Askofu Fredrick Shoo: Wale wote wanaojaribu kupotosha ukweli wa waraka wa Maaskofu kwa kuupaka matope ni wajinga

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo, amesema wale wote wanaojaribu kupotosha ukweli wa waraka wa maskofu kwa kuupaka matope ni wajinga.

Askofu Shoo ametoa kauli hiyo leo katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini, mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Pasaka katika ibada maalumu ya kusherekea sikukuu hiyo.

Amesema kumekuwa na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa ambao wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kupotosha waraka wa maaskofu hao na kulipaka kanisa matope kwa malengo yao binafsi jambo ambalo halipendezi na kwamba watu hao ni wajinga.

“Wapo wanaotumia nguvu nyingi kutaka kupotosha ujumbe wa waraka wa maaskofu na wamekuwa wakilipaka kanisa matope ili waweze kurejea katika waraka ule, watu hawa naweza kuwaita ni wajinga lakini pamoja na hilo nataka wakayatafakari na kama wanaona kuna hatua za kuchukua wachukue.

“Kanisa limekuwa linapata kejeli za aina mbalimbali kutoka kwa watu hao na kuwatuhumu kuwa maskofu walifikia maamuzi ya kuandika waraka huo kutokana na sababu za kimaslahi kwa maana ya sadaka makanisani kupungua jambo ambalo si la kweli.

“Kanisa linasitikika sana, tunaposema jambo la kweli na jambo linalohusu maisha ya Watanzania wote, halafu kunatokea watu chache ambao naweza kuwaita wajinga wanakebehi na kusema eti kwa sababu sadaka zimepungua kanisani sisi sadaka hazijapungua kwani wakristo wanajitoa sana na hatujapungukiwa na kitu ila tunasema yale tunayoyaamini,” amesema.

Askofu Shoo amesema anafahamu kuwa kupitia waraka ule maaskofu wa kanisa hilo watabatizwa majina ya aina mbalimbali na kwamba hizo ni jitihada za kujaribu kuuzima ukweli ulipo katika wataka huo na wao hawajali kuhusu hilo bali watasimamia ukweli zaidi.

“Najua tutaitwa majina mengi maaskofu na hizo ni jitihada za upotoshaji wa ule ukweli ulipo katika waraka na tukumbuke hili si jambo la hivi hivi tu…. kwani kwa wakati mmoja mabaraza ya maaskofu wa makinsa makubwa mawili nchini kukaa na kutoa waraka ambao una ujumbe ulioshabihiana si kitu cha kawaida mimi nasema kuna kitu Mungu anataka kutuambia kupitia ujumbe ule tutafakari hili kama taifa,” amesema.

IMG_20180401_125535.jpg
 
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo, amesema wale wote wanaojaribu kupotosha ukweli wa waraka wa maskofu kwa kuupaka matope ni wajinga.
Askofu Shoo ametoa maneno katita ibada ya Pasaka imefanyika leo
View attachment 731279
Umenene baba askofu hakika kila goti litapigwa na kila kinywa kitakili kwamba wewe ni bwana
 
Kama taifa tujitafakari,hizi lugha hazina afya kwa taifa kwa kila mmoja kutumia jukwaa lake kumshambulia mwenzake
 
Kipimo cha wajinga na welevu ni kipi?
Wakati mwingine ujinga unaweza kuwa ni msaada na
Welevu kuwa tatizo.
Kwanini tunazidi kuendelea na mijadala yenye kuwagawa na kuwakejeli wenzetu kisaiklojia?
Hii nchi pengine imefika hapa kutokana na ujuaji wa welevu wachache kuwakandamiza wajinga wengi.
Lakini pia welevu wamekuwa ni wasaliti na wa binafsi kwa wenzao kwa kutumia miamvuli mingi kujificha.
Bora kutawaliwa na wajinga wenye kujali maslahi ya wajinga wenzao kuliko kutawaliwa na welevu wenye kujali maslahi yao na ya wachache.
 
Back
Top Bottom