Askofu Isangya atabiri Tanzania kuwa ya Asali na maziwa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
750
1,800
Kanisa la International Evangalism Church(IEC) hapa nchini limetamka kumuunga mkono Rais John Magufuli katika juhudi za kupigania rasilimali za taifa huku likiitabiria Tanzania kuwa ,hivi punde itakuwa kiuchumi na kuwa nchi ya asali na maziwa na wananchi wake watakula mkate wenye siagi.

Askofu mkuu wa kanisa hilo hapa nchini,Eliud Isangya wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa ambapo alisema ya kwamba kanisa hilo limekubaliana kumwombea na kuwataka watanzania kumuunga mkono jitihada zinazofanywa na rais huyo.


Akizungumza na waandishi wa habari Askofu Isangya alisema kwamba kitendo cha Rais Magufuli kuzuia makontena yaliyokuwa yakisafirisha mchanga wa madini ya dhahabu na kutaka yakaguliwe ni kitendo cha ujasiri na uzalendo, amethubutu na kinastahili kuungwa mkono na watanzania wote .

27bde4cbe45138facf0487aadecd9784.jpg


545657d6f4a80359f1b683e1909488ae.jpg
 
Back
Top Bottom