Askofu aipinga tume ya Pinda

Askofu aipinga tume ya Pinda

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221

na Danson Kaijage, Dodoma

ASKOFU wa Kanisa la PAG, Charles Kanyika, ameikosoa serikali kwa kusema kuwa kuundwa kwa tume ya kuchunguza chanzo cha wanafunzi wa kidato cha nne kushindwa kufaulu mitihani si dawa ya kutatua tatizo la elimu nchini.

Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake juzi, aliongeza kuwa kitendo cha wanafunzi kufeli ni hatua mbaya zaidi kwa serikali na kutengeneza taifa la watu ambao hawajui la kufanya hapo baadaye.

Alisema makosa hayo si ya walimu bali ni ya serikali, kwani imekuwa ikipuuzia maoni ya wadau wa elimu ambao huishauri serikali kwa nia njema ya maendeleo.

Alisema tume zinazoundwa na serikali mara nyingi hazina majibu ya kuridhisha na badala yake hutumia fedha nyingi za walipa kodi bila kupatiwa faida wala majibu ya kina.

Askofu Kanyika alisema kuundwa kwa tume kulikotangzwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hakuwezi kutoa majibu sahihi ya tatizo lililopo.

Akizungumzia masuala ya udini ambao unaonekana kushamili kwa kasi, Askofu Kanyika alisema vuguvugu hizo ni mbegu ya serikali kwani mara kwa mara walikuwa wakieneza chachu ya udini kama sehemu ya propaganda za kisiasa.

source;Tanzaniadaima
 
Mbona siyo huyo tu asikofu aliyeipinga hiyo tume bali hata mimi nimeipinga
 
wakati waislam waliposema kuna tatizo baraza la mitihani walionekana wapenda kulalamika,sasa,tume za nini?mwisho kitaeleweka tu,watu wakiwa hawana cha kufanya,na hawana pakwenda,ndio atapojitokeza mtu kuwatumia hawa waliokosa cha kufanya na pakwenda kwa mambo mabaya,
 
Back
Top Bottom