Askofu Bagonza: Utitiri wa watia nia na wenye kamba miguuni

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Tumemaliza hatua ya kutia nia. Sasa ni kuchukua fomu. Utafuata uteuzi. Mawili yamejitokeza katika utiaji nia na uchukuaji fomu.

Kwanza kuna utitiri wa watia nia katika chama tawala na ukame wa watia nia katika vyama vingine. Kwa nini? Nitaeleza hivi punde.

Pili, kuna sura mpya zisizotegemewa katika medani hii. Ni kama kuku wageni wenye kamba miguuni. Wengine wanachomekea mashati yasiyochomekewa. Wengine wamevaa kijani juu ya nembo za taifa. Historia imewekwa kwa kuwaona tuliodhani hawana vyama, kumbe sasa wana vyama: maaskofu, wana usalama, watumishi wa vyombo vya utoaji haki mpaka watumishi wa tume ya uchaguzi. Tusijidanganye tena kuwa viapo vinafuta itikadi, dini, kabila na urafiki! Madhara yake watajua wajukuu.

Kwa nini utitiri? Sababu zaweza kuwa nyingi. Nimesikia mbili zikitajwa na wengi:

1. Chama kinafunika mengi. Mgombea unakuwa salama ktk biashara, kodi, uraia, ajira, uteuzi, kura hewa, ulinzi, na hata mahakamani. Unakuwa salama kabla, wakati na baada ya kugombea. Haya yote tumeyashika tangu utoto ila safari hii hata waliovaa shati la kijani juu ya gwanda wametia nia!! Tutaisoma namba na herufi.

2. Kugombea kupitia chama hiki si lazima ufanye lolote ukiishachaguliwa. Serikali itafanya. Useme usiseme, serikali ipo. Wewe tulia na ule nchi kwa miaka mitano. Kusemasema si vizuri wakati wa kula. Hiyo ni kazi ya wasio na chakula.

Kwa nini kuna ukame wa wagombea katika vyama vingine? Nimesikia mbili zikisemwa na wengi kati ya nyingi:

1. Hawatapitishwa na tume kugombea. Fomu zao zitachafuliwa. Wanaowaunga mkono wagombea hao hawatapiga kura. Wakijitokeza kupiga kura watazuiwa. Wakilalamika watakamatwa. Wakipiga kura hazitahesabiwa. Zikihesabiwa hazitatangazwa. Ni utitiri wa visa!

2. Ni maisha ya roho mkononi kila wakati. Uraia, kubambikiwa kesi, kufilisiwa, kutekwa, kujeruhiwa, kuuawa, na kuteswa kisaikolojia. Atakayewafanyia haho hajulikani. Utitiri wa visa na hofu mbalimbali. Fomu ya kugombea mkononi na wosia mkono wa pili!

Haishangazi wagombea wengi wa upinzani ni kina mama (mashujaa wa nchi waliosahauliwa na historia). Kina mama ni jasiri. Kila nyuma ya mwanamme aliyefanikiwa kuna mama lakini si kila nyuma ya mama aliyefanikiwa kuna mwanamme au baba ! Hilo ni somo jingine kwa siku nyingine. Muda si mrefu, wanaume tutagombea viti maalum!

Jamani eh!! Maisha ni siasa na siasa ni maisha. Usiposhiriki utashirikishwa bila kutaka. Hata maiti inashiriki siasa ndo maana kuna Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi.

Nina tatizo moja tu. Mnaogombea litatueni mpate kura yangu.

Madhara ya siasa mbaya hayabagui, lakini sisi tunabaguana na kutesana.
Daima mkumbuke kuna maisha baada ya siasa. Kuna watu tulikuwa haturuhusiwi kula mpaka wafike kwanza, hivi sasa tunawaambia waondoke ili tule.
 
Chadema hawampi jimbo huyu Askofu kada wao, haa, maana anawapa hoja wanazoona zina mashiko sana huko Chadema mpeni tu jimbo..
 
Write your reply....Mungu akutunze Askofu Bagonza umebaki peke yako Tanzania msema ukweli Gwaji kesha jishusha mwenyewe anazidiwa akili na Mzee Wa Upako?
 
Back
Top Bottom