Askofu anayeondoka Same itakuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu anayeondoka Same itakuwaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paschal Matubi, Jun 15, 2009.

 1. P

  Paschal Matubi Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Wachimbi wanaendelea kumjadili yule askofu aliyeondolewa kule Same ambako inaelekea ni eneo maarufu kwa mitafaruku ya kidini.
  ---
  Makala ya Tanzania Daima
  Website hii: Jacob Koda sasa ni askofu jimbo gani?
  ---

  ASKOFU Jacques Gaillot wa Ufaransa alijulikana kama Askofu wa Jimbo la Evreux tangu mwaka 1982. Ulaya ilishuhudia ugomvi wake na Vatican wa muda mrefu na ambao haukuwa ukijificha machoni mwa watu.

  Januari 12, 1995 aliwaambia waandishi kwamba kaambiwa na Vatican kuwa jimbo la Evreux si lake tena. Liko wazi likisubiri askofu mwingine. Haikushangaza, kuondolewa kwake Evreux. Kilichoshangaza ni kukamilisha hiyo taarifa yake kwa sahihi iliyoonyesha yeye sasa ni askofu wa jimbo la Parthenia.

  Baadhi wakashangaa Papa John Paul II kumpa askofu huyu jimbo jingine. Je, Papa haoni yaliyotokea Evreux yatajirudia Parthenia?

  Wakaanza kulidadisi kulijua hili jimbo Parthenia atakalohamia Askofu Gaillot. Wakagundua liko katikati ya jangwa la Sahara. Liliteketea karne ya tano kwa kufunikwa na mchanga mkubwa wa jangwani (sand dunes). Kumbe ni nadharia tu, kiuhalisi jimbo hilo halipo. Hivyo, Gaillot ni Askofu wa hiyo Parthenia, lakini kivitendo hana eneo la kutawala wala wanajimbo.

  Sebuleni nina picha kubwa iliyotengenezwa na Baraza la Maaskofu (TEC). Ina ramani ya Tanzania yenye picha ndogo za kila askofu katika jimbo lake. Pia ina picha za mapapa sita, maaskofu wa zamani (Emeritus) na Balozi wa Papa nchini (Askofu Mkuu Joseph Chennoth).

  Marafiki walionitembelea iliwavutia. Mmoja aliyeiona (si mkatoliki) aliniuliza “mbona Dar es Salaam ina maaskofu wawili”? Nikamjibu uwezekano wa maaskofu wengi jimboni. Alipomtazama Balozi wa Papa akaniuliza tena “mbona askofu huyu hana jimbo?”.

  Nikamfafanulia dhana ya majimbo yanayoitwa Titular Diocese na kwamba maaskofu wa majimbo haya wanajulikana kama Titular Bishop akiwemo Balozi wa Papa. Nilijilaumu kutomfafanulia mapema alipouliza Dar es Salaam yenye maaskofu wawili.

  Wakatoliki wenzangu wakaibua mjadala mkali tulioutuliza kwa kurejea vifungu kwenye kitabu chenye Sheria za Kanisa yaani “New Commentary On The Code of Canon Laws” kilichotolewa na “The Canon Law Society of America” na kuchapishwa India mwaka 2003. Sijaelewa kwa nini mjadala wa Titular Bishops huzaa ubishi kidogo lakini kila mmoja ana haki ya kuielewa dhana hiyo si jambo la siri.

  Tumeona hata Ulaya walivyoshtushwa Gaillot kupewa jimbo jingine yaani Parthenia. Walioshangaa ni wale ambao hawakujua kwamba hii Parthenia ni Titular Diocese.

  Je, Titular Diocese au Titular See ni nini? Sijajua niyaiteje kwa kiswahili. Lakini ni majimbo yaliyokuwepo kale kama yalivyo majimbo yetu ya sasa. Ushamiri wake umepotea kwa sababu kadhaa kama vita au kubadili jina. Yako sehemu mbalimbali duniani. Sikuwahi kuyasikia hapa Tanzania. Lakini mitandao imeshatutangazia kuwa Januari mwaka huu tumepata mawili yaani Nachingwea na Rutabo (Rejea: Changes in Ecclesiastical Circumscriptions (2009)). Nachingwea ndiyo iliyobadilika kuwa Lindi kama Rutabo ilivyobadilika kuwa Bukoba. Hivyo, ni kama yamefufuka lakini sasa ni Titular Diocese au Titular See. Yote mawili yako wazi hayajapata Askofu.

  Askofu wenye majimbo tunayoishi kama Mwanza (Mayala), Same (alivyokuwa Koda) huitwa Diocesan Bishop (Askofu wa Jimbo). Wasio na majimbo hujulikana kama Titular Bishop na hivyo hupewa moja ya hizi Titular Diocese au Titular See.

