Salaam!
Inaendelea live,
Askofu Gwajima amesema kumekuwa na mlolongo wa matukio ya watu kutekwa pamoja na kupotea hivyo kutokana na hayo ameamua kuitisha mkutano huu na waandishi wa habari kuongelea kuhusu suala hili na kisha kutoa ushauri wake.
Gwajima anasema huwa haongei kwa kubahatisha, mpaka anakuja kuongea mbele za watu ni kwasababu ana data, na data hizo amekuzikusanya kutoka matukio yaliokuwa yanafanyika miaka kadahaa na kupata orodha ya watu takribani 83 waliopitia matukio haya ya utekaji, amewataja Mzee Soka, Mdude Nyangali, wanaharakati wa Kenya na Uganda na wengine wengi akijenga hoja kuwa kuendelea kunyamaza Katika Hali hii hauwezi kujua atayefuata kutekwa ni nani, hivyo Bora kusema na kushauri Ili mambo yatatuliwe.
Pia soma: Pre GE2025 - Askofu Gwajima: Wakuu wa Vyombo vya Usalama wasiondolewe kwenye nafasi zao kwa mapenzi ya mwanasiasa aliyewaweka
Ushauri
Tanzania ni yetu sote na ni tanzania kwanza, mengine yote yanafuata
- Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, wa bara na znz wanateuliwa na Rais na wanaondolewa na Rais pale anapoona hawafai, vile vile kwa mkuu wa jeshi la polisi na magereza. Mkuu huyu (yoyote kati ya hao) akipishana na rais kwenye jambo lenye maslahi ya nchi, halafu akashauri anaona jambo hilo linahatarisha usalama wa taifa anafukuzwa kazi! Kwasababu unaemshauri ana mamlaka tmya kukufukuza kazi, analetwa mwingine. Akionekana naye anakwamisha mambo fulani fulani kwa maslahi ya nchi anafukuzwa pia, akifukuzwa watu, akija wa nne atakubali kwasababu hawa ni binadamu, nao wanafamilia, na wana maisha na matamanio yao. Akiona mwenzake alitetea maslahi ya nchi akafukuzwa itabidi yeye kubali
Anafukuzwa sio kwasababu amefanya kosa, ni sababu anatetea maslahi ya nchi. Kwahiyo tukifanikiwa kuwalinda hawa wakuu wa vyombo wasifukuzwe hivi hivi kirahisi watakuwa na uwezo wa kusimamia nchi yetu vizuri bila kupata madhara ya yanayoathiri familia zao, utekaji utaondoka.
1. Tubadilishe sheria zetu kwamba wakuu wa vyombo vya ulinzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (DGIS) na wasaidizi wake, Mkuu wa Jeshi la polisi (IGP) na wasaidizi wake wote ambao ni wateule wa Rais, Mkuu wa Jeshi la Magereza, Jeshi wa Wananchi waendelee kuwa wateule wa Rais lakini wakitaka kutenguliwa, sababu za kutenguliwa kwao zipelekwe kwenye Kamati ya Bunge ya Usalama na Mambo ya Nchi za Nje ili ionekane kama hatolewi kutokana na uzalendo aliofanya. Asijekuwa anatolewa kwa sababu ameuza bandari (kwa mfano, sijasema bandari imeuzwa), kuuza mapori au kutetea wananchi tukajikuta tunapoteza wakuu wa vyombo wazuri wenye uwezo wa kutetea nchi na tunakuwa na wakuu wa vyombo ambao hawawezi kuitetea nchi.
2. Maslahi ya wanajeshi usalama wa taifa, polisi, magereza na jeshi la wananchi
Wanatakiwa kulipwa vizuri. Paka mwenye njaa ukimuachia maziwa lita 2 na kumwambia akulindie lakini ana njaa, utamkuta huyo paka amekunywa lita moja. Anasema Boss nilipata njaa, ili niendelee kuwa kwenye lindo nimekunywa lita moja na sio kwamba huyu paka hana maadili, ana njaa. Lazima tujifunze kuwalipa vizuri majeshi yetu. Sisemi kwamba hawalipwi vizuri, kama wanalipwa vizuri basi walipwe vizuri zaidi. Tutakuwa na vijana/wanajeshi/polisi imara, wanalipwa vizuri, maslahi na bima zao ziko vizuri, kila kitu kipo vizuri, tutakuwa na jeshi la wananchi imara wanaotoa uhai wao kwaajili ya kulinda nchi yetu.
Jambo hili litawezekanaje? Tuchukue mfano wa china, tunaweza kuanzisha makampuni ambayo yanatoka jeshi la wananchi, mfano makampuni ya ujenzi linatoka jeshi la wananchi, wanapewa tenda ya kujenga barabara kwahiyo hela inalipwa ndani ya nchi na kuzunguka kwa wanajeshi, wanapata maokoto, wataipenda nchi yao, na watafanya kazi. Jeshi la polisi litapata pesa ambazo tungemlipa mchina, hivyo hivyo kwa polisi wengine, kulikoni sasa hivi barabara zijengwe na mchina, umeme, nk.. tuamue tuwe na kitaasisi fulani ambako kazi zikitoka watapewa, tujaikuta pesa inazunguka ndani na vyombo vya nchi vinapesa, sio vyombo vyenye njaa. Mtu mwenye njaa hawezi kukulindia chochote.
Hapa umejaribu kuvitetea vyombo vya ulinzi lakini ni kama unaurusha mpira/lawama kwa wateuzi wa hivi vyombo vya ulinzi. Mtu anayeteua na kuondoa hivi vyombo vya ulinzi kwa katiba yetu ni Rais, na umezungumzia wanufaika wa haya mambo ni wanasiasa. If thats the case, hapa itatafasiriwa kwamba Askofu Gwajima anakuja kumnyooshea kidole Rais kwasababu ndio mwanasiasa na ndio mteuzi wa hawa watu, kwamba yeye ni mnufaika wa haya mamabo yanayoendelea. Wewe taasisi ya urais unaifahamu nchi hii inalindwa na nguvu ya kikatiba, je umejiandaa?