Askari trafik no. F 3652 anakula rushwa

Askari trafik no. F 3652 anakula rushwa

Escoba

Member
Joined
Jan 10, 2013
Posts
75
Reaction score
18
Kamanda Mpinga, askari wako wa barabarani (Trafik) mwenye Namba F.3652. Ni mfupi mweupe.

Leo muda mfupi uliopita kanisimamisha nikiwa naendesha gari maeneo ya makutano ya barabara ya shekilango na Morogoro, baada ya kuona sina kosa akanambia nimpe elfu 10,000 niende nikakataa akaamua kuniandikia faini eti side mirror ina cracks.

TAKUKURU na wanaohusika mchunguzeni.
 
ushahidi si ni faini aloniandikia wakati kosa sina ,,,side mirror ina crack ndogo sana
 
OK. kwani side mirror yako haijakreki..?? maana rushwa yake haiwezi tumika kama utetezi wa makosa yako
 
side mirror kweli imepasuka? na kama imepasuka ni kosa au si kosa ambalo ulistahihi kulipa fine?
 
Kamanda Mpinga askari wako wa barabarani (Trafik) mwenye Namba F.3652. Ni mfupi mweupe. Leo muda mfupi uliopita kanisimamisha nikiwa naendesha gari maeneo ya makutano ya barabara ya shekilango na Morogoro, baada ya kuona sina kosa akanambia nimpe elfu 10,000 niende nikakataa akaamua kuniandikia faini eti side mirror ina cracks. TAKUKURU na wanaohusika mchunguzeni.

Hilo nalo kosa rushwa ya nini?
 
Atakumbukwa sana the Blessed Mwal. J.K Nyerere. Ila yana mwisho hata kama si leo.
 
watu wengne bhana umegundulika unakosa tena hauishi kulalama. Achen kuwapaka matoe wenzenu bhana
 
Sijui kama watakusikiliza hao wakubwa...

Hivi hujui kuwa hao wazee wa favor hutakiwa kupeleka hesabu kwa wakubwa...

Mkuu watu8, hivi hili huwa ni kweli!??

ushahidi si ni faini aloniandikia wakati kosa sina ,,,side mirror ina crack ndogo sana

Mkuu Escoba, endelea hivyo hivyo kuikataa rushwa. Nenda katengeneze side mirror ya gari lako ili siku nyingine asiwe na sababu ya kukuandikia hata notification!

OK. kwani side mirror yako haijakreki..?? maana rushwa yake haiwezi tumika kama utetezi wa makosa yako

Rushwa ni ugonjwa wa taifa. Huenda kweli huyo askari hapo awali alitaka rushwa na baada ya kukataliwa akaamua amtoze faini kwa kosa la crack kwenye kioo. Kosa kama hilo kawaida mtu hupewa onyo.

Mimi niongezee kuwa;

- Ni wajibu wa kila raia kukataa (R) kukataa rushwa - kuomba na kutoa!

- Jitahidi kutengeneza chombo chako cha usafiri na kuendesha kwa usalama wakati wote. Hii ni kwa ajili ya usalama wako na watumiaji wengine wa njia za usafiri

- Hakikisha unafuata sheria (hasa za barabarani) na kuzitii

- Jitahidi kuwa na lugha nzuri unaposimamishwa na askari - you will be shocked matokeo yake yatakavyo kuwa!

- Tusiache kutoa ripoti kwa viongozi wa Polisi pale tunapopewa huduma pungufu na mategemeo/haki yetu.

- Tusiache kuwatia moyo na kutoa ushirikiano kwa Polisi pale tupatapo nafasi/uwezo wa kufanya hivyo.


Wenu x-polisi, Mentor.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom