Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook anasema:
RAIS APOKEE NYONGEZA YA KERO
Mh. Rais Samia amewatubia Majaji na Mahakimu. Ametumia fursa hiyo kueleza kero zake juu ya mwenendo wa mahakama na utendaji wa Majaji na Mahakimu.
Ametaja: Ubambikiaji wa kesi; Kuhukumiwa vifungo kwa uonevu na akatamka rasmi kuwa BILA HAKI hakuna maendeleo. NAMPONGEZA SANA. Napenda niongozee orodha yake ili ajipime kama anakerwa kama mimi:
1. Utekaji wa watu na kuwaficha kusikojulikana. Mahakama inatoa amri waletwe lakini Polisi wanapuuza amri hizo. Inapunguza uhuru wa mahakama.
Kwa kuwa rais anakerwa na kukosekana kwa haki, hata kama hajui kuwa kuna watu wanashikiliwa, ajifanye amejua ili waachiwe. Inachafua serikali yake pakubwa.
2. Polisi wanashikilia mahabusu kwa muda mrefu. Mawakili wanapeleka “Habeas Copus” kuwashtaki polisi. Siku ya kesi hiyo kusikilizwa, Polisi wanaachia mahabusu au kuwaleta mahakamani. Ni mchezo wa kitoto unaochezwa na watu wazima. Mahakama iheshimiwe na polisi.
3. Ubambikiaji wa Kesi: Bora anayebambikiwa kesi akahukumiwa kutumikia kifungo kuliko anayeshikiliwa mahabusu bila kuhukumiwa, na baada ya muda mrefu DPP akasema hana haja na kesi hiyo tena. Huyu anatumikia adhabu bila kuhukumiwa.
4. Polisi kupiga watuhumiwa kana kwamba wameishahukumiwa. Zimetolewa tuhuma mbaya za kufira, kulawiti, mateso makali (torture) nk. Watuhumiwa wanaposhinda kesi au kuachiwa huru mbona Polisi waliowapiga hawarudishiwi fimbo zao?
Tuhuma hizi ni nzito na zinakera.
5. Maafisa wa serikali “wanaojituma” kuwatisha majaji na mahakimu kuhusu kesi fulani au kuwaahidi maslahi wakiamua kesi fulani. Licha ya mahakama kuingiliwa, inaichafua serikali na wanaoiongoza.
6. Jaji Mkuu kuomba omba maslahi ya watumishi mbele ya rais huku akisisitiza uhuru wa mahakama! Bila mahakama kujitegemea kimaslahi, haitakaa iwe huru. Jaji Mkuu, Rais na Spika wote waombe fedha bungeni.
7. Huduma ya utoaji haki iwe wazi muda wote sawa na hospitali. Hata usiku mahakama iwe kazini kwa waliopumzika mchana. Uhairishaji na ucheleweshaji wa kesi ni kitalu cha kustawisha dhuluma. Haki itendeke na ionekane inatendeka.
8. Kuondoa Ma DC na Ma RC katika kamati za Nidhamu za mahakama ni wazo bora. Tuondoe Makamanda wa Takukuru wa Wilaya, Mikoa na Taifa katika Kamati za Ulinzi na Usalama. Viongozi wetu wa ngazi hizo hawana chanjo ya kuwazuia kupokea au kutoa rushwa. Makamanda watashughulikaje nao ikiwa ni wenyeviti wao?
9. Taifa letu ni linaongozwa Kijeshi hivi sasa kuliko huko nyuma (Military Government). Maaskari wenye sare na wasio na sare wamejaa kwenye mihimili yote. Hata huku mahekaluni tumeingiliwa. Sisi ni Jamhuri, tuongozwe kiraia. Tunza hii namba 9, siku moja mtaikumbuka.
10. HAKI anayoipazia sauti Rais, imeshikamana na neno UHURU. Hata uhuru wa mahakama unakosekana kwa sababu watu hawako huru. Uhuru ukikosekana, mhanga mkuu ni Rais kwa sababu atadanganywa sana na washauri na wasaidizi wake. Penye uhuru, Mshauri anaweza kumwambia Rais hata asichokipenda. Rejesha uhuru wa watu.
Siku hizi hata Wajaluo wanaogopa kusema kuwa wanatamani kuoa mke wa pili🤣🤣