majimbo mengi yanajazwa na maaskofu wapya huku wao wakidumu kwenye nafasi zao za uaskofu msaidizi hadi walipostaafu.

  Ingekuwa kupata jimbo ni kupanda hadhi (promotion) basi tungesema hawa watatu hawakuwahi kupandishwa hadhi hadi wamestaafu.

  Uaskofu ni sehemu ya kuhudumia. Maaskofu wote duniani wako sawa. Kwani wamekamilisha ngazi zote tatu za sakramenti ya Daraja Takatifu (Holy Orders). Askofu aweza kuitwa vyovyote kama vile askofu Msaidizi, askofu wa jimbo, askofu mwandamizi, askofu mkuu, Vicar Apostolic, Titular Bishop na kuendelea.

  Yote yale yanaonyesha majukumu yao kwenye muundo kanisa. Majukumu ambayo askofu anaweza kubadilishwa toka jukumu moja kwenda jingine.

  Niliwahi kuandika makala nikifafanua majukumu hayo. Wakati huo mjadala mwingine ulikuwa ukiendelea kutokana na Papa Benedict XVI kufanya mabadiliko kwenye jimbo la Same.

  Tulijadili pia maaskofu ambao majukumu yao si lazima wakabidhiwe jimbo lenye waumini. Aina hii tulisema huitwa Titular Bishop. Kwamba askofu msaidizi kama Method Kilaini ni askofu wa aina hii.

  Tuliona kila Titular Bishop hupewa jimbo linaloitwa Titular See na kwamba la askofu Kilaini linaitwa Strumnitza. Hivyounaweza kumuita “Askofu wa Strumnitza” au “Titular Bishop of Strumnitza”. Ilikuwa ni makala ndefu inatosha kuikumbusha kwa ufupi huo. Tuendelee na hoja yetu kuhusu Askofu Method Kilaini aliyehamishiwa Bukoba.

  Tunaambiwa na baadhi kuwa hii ni mara ya kwanza kwa nafasi ya askofu msaidizi kwenda nje ya D’Salaam. Je, ni kweli?

  Hayati Renatus Butibubage alikuwa Askofu Msaidizi wa jimbo la Mwanza tangu Disemba 19, 1959 hadi Januari 15, 1966 alipoteuliwa kuwa askofu wa jimbo hilo hadi alipostaafu Novemba 18, 1987.

  Hayati James Joseph Komba alikuwa Askofu Msaidizi wa Peramiho tangu Disemba 22 1961 hadi Feb 6, 1969 siku ambayo Peramiho ilibadilishwa jina kuwa jimbo la Songea na yeye akateuliwa kuwa askofu wa jimbo hilo hadi alipofariki Februari 01, 1992.

  Hayati Bernard Mabula alikuwa Askofu Msaidizi wa Tabora tangu Januari 09, 1969 hadi Machi 25, 1972 alipoteuliwa na kuwa askofu wa Singida hadi alipostaafu Aprili 19, 1999.

  Hayati Elias Mchonde alikuwa Askofu Msaidizi wa D'Salaam tangu Machi 24, 1956 hadi Aprili 21, 1964 alipoteuliwa na kuwa askofu wa Mahenge hadi alipofariki Juni 13, 1969.

  Placidus Nkalanga alikuwa Askofu Msaidizi wa Bukoba tangu Aprili 18, 1961 hadi Machi 06, 1969 alipoteuliwa na kuwa askofu wa jimbo hilo hadi alipostaafu Novemba 26 1973.

  Hayati Christopher Mwoleka amekuwa Askofu Msaidizi wa Rulenge tangu Machi 06, 1969 hadi Juni 26, 1969 alipoteuliwa na kuwa askofu wa jimbo hilo hadi alipostaafu Novemba 08, 1996.

  Padri Method Kilaini aliteuliwa kuwa askofu msaidizi wa D’Salaam tarehe 22, Disemba 1999. Siku hiyo inatukumbusha nini? Moja ni kwamba Method Kilaini anakuwa mzalendo wa saba kuwa askofu-msaidizi hapa nchini. Pili ni kama kwamba amerudisha wadhifa wa uaskofu msaidizi ulioikimbia Tanzania kwa miaka 18.