  Hivyo kiuhalisia kila askofu duniani ana jimbo la uaskofu wake. Haipaswi jimbo liwe na maaskofu wawili au awepo askofu asiye na jimbo. Nashauri msomaji upitie kifungu 376 cha sheria za Kanisa kinachobainisha mgawanyo huu (Can. 376). Kuondoka kwa Jacob Koda, kunaifanya Tanzania ya majimbo 31 ibaki na maaskofu 30 wa majimbo.

  Sasa tujadili aina hii ya maaskofu wasio wa majimbo yaani Titular Bishops kuanzia aya ifuatayo. Zamani wote wasiomiliki jimbo waliitwaTitular Bishop wakiwemo waandamizi (Coadjutor) na Bishop Emeritus (wastaafu). Kustaafu, kulimfanya aliyekuwa wa jimbo kuwa Titular Bishop na kupewa Titular Diocese.

  Papa Paul VI alirekebisha kwamba wastaafu au wanaojiuzulu jimboni hawatapewa tena Titular Diocese. Kwamba watambulike kwa majimbo waliyokuwemo (Bishop Emeritus). Wa aina hii ni Lukanima (Arusha), Msarikie (Moshi), Isuja (Dodoma), Nkalanga (Bukoba), Mwanyika (Njombe), Shija (Kahama) na Mwalunyungu (Tunduru-Masasi).

  Pia askofu mwandamizi (Coadjutor Bishop) waliacha kuwa Titular Bishop. Walianza kuitwa kwa majimbo waliyomo. Hawa wana haki ya kurithi jimbo{Sheria: Can. 409(1) na Can. 416}. Mfano ni Polycarp Pengo (Mwandamizi) alivyoirithi Dar es Salaam siku alipostaafu Kadinali Rugambwa.

  Tumejadili wajulikanao kwa majimbo yetu. Sasa tunawajadili (Titular Bishop) wanaofanya kazi kwenye majimbo yetu lakini majimbo ya uaskofu wao (Titular See) yaweza kuwa nchi nyingine tofauti.

  Askofu msaidizi ni aina moja ya Titular Bisshop. Methodius Kilaini wa Dar es Salaam jimbo lake ni Strumnitza yaani Titular Bishop of Strumnitza (Askofu wa Strumnitza). Nadhani ni ile Strumnitza iliyotekwa vitani mara na Bulgaria, Uturuki na Macedonia. Askofu wasaidizi hawa, hawana haki ya kurithi jimbo kama wenzao Coadjutor (waandamizi) { Sheria: Can. 403(1)}.

  Titular Bishop wengine ni Mabalozi wa Papa (Apostolic Nuncios). Majimbo yao mara nyingi huwa majimbo makuu (Titular Archdiocese). Joseph Chennoth aliyepo nchini, jimbo lake huitwa Titular Archdiocese of Milevum. Hivyo anaitwa Askofu Mkuu wa Milevum (Titular Archbishop of Milevum).

  Kuna wanaokuwa Vicars Apostolic. Wanaongoza Apostolic Vicariate (Vikarieti) ambayo haijawa diocese au jimbo (Can. 371(1)). Laurian Rugambwa alianza uaskofu kwa mtindo huu kama Vicar Apostolic wa Kagera-Inferiore (Kagera-Chini). Alikuwa Titular Bishop of Febiana (Askofu wa Febiana). Kagera-Chini lipandishwa hadhi kuwa jimbo la Rutabo. Ndipo Laurian Rugambwa akawa askofu wa jimbo (Deocesan Bishop). Akaachana na ile hadhi ya Askofu wa Febiana iliyomshika kwa siku 468. Febiana aliyoachana nayo ikampata Antonio de Campos, Askofu Msaidizi wa Lisboa (Ureno).

  Titular Bishops wengine wako Vatican kwenye idara za kanisa (Roman Curia). Askofu Mkuu Fortunato Baldelli ni mkuu wa moja ya mahakama kuu za kanisa (Apostolic Penitentiary). Jimbo la uaskofu wake ni Mevania yaani Titular Archbishop of Mevania(Askofu Mkuu wa Mevania).

  Hapo hapo Vatican, mahakama nyingine (Roman Rota) inaongozwa na Askofu Antoni Stankiewicz yaani Titular Bishop of Nova Petra (Askofu wa Nova).

  Titular Bishop wengine ni wale wanaoongoza vikundi (Personal Prelatures) vya kanisa vyenye wafuasi waliosambaa duniani. Askofu Javier Echevarría Rodríguez anaongoza kikundi kiitwacho Opus Dei. Yeye ni Titular Bishop of Cilibia (Askofu wa Cilibi).

