PostGE2025 Askofu Bagonza: Polisi kuvaa kininja mahakamani na kuteka/kukamata bila sare aseme IGP au Waziri?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu,

Askofu Bagonza Disemba 8 aliuliza, "Kuvaa kininja mahakamani na kuteka/kukamata bila sare; aseme IGP au Waziri? Askari wamfuate yupi? Nani awaamue?"

Aliuliza swali hilo, kukiwa na mfululizo wa matukio yanayotokea polisi wakiwa wanaendelea kukamata watu bila ya kufuata utaratibu baada ya Waziri Simbachawene kutoa maagizo ya taratibu kufuata pindi mtu anakuwa anakamatwa.

Majuzi kuna askari alisema kwenye mahojiano kwamba watuhumiwa ni wajanja, wakisikia wanaenda kukamatwa wanakimbia, kwahiyo nao inabidi wavae kiraia ili waende nao sambamba! Hili linatosha kuhalalisha taratibu kuvunjwa?

Tukirudi kwenye swali la msingi la Askofu Bagonza, nani anatakiwa kutoa maagizo hayo, kama hata baada ya Waziri Simbachawene kutoa maagizo, baado ukamataji ule ambao haufuati taratibu na sheria unaendelea?

Screenshot_20251227_110051_Facebook.jpg
 
Tukirudi kwenye swali la msingi la Askofu Bagonza, nani anatakiwa kutoa maagizo hayo, kama hata baada ya Waziri Simbachawene kutoa maagizo, baado ukamataji ule ambao haufuati taratibu na sheria unaendelea?📌🔨
 
Admistratively waziri wa mambo ya ndani ni bosi wa hao askari,
Technically, IGP ndiye boss wao!
 
Mafwele ndo boss wao na ni boss wa waziri pia

Maana mafwele anaweza akatoa maagizo askari wakafuata maagizo ila waziri akitoa agizo askari awalifuati sasa hapo nani boss wao?
 
Makamanda Kimenuka huku maandamano makubwa sana huku
 
Wakuu,

Askofu Bagonza Disemba 8 aliuliza, "Kuvaa kininja mahakamani na kuteka/kukamata bila sare; aseme IGP au Waziri? Askari wamfuate yupi? Nani awaamue?"

Aliuliza swali hilo, kukiwa na mfululizo wa matukio yanayotokea polisi wakiwa wanaendelea kukamata watu bila ya kufuata utaratibu baada ya Waziri Simbachawene kutoa maagizo ya taratibu kufuata pindi mtu anakuwa anakamatwa.

Majuzi kuna askari alisema kwenye mahojiano kwamba watuhumiwa ni wajanja, wakisikia wanaenda kukamatwa wanakimbia, kwahiyo nao inabidi wavae kiraia ili waende nao sambamba! Hili linatosha kuhalalisha taratibu kuvunjwa?

Tukirudi kwenye swali la msingi la Askofu Bagonza, nani anatakiwa kutoa maagizo hayo, kama hata baada ya Waziri Simbachawene kutoa maagizo, baado ukamataji ule ambao haufuati taratibu na sheria unaendelea?

Sheria ndo inasema na si waziri au IGP, Kama sheria inamtaka lazima avae sare, asiyevaa wakati wa ukamataji basi achukuliwe hatua.
 
Makamanda Kimenuka huku maandamano makubwa sana huku
Hebu kua basi eeh hata Kama hakuna chuo Cha kukuzia watu busara ikuongoze!
Viongozi wenu wanahangaika kutwa kutatua tatizo na kutafuta suluhu, wewe na utoto wako unachochea ili upate nini!
Uvccm na wewe Kihongosi hebu vunja hicho kikundi chako Cha mitandaoni kwani hakisaidii kupatikana kwa muafaka Bali kinaamsha hasira zilizopoa ambazo kimsingi hazijalala!
Zikiamka hasira hizi mnazozibagaza na kuzisodoa hali haitakuwa hivi ilivyo.
Endeleeni na upuuzi wenu ila msiwalaumu wakilianzisha na msifikiri mmewashinda.
 
Bagonza mwamba sana huyu Askofu! Kama hauko makini, unaweza kufikiri na yeye ni TEC; adui namba moja wa wahuni/waminyaji wa haki za raia.
 
Simbachawene anatu-enjoy tu, anayewatuma ni Samuya ambaye yuko zake Mkunazini anakunwa na mkunaji wake
 
A
Mafwele ndo boss wao na ni boss wa waziri pia

Maana mafwele anaweza akatoa maagizo askari wakafuata maagizo ila waziri akitoa agizo askari awalifuati sasa hapo nani boss wao?
Na hii ndio tafsiri sahihi ya Gangster government.

Serikali ya kihuni inayoendeshwa kihuni na wahuni waliovaa vazi la uongozi wa kiraia.
 
Back
Top Bottom