Mapengo 17
R I P
- Mar 28, 2014
- 1,228
- 618
Kama mmegundua tangu wiki mbili zilizopita, siku hizi kila Traffic ana kitabu mkononi mwake katika maeneo mbalimbali jijini Das es Salaam, wamepewa zoezi la kukamata watu wenye makosa barabarani na kila kosa faini ni shilingi elfu thelathini, na kila Traffic lazima arudi na makosa matano kwa siku lasivyo anavuliwa uniform na anarudishwa FFU.
Wekeni vitu vyenu vyote sawa kwenye magari, watajaribu kutafuta kosa la aina yoyote lile ili wakupige faini.
Wekeni vitu vyenu vyote sawa kwenye magari, watajaribu kutafuta kosa la aina yoyote lile ili wakupige faini.
na vitabu vingi walionavyo ni feki,sio vile vinavyotolewa na serikali,hii nimeishuhudia live kama miezi miwili hivi iliyopita.tulikuwa kwenye gari binafsi,kufika njia panda ya segerea tukasimamishwa,ni kweli driver wetu alikuwa na kosa,hakufuata sheria ya njia tatu,.trafiki mdada akakomaa na sisi,tukamwambia tuna jambo la muhimu sana na hatuna hela hapo tulipo,driver aache leseni atupeleke halafu atakuja kulipa faini achuku leseni yake.mdada kakataa katakata anataka hela.tukamwambia twende tukailipe kituoni.akaingia ndani ya gari tukaenda stakishari.yule aliyetuandikia stakabadhi akashangaa kuiona fomu tuliyoandikiwa.akamuuliza yule dada hiyo kaitoa wapi.mdada kimya kainamisha kichwa chini hana cha kujibu.yule kaka katuandikie nyingine,tukakataa,tukamwambia tutalipia kwa ile ile tuliyoandikiwa na mdada,kaka kashindwa kuzima soo.ikatokea bahati nzuri aliingia askari mmoja ambae kuna mmoja kati yetu alikuwa akifahamiana nae.wakatoka pembeni wakateta kidogo,then jamaa katuambia tukubali tu kuandikiwa nyingine then tusepe.tukawa tumeyamaliza kikubwa but bidada hata cjui alitokaje kwenye chumba tulichokuwemo