Askofu Gwajima: Kuna mtu ameleta barua Kanisani jioni hii, sikuiona amesema atarudi kesho

Askofu Gwajima: Kuna mtu ameleta barua Kanisani jioni hii, sikuiona amesema atarudi kesho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Mara baada ya kusambaa kwa Barua mitandaoni iliyodaiwa kuwa imetoka kwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa ikihusu kufungia shughuli za Kanisa la Glory of Christ Tanzania (Kanisa la Ufunuo na Uzima), Kiongozi wa Kanisa hilo, Askofu Josephat Gwajima amesema kuna Mtu amefika Kanisani hapo kwa lengo la kuleta barua jioni ya leo Juni 2, 2025

Amesema “Nikiwa kwenye ibada Wasaidizi wangu wamesema kuna Mtu alifika akasema ameagizwa kuleta barua, hawakuipokea, kitambulisho na taarifa zake tunazo, amesema atarudi kesho, tunamsubiri.”

Ameongeza “Hapa nipo na Maaskofu na Viongozi wengi wa Dini wote wanahoji kuhusu hiyo barua iliyosambaa Mtandaoni ambayo nilieleza kuwa siyo ya kweli kwa kuwa sikuwa nimepokea barua yoyote na ilizua taharuki kwamba Kanisa letu limefungiwa.”

Soma Pia: Serikali yalifutia usajili Kanisa la Askofu Gwajima kwa kuingilia masuala ya siasa kwa nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi

Awali, barua hiyo ambayo hakuna Mamlaka iliyojitokeza kuizungumzia ilieleza Kanisa hilo limefungiwa kwa maelezo ya kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa Kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi
 
Sasa kama hakuwa amepokea barua yoyote kwa nini akanushe kuwa hiyo iliyopo mtandaoni si ya kweli?

Huyu naye ana mapungufu makubwa kwenye public speaking.

Gazeti la The Citizen bado linaripoti kuwa kanisa lake limefungiwa, kwa mujibu wa hiyo barua.
 
Back
Top Bottom