Askari trafik no. F 3652 anakula rushwa

Askari trafik no. F 3652 anakula rushwa

Kamanda Mpinga, askari wako wa barabarani (Trafik) mwenye Namba F.3652. Ni mfupi mweupe.

Leo muda mfupi uliopita kanisimamisha nikiwa naendesha gari maeneo ya makutano ya barabara ya shekilango na Morogoro, baada ya kuona sina kosa akanambia nimpe elfu 10,000 niende nikakataa akaamua kuniandikia faini eti side mirror ina cracks.

Labda ni kwa kuwa umekataa kumpa hela ya mboga aliyotumwa kuokota na bosi wake. Mke wa bosi wake alikuwa ameshaweka maji ya ugali jikoni anasubiri hela ya mboga akaambiwa na mumewe subiri kuna askari nimemtuma akaokote hela ya mboga pale Shekilango nitakuletea sasa hivi!
 
Inauma ndani ya nchi yako unapoamua kuripoti uovu unaonekana mjinga. Rushwa imekua jambo la kawaida kiasi kwamba ukilalamika kuombwa rushwa unaonekana mjinga
Hata mimi nimeshangaa sana, humu kuna watu wanamuandama mleta mada, kwa mtindo huu, rushwa haitaisha
 
Ahsante kwa taarifa, kamanda wao wa usalama barabarani wiki mbili zilizopita alitangaza kwa kupitia ktk vyombo vya habari kuwa askari yeyote wa usalama barabara akikuomba hela, mpatie kisha njoo UTOE TAARIFA, So take action.
 
Kati yetu hapa ndani nani hajawahi kutoa au kupokea rushwa ktk huduma yyt? Tusiwe wepesi was kupaza sauti midomoni wakati nafsi zetu zinatusuta
 
Kuna makosa na bahatu mbaya,indicator kutowaka au site mirror kupasuka inaweza kutokea ukiwa safarini so hili linatakiwa karipio siyo notification.askari ana kosa.
 
Wewe acha u bushlawyer krek ni krek tu kama haungekuwa na kosa si ungeenda nae kituoni.

Krek ni kosa hata kama ni kidogo na askari anaingia kwenye ula rushwa baada ya kumwambia atoe mwekundu jamaa akakataa then akaamua kumuandikia kosa
 
Binafsi huwa siwaelewi hawa trafc!!! Inamaana kila kosa ni lazima liwe na faini yake? au makosa mengine yanatakiwa kuwa na karipio? Pia kwa mwendo huu wa baadhi ya wachangiaji rushwa haiwez kwisha kamwe!!! Maana wengi hapa wanatetea rushwa
 
[/COLOR]
Hapo umenena mkuu, sasa hivi hakuna aliye kiongozi mzalendo.

Hasa ukizingatia viongozi wengi wanawekwa madarakani kwa mchango wa kampeni toka kwa wafanyabiashara hivyo hata kama magari yao yatafanya makosa hawachuliwi hatua. Unafikiri kwanini kila siku buses zinapata ajali na kuua maelfu lakini hazikomi kwa kuwa kuwa wana uhakika gari ikipata ajali hata kama ilikuwa mwendokasi wa ajabu watalipwa bima ya gari pamoja na ya abiria ambao wote huwa hawapewi haki yao kutokana na mlolongo mrefu na hakuna utaratibu mzuri wa kusimamia abiria, kamanda wa mkoa mbele ya vyombo vya habari atasema kwa hisia kwamba ajali ni uzembe wa dereva alafu report ya RTO inakuwa tamu ili kumwezesha jamaa alambe bima yake vizuri. Hata enzi za Mwinyi pamoja na upole wake ikitokea ajali serikali inakoroma mfano mzuri ile ya bus la Yarabi Salama kesho yake waziri mkuu Malechela akatema cheche na kutoa agizo mpaka leo hii mabasi yanasafiri mchana ili yawe monitored lakini wazee wa favor siku hizi hawafanyi yao na haikutokea ajali kubwa baada ya miaka 5 ilipotokea ile ya Air Msae. Lakini siku hizi ajali za mabasi kawaida leo wamekufa 16 baada ya wiki 30 baadae miezi 10 na inachukuliwa poa tu
 
Kamanda Mpinga, askari wako wa barabarani (Trafik) mwenye Namba F.3652. Ni mfupi mweupe.

Leo muda mfupi uliopita kanisimamisha nikiwa naendesha gari maeneo ya makutano ya barabara ya shekilango na Morogoro, baada ya kuona sina kosa akanambia nimpe elfu 10,000 niende nikakataa akaamua kuniandikia faini eti side mirror ina cracks.

TAKUKURU na wanaohusika mchunguzeni.

Kuna mmoja nimekutana nae juzi kioo cha mbele cha gari kilikuwa na crack, akataka aniandikie notification nikamwambia sina hela, kama unataka gari lipeleke tu polisi, akadai nimmpe hela nusu aniachie hela nyingine ya fine iliyobaki nitamlipa siku nyingine..
 
wanazingua sana trafiki; wanasema wameagizwa kusanya hela kwa ajili ya kampeni za urais mwakani; ili ccm wapate hela ya kuprint ma-t shirt ana kanga za chagua ccm; ndio maana wapo speed sana; wamewekewa kiwango cha kukusanya kwa siku kila trafiki anatakiwa apeleke jiwe na nusu jioni kwa mabosi zao; kinachozidi hapo kinakuwa cha juu chao...
 
Kamanda Mpinga, askari wako wa barabarani (Trafik) mwenye Namba F.3652. Ni mfupi mweupe.

Leo muda mfupi uliopita kanisimamisha nikiwa naendesha gari maeneo ya makutano ya barabara ya shekilango na Morogoro, baada ya kuona sina kosa akanambia nimpe elfu 10,000 niende nikakataa akaamua kuniandikia faini eti side mirror ina cracks.

TAKUKURU na wanaohusika mchunguzeni.

soja anasema kakuchukilia mchuchu ukatafuta force no zake ili umkaange kwa style hii
 
Siku nyingine ukiwa unaongea na askari rekodi kwenye sim. Bonge la ushahidi! Au ukiweza rekodi video. Ila kumbuka alichofanyiwa Jerry Muro. Wana mtandao hao.
 
Back
Top Bottom