  Pia kuna uaskofu-mwandamizi (Coadjutor bishop) ambao majukumu yao hunafanana sana na uaskofu msaidizi. Tofauti kubwa kati yao ni kwamba mwandamizi ana haki ya kurithi jimbo wakati msaidizi hana haki hiyo (Rejea: Sheria za Kanisa, Can. 403).

  Maaskofu waandamizi (Coadjutor Bishop) waliowahi kurithi jimbo ni askofu Polycarp Pengo aliyerithi jimbo la D’Salaam mwaka 1992 siku alipostaafu Kadinali Laurian Rugambwa. Askofu Castor Msemwa alirithi jimbo la Tunduru-Masasi mnamo Agosti 5, 2005 siku alipostaafu askofu Magnus Mwalunyungu. Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa hakurithi jimbo la Sumbawanga alipata uhamisho wa kwenda Iringa ambako ni askofu wa jimbo hilo hadi leo.

  Hivyo, si rahisi kusema askofu Method Kilaini atarithi jimbo la Bukoba kwa sababu askofu Nestorius Timanywa anafikisha miaka 75 hapo Mei 07, 2012 na hivyo kutakiwa kuomba kustaafu {Rejea: Sheria za Kanisa, Can. 401(1)}. Tungesema hivyo kama angepelekwa huko kama askofu mwandamizi.

  Sasa tujadili baadhi ya hoja zinazojitokeza kwenye mijadala kuhusu Askofu Kilaini. Kuna dhana kuwa yale majimbo makuu (archdiocese) yana hadhi tofauti na yale majimbo mengine. Ni yale ambayo pia huitwa majimbo” na wengine huridhika kuyaita “majimbo madogo”. Kwa kiingereza huitwa (suffragan diocese).

  Ukikubali neno “majimbo madogo” basi utakubali kuwa Method Kilaini anatoka D’Salaam ambalo ni jimbo kuu (archdiocese) anakwenda Bukoba ambalo ni “jimbo dogo”.

  Historia kuhusu majimbo makuu (archdiocese) ni makala ndefu inayojitosheleza. Yatosha kusema ni vizuri kusoma kanuni nne za Sheria za Kanisa yaani 435 hadi 438 (au Can. 435-438).

  Leo hii jimbo la Bukoba likitangazwa kuwa jimbo kuu (Archdiocese of Bukoba), mabadiliko hayo yatamgusa askofu Nestory Timanywa tu ambaye sasa atakuwa askofu mkuu (archbishop). Askofu Kilani yaani askofu Msaidizi ataendelea kuwa hivyohivyo yaani Auxiliary Bishop of Bukoba. Tahadhari! Askofu Mwandamizi, yeye atabadilikia na kuwa Askofu Mkuu mwandamizi wa Bukoba (Coadjutor Archbishop of Bukoba).

  Hivyo hata ile dhana ya kupanda (promotion) ingekuwa kweli askofu msaidizi anabaki hivyohivyo hata ahamie jimbo la Roma kwa wadhifa huohuo. Kwa kiingereza mara nyingi neno “See” hutumika badala ya neno diocese (jimbo) au archdiocese (jimbo kuu).

  Kuna swali linaulizwa kuwa ni askofu gani mpya atakayeziba nafasi ya Method Kilaini pale Dar? Mwenye swali akisoma makala hii aweza kulibadili na kuuliza, kwa nini maaskofu wasaidizi nafasi zao hazizibwi?

  Sheria ya Kanisa {Can. 406(2)} inamtaka askofu wa jimbo kumpa Askofu Msaidizi jukumu linaloitwa Vicar General au umakamu wa askofu. Katika mazingira hayo ni rahisi kudhani kwamba D’Salaam haikuwa na Vicar General kipindi chote cha uaskofu wa Kilaini.

  Haitashangaza hali hiyo kuhamia Bukoba alikoenda Method Kilaini. Vilevile haitashangaza kwa D’Salaam kumtangaza padri mmoja kuwa Vicar General au makamu wa askofu..

  Hoja yangu ya mwisho kuijadili leo ni dhana kwamba askofu Kilaini amemzidi Kadinali Polycarp Pengo kutokea sana kwenye vyombo vya habari. Je, tumetafiti chanzo cha hali hii kama ni kweli? Mimi naitafakari kama ifuatavyo.

  Nimeanzamakala hii nikimtaja makusudi Kadinali Camillo Ruini aliyekuwa askofu msaidizi wa jimbo la Roma. Isingekuwa umaarufu wa Papa duniani basi huenda angemzidi hata Papa kwa kuwa chanzo cha habari licha ya kwamba wote wako jimbo la Roma lililoko nchini Italia.

