Africanar
Member
- Jan 20, 2018
- 86
- 24
Habari za muda huu ndugu zanguni mabibi na mabwana(wakuu) humu ndani ya chama, poleni na mihangaiko ya hapa na pale katika kutafuta girisi(by mkulu voice) ili kutatua mkazo huu wa vyuma ambao unatuandama awamu hii.
Kwanza napenda kutoa pole(kama binadamu) kwa kuondokewa kwa bahati mbaya dada yetu(mwanafunzi) wa NIT kwani ni katika mazingira tatanishi sana Mungu aiweke roho yake mahali pema. Pasipo kupoteza muda ndugu zangu baada ya vuguvugu la siku chache zilizopita za uchaguzi na binti kupigwa risasi kuna mambo machache ya kuambizana na kujifikirisha hapa.
Sasa katika hili tatizo lililotokea ni kweli imetokea kiasi kwamba kuna baadhi ya raia wanadai walishuhudia wakati risasi inapenya katika mwili wa mwanafunzi ila tujiulize maswali haya;
1.Je, kuna uthibitisho gani kama askari ndiye aliefyatua risasi maana Kamanda Mambosasa amebainisha kuwa yawezekana ile risasi haikutoka mikononi mwa askari ila watu wasiojulikana ambapo ukiangalia kwa jicho la pili utaona Kamanda anaweza kuwa sahihi maana mashuhuda wote hawakuona kama ilitokea upande wa polisi kwani kulikuwa na vuguvugu na hivyo watu wabaya wakatumia nafasi hiyo.
2.Kama askari ndio waliofyatua risasi je matumizi ya silaha kwa askari yapoje? Kwanini wachunguzwe askari wa chini waliotumia silaha za moto katika hiyo ghasia wakati silaha zinaizinishwa na wakuu wa jeshi la polisi kabla ya kuzitumia(huwaruhusu kutumia) na kuachishwa waachishwe waliotumia?
Ndugu zangu tujaribu kuangalia kiubinadamu haya maswali mawili kuhusiana na haya matukio, yaani uhakika wa aliyepiga risasi na hukumu kwa askari waliotenda ilhali ruhusa ya matumizi ya silaha hutoka juu ambapo wawajibishwaji wangeanzwa na maafisa wa jeshi kwanza.
Niko tayari kukosolewa kwa huu waraka mfupi kuhusiana tukio lililotokea siku chache zilizopita.
[HASHTAG]#Africanar[/HASHTAG]