Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama mwanadamu anayo mapungufu na hivyo ni haki kwa mtu ye yote kutofautiana na misimamo au mitazamo yake. Lakini si haki hata kidogo kumtusi, kumtweza, na hata kumdhalilisha kwa namna ye yote ile.
Ukifanya hivyo utakuwa unajikosea wewe mwenyewe katika nafsi yako na pia utakuwa unatukosea na sisi wengine wote haijalishi kama tunakubaliana au tunatofautiana na mitazamo au misimamo yake.
Tujifunze kutumia hoja katika kutofautiana na watu pasipo kutumia lugha za matusi kwa viongozi na hata watu wa kawaida na huo ndio utu.
Tujifunze na tujenge utamaduni wa kuheshimu utu wa watu hata wale tunaotofautiana nao kwa kuwa kwa kufanya hivyo tutakuwa tunamheshimu Mungu kwa vitendo.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.