  Je Kadinali Polycarp Pengo anaijua hali hiyo, kwamba moto wa yeye kuwa chanzo cha habari si mkubwa kiasi kile? Kama anaijua, ni nini maoni yake kuhusu hali hiyo?

  Tuyaone maoni yake (Pengo) alipojibu swali aliloulizwa na jopo la Padri Stephano Kaombe na Ndg. Paschal Maziku. Hawa wawili walimuhoji Kadinali Pengo maswali kumi na nane wakayakusanya kwenye kitabu kidogo kilichoitwa KUISHI KWANGU NI KRISTO. Kitabu hicho kilitolewa rasmi kwa ajili ya kumbukumbu ya jubilei ya fedha ya uaskofu wa Mwadhama Polycarp Pengo.

  Swali la 15 lililoko ukurasa wa 22 anaulizwa hivi: “Kuna tetesi kwamba umeanza kupunguza moto katika kukemea mapungufu, hasa katika masuala ya kitaifa, je ni kweli?”.

  Mwadhama Pengo aligawanya jibu lake katika aya tatu.. Aya ya kwanza alikiri kusikia madai hayo. Lakini akaeleza pia hushtuka kusikia wanaosema wamehojiana naye wakati hata sura zao hazijui.

  Aya ya pili ameeleza hana uhakika kama kweli amepunguza “Sauti yake ya unabii” , lakini pia akataja majukumu yanayomtinga ambayo ni kuongoza jimbo, urais wa SECAM, na ujumbe idara tatu za Vatican.

  Aya ya tatu ameeleza kwamba anaona kama maoni ya taifa yako mikononi mwa vyombo vya habari. Kwamba vyombo vya habari vinaandika habari zile ambazo wanazipenda.

  Ni kitabu kizuri chenye utangulizi wa Katibu wa Baraza la Maskofu, Padri Anthony Makunde kinapatikana kwenye duka liitwalo Paulines Media lililoko kwenye Kanisa Kuu la St. Joseph jijini D’Salaam.

  Je, kwa hali hiyo tumtegemee vipi kila mara awe na waandishi wakati mwenyewe anakiri wingi wa kazi alio nao? Kwa hali hiyo, kwenye jimbo lenye askofu msaidizi, na kinachotafutwa ni kauli ya kanisa jimboni, kuna sababu gani zinazozuia asitafutwe askofu Method Kilaini kufafanua?

  Ni mara ngapi askofu Kilaini ameitisha mkutano wa waandishi wa habari (press conference) ili kueleza masuala ya kanisa au mengine?

  Kama askofu Kilaini anapatikana, je kuna chochote kinachokwamisha kuwapata askofu Ngonyani wa Lindi, askofu Maluma wa Njombe, askofu Minde wa Kahama, askofu Kinyaia wa Mbulu au askofu Dallu wa Geita.

  Je, hao maaskofu watano niliowataja, tumewatumia vipi kama chanzo cha habari kama alivyotumika Askofu Kilaini?

  Kama mtu ulikuwa nje ya nchi na husomi magazeti ya hapa, halafu siku ya kurudi usimuliwe mjadala wa waraka ulivyokuwa, kisha uambiwe idara anayoongoza askofu Paul Ruzoka kwenye Baraza la Maaskofu. Basi haishangazi iwapo utafikiri kwamba jimbo la Tabora aliko askofu Ruzoka liliongoza kuwa chanzo cha habari kipindi chote cha waraka. Kwamba hata angezima simu ingeripotiwa kwamba “simu ya askofu imetafutwa bila mafanikio”.

  Je, tunaonaje tunapojkuta tumelifanya jimbo moja au askofu mmoja kama chanzo cha habari? Je, huu si mwanzo wa kukosa tunu zilizojaa kwenye majimbo mengine.

  Sasa Askofu Kilaini anaenda Bukoba, hivi kama ni kweli ndiyo tabia yake kuwasiliana halafu anasikika, je, hilo litamshinda akiwa hukohuko Bukoba? Ni mawasiliano gani ambayo hayafiki au hayasikiki Bukoba?

  Tembelea mwenyewe tovuti ifuatayo (http://kiongozi.tripod.com). Utaona maneno yameandikwa (Last Updated on July 12, 2000 by Norbert Kija and Method Kilaini with help from Miss. Christina Nyambo)

  Dalili kwamba ujuzi wa kutunza taarifa kwenye mtandao au kucheza na mitandao anao hata hajawa askofu. Dalili pia kwamba tangu ajikite na shughuli za uaskofu jimboni D’Salaam basi tovuti ile ikapunguza kasi ya kutunza habari mpya.

  Source: Tanzania Daima Jumapili
   
 8. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  Splendid ANALYSIS!

  Huyu ni Magobe T nini? maana hii analysis you can only get it through these catholic chaps.

  Again, thanks kwa haya maelezo. Nilikuwa natamani yasiishe. Ni very precise and educative. Asante sana mwandishi na ubarikiwe sana.

  Wacha wanaotaka kulink kila kitu na siasa njaa zetu za akina Makamba!

  Masanja,
   
 9. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huyu mwandishi makini anafanya utafiti wa hali ya juu. Anajua mambo mengi sana kuhusu kanisa katoliki. Ni Engineer yuko TTCL.
   
 10. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huo mtiririko umenifurahisha.
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  ALIYEKUWA Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Method Kilaini amesema uhamisho wake kwenda Jimbo la Bukoba, hauna uhusiano na siasa wala mkono wa Rais Jakaya Kikwete.

  Amesema ni uhamisho wa kawaida, tena wa kichungaji ambao hata hivyo umechelewa kutolewa kwa sababu kwa mujibu wa hadhi yake kikanisa ya Askofu wa Strumizza, alipaswa asikae kwa zaidi ya miaka mitano katika jimbo moja.

  Yeye amekaa Dar es Salaam akiwa Askofu Msaidizi kwa miaka tisa na nusu; na wiki moja iliyopita Baba Mtakatifu Benedict wa XVI alitangaza kumhamishia katika Jimbo la Bukoba.

  Askofu Kilaini akizungumza jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay, Dar es Salaam, alisema amesikia mengi wakati akiwa hija ya siku nane nchini Israel kuhusu uhamisho wake, kiasi cha kuhusishwa na mambo ya kisiasa, lakini alisema kwa asilimia 100, hayo hayana ukweli wowote.

  “Nimeelezwa mengi yamesemwa, ila ukweli ni kwamba nimehamishwa kwa utaratibu wa kawaida wa kanisa, mimi ni mchungaji na kwa hadhi yangu ni tofauti na Askofu aliyekabidhiwa Jimbo, hivyo naweza kupelekwa kokote na wakati wowote,” alisema Kilaini ambaye alirejea nchini jana asubuhi akitokea Israel.

  Alisema hadhi yake hiyo ya Usaidizi inayoitwa kikanisa Strumizza, iko Macedonia na maaskofu wachache wanayo ambapo inafanana na ya Balozi wa Baba Mtakatifu nchini ambaye anatumwa kokote na anapaswa kutii na kwenda.

  Kuhusu habari zilizoandikwa na gazeti moja la wiki siku kadhaa zilizopita zikihusisha uhamisho wake na kuwa karibu na Rais Kikwete ambaye anadaiwa alishiriki kumlipia matibabu nchini India Septemba 2007, Kilaini alisema habari hizo ni uvumi na uzushi na hazina ukweli hata kidogo.

  “Nimepelekwa India kwa matibabu na masista (watawa) wa Shirika la DMI ambao pia ni wamiliki wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kule Luguruni, Kibamba (Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam), hivyo kusema kuwa Rais Kikwete alinipeleka, ni uongo wenye lengo la uchonganishi,” alisema Kilaini na kuongeza:

  “Unajua sisi viongozi wa dini ni wachungaji, dini si chama cha siasa, kazi yetu kubwa ni kuchunga kondoo na hatuchagui kondoo, serikali ikifanya vizuri tunaipongeza na ikikosea tunaigonga ili ijirekebishe…sasa nikimpongeza Kikwete wapinzani wananisema na wanasema nipo karibu naye.”

  Alisema uongozi wa Kikwete umetoa fursa kwa watu kuanika uchafu wote hadharani, tena uchafu ambao yeye (Kikwete) ameukuta alipoingia madarakani, hivyo nafasi hiyo wengine wameitumia vibaya na kumlaumu yeye (Rais) badala ya kuitumia fursa hiyo kukosoa na kuleta maendeleo.

  Kilaini, huku akitoa mifano kadhaa ambayo hakupenda iandikwe gazetini, alisema mara nyingi amekuwa akiikosoa serikali inapokosea na amekuwa akiipongeza inapofanya vizuri na kwamba kama hakuzungumza binafsi, basi yote aliyokuwa akisema yaliwahusisha maaskofu wa kanisa hilo.

  “Sikuwa nazungumza tu kama wengine wanavyodhani, nilikuwa naagizwa na wenzangu maana walikuwa wanasikia kutoka katika vyombo vyenu hivyo hivyo, kanisa lina mfumo wa kazi, hatukurupuki kama wengine wanavyodhani,” alifafanua kiongozi huyo maarufu wa Kanisa Katoliki nchini na kuongeza:

  “Lakini kuna wakati nilisema kama mimi binafsi maana ni Mtanzania na Katiba inaniruhusu kusema.” Kilaini, ambaye alisema kwamba kicheo yeye ni mtu mdogo sana, alijibu swali hilo baada ya mwandishi kutaka ufafanuzi wake kwani mara nyingi alionekana kama msemaji wa TEC wakati kuna Katibu na Rais wa Baraza hilo.

  Alisema kanisa lina utaratibu wa kutoa uamuzi au azimio rasmi la kila kinacholihusu, lakini mara nyingi alipaswa kulitolea ufafanuzi suala husika kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuhusu ukweli wa jambo wakati taarifa rasmi ikiandaliwa, ingawa alidai mengi yalikuwa yakipotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari.

  Kilaini aliyetumia mahojiano na gazeti hili kuwaomba msamaha wananchi wa Dar es Salaam pale alipowakwaza au kukosea kwa kuwa ni binadamu, alivitaka vyama vya upinzani kuipa serikali changamoto zenye kujenga badala ya kuhubiri siasa za chuki ingawa alikubaliana nao kwamba ni mara chache wanaweza kuisifu serikali iliyoko madarakani.

  Alisema kama mchungaji, ametekeleza wajibu wake kwa waumini na wasio waumini wa Dar es Salaam kwani kabla ya kuwa Askofu na kuteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, amekuwa Katibu wa TEC kwa miaka tisa.

  Kuhusu uhamisho, alisema alifahamu kabla hajakwenda hija na anashukuru kupata nafasi ya kurudisha fadhila kwa Jimbo lake ambalo aliondoka zaidi ya miaka 30 iliyopita na kuongeza kuwa Jimbo la Dar es Salaam ni gumu hivyo linahitaji Msaidizi ingawa ni uamuzi wa Baba Mtakatifu na Kardinali Polycarp Pengo.  Source: Gazeti la Habari Leo
   
 12. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  As far as I know, the article was not a news story, it was a feature. A news story is about an event that happened (asnwering the 5Ws + an H: Who, what, when, why and how an even happened). A feature could be an opinion of a writer or even a reseach article.
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  muwe mnachekecha habari ninyi watu wa CUT-AND-PASTE!

  au jifunzeni namna ya ku-present thread kwa staili nzuri kidogo ili ijadilike

  nilidhani mtu angerusha thread akiulizia SHERIA ZA KANISA KATOLIKI zinatumika kumsimika askofu mkuu,askofu msaidizi(kama kilaini),na mwadhama kardinali.

  watu wengi waliamini kwamba kilaini ATAMRITHI PENGO!polen sana.fuatilieni protocols za kanisa katoliki halafu njooni tujadili
   
 14. M

  Mdanganywa JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 542
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Waliodhani hivyo hata utafiti mdogo hawawezi. Hata kwa kigezo cha umri Pengo anamzidi Kilaini kwa miaka minne tu. Sasa utasemaje atakuwa mrithi wake?
   
 15. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  NDO MAANA NAWASHAURI WATU WAWE MAKINI NA HIZI THREAD ZAO!sio cyt-n-paSTE!

  siku ingine wawe wanakuja na thread zao
   
 16. d

  dapo Senior Member

  #16
  Nov 24, 2012
  Joined: Oct 26, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hilo ndo kanisa katoliki bana the complex one
   
 17. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,750
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Ahsante mleta uzi
   
 18. kelao

  kelao JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2012
  Messages: 4,842
  Likes Received: 1,235
  Trophy Points: 280
  Wewe ndo yule wa clouds fm nini?
   
Loading...