Askofu Gwajima amtetea Lowassa

PINDA NI MUHANGA WA VITA YA URAIS.

*Kashfa ya sukari - MAJIBU.

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa ya uzushi ambayo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye baadhi ya magazeti yenye kichwa cha habari "KASHFA YA SUKARI *Pinda ndani, * Masaburi amvaa Kinana"

Katika habari hiyo, inatajwa kuwa kuna ufisadi mkubwa katika mchakato mzima wa utoaji wa vibali vya sukari na kwamba, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatuhumiwa kuwa ni mnufaikaji mkubwa na mhusika namba moja wa ufanikishaji wa ufisadi huo.

Pamoja na kuhusika kwa Mhe Pinda pia, habari hiyo inataja kuwa Janeth Masaburi, mfanyabiashara Turki, Zacharia, Mohamed Enterprise pamoja na Didas masaburi ni wahusika wa moja kwa moja katika ufisadi huo;

Kwa kuwa habari yenyewe ni ya kutungwa, uongo usiomithilika na ya kipuuzi- hatukuipa umuhimu wowote kwa mara ya kwanza, lakini kutokana na kusambaa kwake na athari zinazoendelea kujitokeza hasa kwa kuendelea kuchafuka kwa jina na hadhi kwa Mhe Waziri Mkuu lakini pia kwa maslahi na heshima ya viongozi wengine wa Chama na Serikali pamoja na wafanyabiashara waliotajwa katika habari hiyo tumeona umuhimu wa kuitolea ufafanuzi na kuwaeleza watanzania ukweli halisi na kupinga upotoshaji, uzushi na uongo uliyomo kwenye habari hiyo;

@ Ktk habari hiyo inatajwa kuwa tarehe 13th July 2014, Bwana Turki (mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka zanzibar) alikabidhi fedha taslimu kiasi cha Bilioni 4.13Tshs, kwa Bwana Didas Masaburi (mpiga kampeni wa Pinda), katika hotel ya PEACOCK.

--> Majibu ya hoja hii ni kama ifuatavyo:-
1. Ndugu Hassan Turki, si mjumbe na hakuwai kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kutoka Zanzibar.

2. Tarehe tajwa hapo juu yaani 13th July 2014, Waziri Mkuu Mhe Mizengo K. Pinda alikuwa bado hajatamka nia yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo hakuna ukweli wowote kuwa Mhe Pinda alikuwa akimtumia ndugu Didas Masaburi kama mpiga debe wake.

3. Kiasi cha fedha bilioni 4.13 ni kikubwa sana, makabidhiano ya kiasi hicho cha fedha kufanyika katika hotel tena katika mfumo wa fedha taslimu ni uongo mwingine wa dhahiri, ambao kila mmoja anaweza kuushuhudia.
katika habari hiyo imetajwa kuwa, mnamo tarehe 8/9/2014 ndugu Janeth Masaburi akiongozana na Kijana anayeitwa Mole (kijana wa Maswi wa ESCROW) walifika katika ofisi za Kwanza Limited, Kampuni Tanzu ya Mohamed Enterprise, eneo la Kamata na kukabidhiwa milioni 900.7 tshs.

--> Hii ni hoja nyingine dhaifu, kwani taarifa hiyo inataka kuliambatanisha suala hili na Escrow, jambo ambalo halihusiani kabisa lakini pia taarifa hiyo haisemi fedha hiyo ilitolewa kwa ajili ya kazi gani au makubaliano yapi.
habari hiyo ya uzushi pia inataja kuwa mnamo tarehe 22 Nov 2014, Ndugu Turki alitoa kiasi cha Bilioni 3 kwa ajili ya salamu za X-mass na mwaka mpya, ambapo kila mjumbe wa Halmashauri Kuu alipewa kiasi cha shilingi laki 8 (800,000tshs) na wajumbe wa mkutano mkuu kiasi cha shilingi laki 4 (400,000) na kwamba fedha hiyo alikabidhiwa Ndugu Didas Masaburi kupitia akaunti yake namba 01j2692311300 iliyopo Tawi la Azikiwe, CRDB.


--> Tuhuma hizi zinaonyesha udhaifu mkubwa unaotokana na kukosa hoja zenye msingi wa kihisabati, wajumbe wa NEC jumla yake ni 327 na wajumbe wa mkutano mkuu hawazidi 2300. Kwa kiasi cha uwiano wa laki 8 na 4 kwa kila mjumbe, haiwezi kutumika hata nusu ya Bilion 3.

Lakini udhaifu mwingine wa hoja hii ni ushahidi kuwa hakuna mjumbe hata mmoja wa Halmashauri kuu ama mkutano mkuu aliyepokea hata elfu 20,000 tu kutoka kwa Mhe. Pinda kwa ajili ya X-mass na Mwaka mpya.

Pamoja na hayo, ndugu Didas Masaburi hana na hakupata kuwa na akaunti katika tawi la azikiwe, CRDB yenye namba hizo tajwa.

