Askari Trafiki wa Memorial Moshi, anapokea Rushwa

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
7,681
12,313
Wadau habari zenu?

Kuna trafiki mmoja mweupe na ni kijana,Leo(14/2/17) amekuwepo eneo la eneo Memorial(high way ya Arusha to MOSHI). Huyu trafic amezidi kusimamisha magari na kuyatafutia makosa na akishayapata anataka walipe faini au watoe rushwa,na ameandaa vijana wake hasa wauza magazeti ili wamkusanyie hizo pesa.

Ameshika kitabu cha notifications mkononi kwa ajili ya kuzugia na kutisha watu ili watoe pesa.

Naomba uongozi wa Polisi na wadau wengine mtambue hilo.

Muhanga
 
Wadau habari zenu?
Kuna trafiki mmoja mweupe na ni kijana,Leo(14/2/17) amekuwepo eneo la eneo Memorial(high way ya Arusha to MOSHI)
Huyu trafic amezidi kusimamisha magari na kuyatafutia makosa na akishayapata anataka walipe faini au watoe rushwa,na ameandaa vijana wake hasa wauza magazeti ili wamkusanyie hizo pesa.
Ameshika kitabu cha notifications mkononi kwa ajili ya kuzugia na kutosha watu ili watoe pesa.
Naomba uongozi wa polisi na wadau wengine mtambue hilo.

Muhanga
Weka picha yake mkuu
 
Weka picha yake mkuu
Picha yake sina ila kwa watumiaji wa Barabara hiyo na bosi wa trafiki atakuwa anajua ni ndani alimpangia hapo kwa siku ya leo,maana alikuwa trafiki peke yake(mwanaume) na hakukuwa na trafiki mwingine zaidi yake.
 
Wasiwasi wa nini? Wewe weka chombo chako Safi kama utasumbuliwa.
Hawezi kukubambikia kosa kama umejikamilisha! Na ukiona anakuomba rushwa, nenda nae ukalipe kwenye mamlaka husika
 
Wasiwasi wa nini? Wewe weka chombo chako Safi kama utasumbuliwa.
Hawezi kukubambikia kosa kama umejikamilisha! Na ukiona anakuomba rushwa, nenda nae ukalipe kwenye mamlaka husika
Hakuna chombo kilichokamilika 100%
Na watu wengi tunaona kulipa faini ni pesa nyingine bora umtoe na khaki au msimbazi!
 
Hakuna chombo kikixhokamilika 100%
Na watu wengi tunaona kulipa faini ni pesa nyingine bora umtoe na khaki au msimbazi!
Nawe ni mtuhumiwa! Kwanini utoe rushwa?
Na kwanini useme hakuna chombo kilichokamilika kwa 100% wakati ninyi ndio hamfati sheria?
Hebu sema kosa alilokutosa nalo faini ndio tujue kakuonea au wewe ndio mkwepa sheria
 
Kama faini ni sh 30,000 wewe ukaona ulipe kidogo pasipo sheria, kumbuka wote mtakua mmetenda kosa sawa.

Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni kitu kimoja! Alafu mkuu unapokuja kulalamika sehemu public namna hii, unatakiwa kwanza mlalamikaji uwe msafi
 
Nawe ni mtuhumiwa! Kwanini utoe rushwa?
Na kwanini useme hakuna chombo kilichokamilika kwa 100% wakati ninyi ndio hamfati sheria?
Hebu sema kosa alilokutosa nalo faini ndio tujue kakuonea au wewe ndio mkwepa sheria
Ficha Ujinga wako,nimesema huyo trafiki ni kero kwa madereva wa magari ya abiria na kwenye magari binafsi.
Suala la Mimi kutoa au kutotoa rushwa sio agenda ya Uzi huu.
Ila nimeona wauza magazeti wakikusanya pesa kwa niaba yake!
 
Kwanini hujatoa ripoti kwenye mamlaka husika uje kulalama mitandaoni?

Wewe ndio ufiche ujinga wako
 
Wadau habari zenu?
Kuna trafiki mmoja mweupe na ni kijana,Leo(14/2/17) amekuwepo eneo la eneo Memorial(high way ya Arusha to MOSHI)
Huyu trafic amezidi kusimamisha magari na kuyatafutia makosa na akishayapata anataka walipe faini au watoe rushwa,na ameandaa vijana wake hasa wauza magazeti ili wamkusanyie hizo pesa.
Ameshika kitabu cha notifications mkononi kwa ajili ya kuzugia na kutosha watu ili watoe pesa.
Naomba uongozi wa polisi na wadau wengine mtambue hilo.

Muhanga

MWEUPE ANA MWILI KIDOGO?????????????????
 
Ndio! Ananing'iniza funguo ya gari kwenye ruksi ya suruali.

MPUMBAVU SANA HUYO JAMAA, ALIKUWAGA DEREVA NADHANI WA YULE MAMA TRAFIC BOSS WA MKOA HAPO.

DAWA YAKE KAMA NI MPITAJI UNAJIFANYA UNASIMAMA THEN UNAKANYAGA MAFUTA. HANA MAANA.
 
Back
Top Bottom