  Kanisa liliwahi kutoa uaskofu kwa watawa wa kiume (Territorial abbots) kwenye maeneo waliyokuwa kikundi pekee cha mapadri (Can. 370). Mwaka 1933 Ndanda ilimpata Askofu Joachim Ammann, mkuu wa abasia hiyo akijulikana kama Titular Bishop of Petnelissus (Askofu wa Petnelissus).

  Husemwa kwamba hata makadinali sita (Cardinal Bishops) walioko Vatican , huwekwa katika kundi hili. Kwani kila mmoja ana kanisa jijini Roma (suburbicarian see) kama ishara ya jimbo. Mkuu wa jopo la makadinali duniani (Dean of Cardinals) anaongezewa moja (Ostia) hivyo kuyafanya yawe makanisa saba.

  Tumeona Titular Bishops wengi wamekabidhiwa majukumu. Tulipomjadili Askofu Jacques Gaillot tumeona kuwa kumbe askofu anaweza kuondolewa jimboni, akapewa Titular Diocese. Kwa njia hiyo anabaki kuwa askofu asiye na jukumu lolote.

  Lakini kwa Gaillot ilileta kitu kisichotarajiwa. Badala ya kunyamaza alihamishia maoni yake kwenye mtandao hadi tovuti yake ikaitwa cyber-diocese au jimbo jipya mtandaoni.

  Mjadala kuhusu Jacob Koda huenda haujaisha. Balozi wa Papa keshaeleza kilichomuondoa basi inatosha. Hata hivyo mitandaoni waweza kushuhudia maoni mengi. Pengine kilichomuondoa Koda ni kingine kabisa kana kwamba taarifa ya Balozi Chennoth ilikuwa ni kichwa cha habari na habari kamili wanayo wao.

  Kuwazuia hawa si rahisi maana hatutazuia simu zao kusambaza mawazo yao kona zote wanazotaka. Kama hatutawapuuza basi nadhani hawa tuwakaribishe kwenye mjadala kama makala hii. Ukizingatia makala yangu utagundua cha msingi sasa ni kujua hatima ya Askofu Jacob Koda kulingana na sheria za Kanisa zinazoongoza wakatoliki walio kwenye ushirika na Papa (Communion with the Holy See).

  Sikujua kama wengi mnajua niliyoyajadili, hasa ile dhana ya Titular Bishop. Ningejua mnajua, makala ningeifupisha kwa maswali matatu tu yafuatayo: 1: Je Askofu Jacob Koda sasa amekuwa Titular Bishop na kupewa Titular Diocese kama Askofu Jacques Gaillot? 2: Je, sasa amekuwa Bishop Emeritus (mstaafu) wa jimbo la Same kama ilivyokuwa Askofu Pius Ncube wa Bulawayo mwaka juzi? 3: Je ameondolewa kabisa utumishini (laicization) ajichagulie shughuli binafsi kama Askofu Fernando Lugo ambaye sasa ni Rais wa Paraguay?

  Nimekomea kwenye haya matatu maana sijaona dalili kwamba labda ametengwa (excommunicated) hata akakosa Titular Diocese kama alivyotengwa Askofu Marcel Lefebvre na wenzake wa SSPX mwaka 1988.
   
 2. share

  share JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Ni tundiko zuri sana. Inaonekana mkuu Paschal Matubi unao ufahamu mzuri wa masuala haya. Kati ya maswali yako matatu, mimi nalipa uzito la kwanza, ya kuwa atapewa Titular Diocese kwa misingi kuwa ni kijana (hajatimiza miaka 75) na hivyo hawezi kuwa Bishop Emeritus (swali lako la pili) na vilevile haijatangazwa rasmi iwapo ameondolewa utumishi (swali la tatu). Hivyo nadhani huyu atatupwa sehemu fulani Italia asahaulike huko na wakati huohuo kupewa Titular Diocese fulani lisilokuwa hai katika ulimwengu wa leo.
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  hapo ndo huwa nawapa tano kanisa katoliki, hakuna malumbano wakishakutimua baada ya kuboronga huyna hata wa kumuuliza, ingekuwa madhehebu mengine ungesikia kuna kundi limemeguka naye
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  nakubaliana na kanisa 100% UKIBABAISHA UNANGOLEWA KISAYANSI
   
 5. P

  Paschal Matubi Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Mkuu, Niliisoma jana kwenye TANZANIA DAIMA na imo kwenye website ya gazeti hilo.
   
 6. G

  Gashle Senior Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yeah,
  Uzuri wa makanisa haya ya kimsingi (traditional churches) ndio kama huu, hakuna malumbano, utaratibu unaeleweka. Umeonewa, hujaonewa lazima continuity iwepo. Heko Catholics, hata Walutheri pia. Lakini ndugu zangu makanisa ya 'kiroho' kazi bado mnayo. Kule administration ni shaghala baghala. Tujifunze yaliyo mema.
   
Loading...