Ama juu ya kauli za Ndugu Masabiri kuwa amemtuhumu Ndugu Kinana (Katibu Mkuu wa CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho Mhe Jakaya Kikwete kuwa wamemuandaa MAGUFULI kuwa mgombea wa CCM na Rais wa Awamu ya tano ni ngonjera isiyohitaji kiitikio, hakuna namna ya kulijibia hili isipokuwa ni kulipuuzia, ni upuuzi unaopaswa kupuuzwa.

Huu ni muendelezo wa siasa chafu, zinazofanywa ili kuharibu hadhi na sifa za wengine. Ni upuuzi na ufedhuli kutunga uongo ili kumchafua mwengine, na kama PINDA anatafutwa katika kesi ya RUSHWA kwa namna hii, basi HATOPATIKANA.

Pamoja na maelezo haya ambayo yanatoa ufafanuzi katika tuhuma hizo za kutunga, bado wahanga wa uongo huo wanayo haki ya kisheria ya kufungua kesi na kuwashitaki wale waliohusika ktk kutunga na kusambaza uzushi na uongo huo wenye kulenga kuwafedhesha na kuwavunjia heshima waliyonayo mbele ya jamii.
 
Last edited by a moderator:

lowassa kaishiwa hadi anaomba msaada kw kanjanja gwajima. Ikulu atapasikia tu. Kwake ni segerea au ukonga au keko. Ngoja tumalize kazi Oktoba
 
Humu JF kuna watu wana ubongo wa matope.

Hapa Gwajima amejitosaje kwenye uraisi??????????
Anagombea???
Watu wanaandika upuuzi. Hekima na kweli vimekuwa ni adimu sana kwetu!
What he has said should be the clearest and the best utterance ever to be said by the post independence leader in Tanzania.
 
Hivi gwajima ndiyo anayetembea na wake za watu kama ndiye kesha laaniwa hata anayozungumza siyo yeye ni shetani aliyemwingia.
mtu atoke kwake asubuhi anarudi keshajitangaza kuwa ni askofu,watu hawa ni hatari ni mataperi kama wanaouza makanisa,hivyo anaweza kuwa kaajiriwa na fisadi kwani lengo lake ni pesa na fisadi anazo,wenye ufahamu eleweni.
 


Yeees, kama kuna mgombea asiyetumia pesa na arushe mawe!
WATU WAACHE UNAFIKI!
 
Kama uaskofu ndio huu wa kujipachika kisha kuuza sembe basi kuanzia leo na mimi ni kardinali
 
Gwajima ni lazima amtete sana Lowassa kwa sababu amemsaidia pesa za kununulia helkopita Kwa msiofahamu lowassa hivi sasa ni bilionea ameuza hisa zake vodacom na kupata zaidi ya Sh bilioni 280 ambazo sasa anazigawa
 
jamani twende turudi kwenye uchaguzi hata wa mwenyekiti pesa muhimu. huku kwetu m/kiti ni chadema ila kabla ya uchaguzi amewapa vijana viroba vingi
 
Watanzania tuna tatizo la kusoma na kuyaelewa maandishi,wacha wanasiasa wàendelee kutupeleka peleka.
 
Mnapayukaaaa tu bilaaa hela mnaweza kufanya harakati ,mkono mtupu haulambwi.....
 

Dk.Magufuli hana kundi na hilo linajulikana yeye kama yeye anajitosheleza kuomba uongozi wa nchi hahitaji support za kimakundi, tungoje wakati ufike.
 
Last edited by a moderator:
hakuna msafi...

Mlitegemea kusikia nini kutoka kwa mtu kama Gwajima.
Naye ni tapeli na fisadi namba moja.
Tangu lini mtu akasema ana uwezo wa kufufua watu . Ni Gwajima huyu kajipa upako wa kishetani huyu mhuni kama wahuni wengine , anatembea na wake za watu , muuza unga alafu anajifanya mtu wa Mungu.
Biblia inasema wacha wafu wazike wafu wenzao. Huu ndo mtiririko wenyewe lazima kutetewa na Gwajima uwe kwenye fungu moja linalobeba watu wachafu
, baradhuri na mafisadi
 
Gwajima Unalaana Na Mimi Ni Papa Nimetoka Vatcan Kum a Ma Yo

Wewe una laana kweli kabisa. Usimtukane kiongozi wa dini, hata kama hakuongozi kanisani wala msikitini. Kiongozi wa dini si watu wa kuwaongelea maneno ya kijinga, mdhaha na upumbavu kama unavyojisikia.
 

Kama jina lako lilivyo linasadifu uchovu wa akili zako, una uhakika na uyasemayo?? Hapa sio Facebook kuandika upuuuzi pasipo kuwa na ushahidi stahiki wa jambo husika.. Akili hizi ulizonazo sidhani kama zinastahili kuwemo humu ndani, makanjanja wengi na vibaraka hata kusoma habari hamsomi mnaishia kuongea mambo msiyoyafahamu... acha kudakia mada ambayo hata gazeti hujasoma, yani wewe kichwa cha habari tu cha gazeti unaanza kucoment!! Aisee uwe unatumia akili za kiutu uzima basi, mana ukichoandika ni sawa na analysis ya mtoto wa darasa la tatu
 
Namkubali pastor Gwajima kuwa si miongoni wa viongozi wa dini Uchwara na Wanafiki katika nchi yetu mnaowajua kama ....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…