Askari wawili wafukuzwa jeshi kwa utapeli

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
Kenyela(11).jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Charles Kenyela



Hatimaye Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewafukuza kazi askari wake wawili waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kijeshi, na hivyo kuthibitika ni kweli walikula njama ya kumtapeli mwananchi
mamilioni ya shilingi ili kumuonyesha liliko gari lake lililoibwa.

Mbali na kufukuzwa kazi, jeshi hilo limeagiza pia kufikishwa mahakamani kwa askari hao pamoja na washirika wao watatu ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Askari waliofukuzwa kazi ni Koplo David na Koplo Lufefe.
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Charles Kenyela, alithibitisha kufukuzwa kazi kwa askari hao.

“Tumeshawafukuza kazi na tumeagiza wafikishwe mahakamani,” alisema Kamanda Kenyela alipotakiwa na NIPASHE mwishoni mwa wiki kueleza hatma ya mashtaka ya kijeshi yaliyokuwa yakiwakabili askari hao.
Hata hivyo, Kamanda Kenyela alisema kuwa gari lililoibwa bado halijapatikana na kwamba, polisi wanaendelea kulitafuta.

“Gari halijapatikana. Linatafutwa,” alisema Kamanda Kenyela.
Askari hao walikamatwa Januari 19, mwaka huu, katika eneo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam, wakijiandaa kumtapeli mwananchi huyo fedha hizo.

Januari 16, mwananchi huyo, Jacqueline Komba, alitoa taarifa katika kituo cha polisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuibiwa gari lake hilo.
Jacqueline alidai kabla ya kuibwa, gari hilo aina ya Suzuki Swift lenye namba za usajili T311 BWU alikuwa ameliegesha

karibu na eneo la Swimming Pool, chuoni hapo.
Baada ya kuripoti katika kituo hicho, Januari 18, inadaiwa kuwa Jacqueline alipokea simu kutoka kwa mmoja wa askari polisi akimtaka ampe Sh. milioni 3 ili wamuonyeshe liliko gari lake.

Jacqueline alikubali kuwa angetoa Sh. milioni 2.5, badala ya Sh. milioni 3.
Inadaiwa kuwa askari huyo alimtaka Jacqueline wakutane katika Baa ya Ani, iliyoko Sinza Makaburini, ili wakabidhiane fedha hizo.

Januari 19, inadaiwa Koplo David alimpigia Jacqueline simu kumkumbusha kuhusu suala hilo.
Hali hiyo ilimfanya Jacqueline aamini kuwa gari lake liko mikononi mwa polisi.
Kutokana na hilo, kwa kusaidiwa na polisi wa kituo cha Urafiki, aliweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Februari 7, mwaka huu, Kamanda Kenyela aliliambia NIPASHE ofisini kwake kuwa askari hao walikamatwa na kushtakiwa kijeshi na kwamba, iwapo ingethibitika kuwa walihusika na tuhuma hizo wangechukuliwa hatua.
Alisema mmoja wa maaskari hao ni wa makao makuu ya jeshi la polisi.




CHANZO: NIPASHE
 
Sawa sawa! sio kuwafukuza tu, lazima wajibu pia mashtaka.
What a shame! Askari should be a model of civility! sijui wanajeshi gani hao!
 
Siku hizi maaskari wamekua wabaya kuliko hata majambazi wenyewe.
Huu utaratibu wa kuajiriajiri watu kiholela ndio unasababisha hata wahuni nao waajiriwe na kuwapa mwanya wa kupiga dili zao.
 
Back
Top Bottom