Askari polis sengerema, apigwa kipigo cha mwizi, Hali yake ni mbaya.

mkuu nimekusoma, umezungumzia uwajibikaji. Ni ukweli kabisa, kuna baadhi ya uhalifu unaendelea ni kwa kuwa tu POLISI nao hawataki kuwajibika kwa nafasi zao. Hilo halina ubishi.

sasa turudi kwenye mada. askari kapigwa akiwa anatekeleza wajibu wake, na amepigwa nusra ya kufa, je hana haki kwa sababu baadhi ya askari wanaendekeza rushwa katika utumishi wao? Je ni kweli anastahili kipigo hicho alichopewa kwa kisingizio polisi wenzake wanakula rushwa?

Na je nini nafasi ya wanaharakati, wanatetea haki za kundi fulani la watu huku makundi mengine wakiyaacha kwa sababu tu watu wa ofisini kwao wananuka kwa utumishi mbovu?
Maaskari Polisi hawahitaji mtu wa kuwatetea. Wana uwezo usio shaka wa kujitetea na kuwachukulia hatua wahalifu kwa misingi ya taratibu na sheria za nchi; fursa mara nyingi wanayoitumia si kwa manufaa ya taifa bali kwa sababu na maslahi yao binafsi. Wanaharakati ni sauti ya wanyonge, wenye kudhulumiwa ambao haki zao zinakanyagwa na mtu au kundi fulani na hawana uwezo wa kujitetea wala wa kuwakemea wanaowadhulumu. Narudia tena, tumesikia hadithi za upande mmoja na hatujasikia upande wa watuhumiwa kuwa ilikuwaje hadi tukio hilo kutokea. Nasisitiza tena; NI VIGUMU KUWAAMINI POLISI WA TANZANIA BILA YA KUPIMA WANACHOELEZA kutokana na tabia yao ya kugeuza ukweli, kutengeneza tuhuma (kubambikia kesi) dhidi ya raia wasio na hatia. Sisi tulioona yaliyotokea Arusha, na walioona yaliyotokea Morogoro, Songea na sehemu kadhaa wanaelewa ninachomaanisha. Hakuna wa kuziamini taarifa za polisi kwa asilimia mia moja siku hizi kabla ya kutafakari anachosimuliwa na polisi wetu hawa labda mwehu. Tunataka kusikia pia upande wa hao raia "walioasi" na kumwadhibu kiasi cha kutishia kuinyofoa roho ya mtumishi wao anayelipwa kwa kodi zao wenyewe.
 
Unaongelea uwajibikaji kwani akina Kamuhanda, Mwema, Jk, n.k n.k wamewajibika kwa makosa yao ya ufisadi na uchizi unaofanywa na Policcm?. Hao wananchi tena walikosea sana kama huyo jamaa hadi sasa hivi yupo hospital................ Siku zote dawa ya kiburi ni jeuri!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom