Kituo hiki ni tatizo kwanza askari wake hawana kauli nzuri. Mfano unaingia tu ni kufokewa kabla hujaeleza shida. Lakini kubwa kuliko ni rushwa ya wazi wazi, wanakamata vijana wa boda boda kisha wanabambikia makosa. Mdogo wangu aliambiwa anatumia bodaboda inayodhaniwa ya wizi. Ajabu akawekwa ndani kwa siku nne mfululizo bila ya kufikishwa mahakamani na tunapoenda kumwekea dhamana na barua ya serikali ya mtaa wanadai tutoe hela, mara anaepeleleza shauri lake hayupo, tumezungushwa kisha tumekwama na kutoa hela ndipo ameachiwa na pikipiki.
Pia kuna tatizo la waharibu mazingira Mto Nyakasangwe ambapo askari hawa hushirikiana na wamiliki wa malori kwa kuchukua rushwa ya 5000 hadi 30000 kutegemea na ukubwa wa gari. Imefikia wakati wananchi wanaolalamika au kuonesha kupinga hili wanarudi nyuma maana rushwa hizi zinachukuliwa hadharani. Tulienda mpaka NEMC ajabu waliwapowashirikisha polisi hawa tu kwenda kuwakamata waharibifu hawa, kwanza waliwapigia simu kuwataarifu waondoe malori lakini pia wakawapitisha njia ambayo si ile wanayopita wenye maroli ili wasikute matokeo yake wakafelisha zoezi.
Matokeo yake mpaka leo mto unazidi kutanuka na kutishia usalama wa makazi ya watu na mafuriko. Waziri Mwigulu Nchemba kwa kuwa ni member humu please mulika kituo hiki. Hata kwa kutumia mbinu zozote kama zile za Mrema enzi zake. Naamini utajua mengi sana yanayoendelea hapa wananchi tunanyanyasika sana badala ya kutuaaidia.
Kuna siku kituko kilitokea walienda huko bondeni ajabu wakachukua rushwa ya Sh 30,000 wakiwa na askari wapya. Mkubwa wao wakagawana isivyo wakagombana na kutaka kupigana kugombea hiyo rushwa. Je hao askari wapya watafanyaje baadae kidogo wakizoea????