Askari polis sengerema, apigwa kipigo cha mwizi, Hali yake ni mbaya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari polis sengerema, apigwa kipigo cha mwizi, Hali yake ni mbaya.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ntagunga, Sep 23, 2012.

 1. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  15.09.2012 Akiwa na askari mwenzake na mgambo wawili, walikuwa kazini wakifanya msako maeneo ya KASOMERI SENGEREMA, waliibukia kwenye kundi la watu walikuwa wakiandaa na kunywa pombe ya moshi au GONGO. Waliwakamata walioweza kuwakamata na vitendea kazi vyao tayari kuwapeleka kituo cha polisi.

  Wakati wakienda kituo cha polisi, walizingirwa na wanakijiji, pamoja na kujitambulisha lakini bado hawakusikilizwa. Ndipo walipoamua kujulisha kwa uongozi wao, wakaambiwa wawaachie wapika/wanywa gongo hao.

  Ndipo askari hao bila hiyana, wakawaachia na kutaka kuendelea na safari ya kurudi kituoni. Mara wananchi wakaanza kuwashambulia kwa mawe, fimbo, mapanga na silaha nyingine nyingi za kijadi hali iliyopelekea askari mmoja aliyeajulikana kwa jina moja tu la HAMISI kujeruhiwa vibaya sana maeneo ya kichwani na kukimbizwa hospitalini sengerema walioamua kumwandikia rufaa hadi bungando alipo kwa sasa.

  Bado hali yake si nzuri, na watu 14 wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

  maswali/changamoto
  1. Je, kama askari huyo angekuwa na bunduki, angeshindwa kuitumia ili kujilinda?
  2. Askari akiiumizwa/akiuwawa katika kazi yake, mbona wanaharakati hatuwasikii wakitoa matamko?
  3. Je hii haina maana kuwa wako biassed na kazi zao? wanaegamia upande mmoja wa shilingi? Kimaadili inafaa?
  5. Kwa nini watanzania hatupendi kuwajibika kwa makosa ambayo tumyatenda? Tunafanya uhalifu wenyewe, lakini tukikamatwa tunagoma kukamatwa? Huu uwajibikaji tunaodai kwa viongozi wetu sisi tunao?

  NAWASILISHA.
   
 2. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  uzi huu upo tangu asubuhi, lakina cha kushangaza......... JF nimegundua ninyi ni watu wa namna gani
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  nini tena mkuu? kimsingi hakuna aliyejuu ya sheria, wote tunatakiwa kuitii sheria. Kwa ninavyo jua mimi, watu hao lazima wafunguliwe mashataka stahili na sidhani kama kuna atakayepewa dhamana kwa sasa. watakaa rumande hadi afya ya huyo mpiginaji irejee katika hali yake ya awali. maana unaweza kuwaachia watu halafu mtu akafa, wale jamaa wanaweza kusepa.

  Kuhu wanaharaka, nchi yetu imejaa unafki mkubwa sana. tuliowengi ni wanafiki, tunachokikataa, tunakitetea kwa mgongo mwingine. Wanaharakati hadi sasa hawajalaani kitendo cha wananchi kuzuia afisa wa serikali kuwajibika kwa nafasi yake, lakini ingekuwa ni polisi kwafanyia raia kitu hiyo, akina nkya wangekuwa wamesha peleka mashataka ICC. HUU ni unafiki mkubwa.
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  JF ni ya great thinkers.
  Police wanawaachia majambazi sugu na kudeal na watu ambao au wanahangaika kumake ends meet (wapika gongo) au waliokata tamaa ya maisha (wanywa gongo ambao hata mapolisi ni member), wakati kuna makosa ambayo yana impact kubwa ktk jamii.

  Point nyingine, ni kuwa wananchi wamechoshwa sana na policcm ambayo kazi yake ni kulinda mafisadi; so hiyo ni reaction ya wananchi!
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Na nyie(polisi) mtii sheria bila shuruti...,,Nyie(polisi) hamtendi haki mnanyanyasa maraia sana!!
   
 6. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  au na wewe ni pongo!?
   
 7. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  nakushukuru kwa mawazo yako, kuwa wanaharakati wako biases.
   
 8. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  ha ha ha, niliipenda kazi hiyo lakini nilikimbia baada ya usaili 2010.
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  ila kwa ukweli wa hali ya vijijini askari huwa wanapiga deal sana na hawa wanywa/wapika gongo usikute jamaa walikataa kutoa kitu kidogo ndio maana askali wakawakamata na wananchi kwa kujua chezo zima wakaingilia kati.......THIS IS ALSO POSSIBLE
   
 10. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Afande unachekesha! Umeleta uzi hapa jukwaani na umekaa zaidi ya masaa tisa bila majibu, so ungejiuliza kwanini reaction ya members wa JF imekuwa hivyo! Afande Ntagunga ni busara ukileta uzi jukwaani, post ya kwanza kabisa tegemea reply itoke kwa mtu mwingine siyo wewe mwenyewe.
   
 11. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  https://www.jamiiforums.com/members/patience96.html natamani ningekuwa afande, coz one day ningefundisha namna bora ya kazi za kipolis zinavyotakiwa kufanyika. lakini mimi nimekuja na hoja kuwa iweje askari anapokuwa kazini akifanyiwa kitu kibaya kama kupigwa, wanaharakati hatuwasikii wakilaani? Je polisio ambao lazima nikiri kuwa wana kazi ngumu sana wenyewe hawana roho kama tulizonazo sisi raia?

  Je siku huyu askari akipona halafu waliompiga wakaingia anga zake tena, na kwa bahati mbaya akawa na silaha, tutegemee nini?
   
 12. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  punguza unafiki wewe au umang'enya unakusumbua?? Umeanzisha mada kimandemba sana ndio mana magreat thinker wametulia tuliii??? Polisi bado wana mengi sana ya kujibu na kuwajibika kwa wananchi wa tz na washawafanyia na wanaendelea kuwafanyia unyama mkubwa sana.. Ingekuwa powa sana kama wangemuua kabisa.
   
 13. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  kama naelewa vizuri ni kuwa inaonekana hii gongo si hatari saaaaana kama wanavyoivumisha, bali ni miongoni mwa vinywaji ambovyo kisheria, narudia kisheria tunakatazwa kukitumia, lakini kijamii kinapingana na katazo la kisheria, nina maana sheria ilitungwa kuwafukarisha wagema wazawa, manake nimeshangaa kijiji kizima kimemlia denge polisi ili kumzuia asiibughudhi "village breweries" na kwa maelezo ya thread ni kuwa polisi mkamataji aliambiwa na afande wake, awaachie!!!!

  Sijui kama kuna muunganiko mzuri hapo, uwaachie wahalifu halafu waanze kukupiga, mimi nadhani kipigo ndio kilisitisha ukamataji.
   
 14. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  yeah, nakubaliana na wewe kabisa kuwa wapo askari ambao hutumia mamlaka yao kuwanyanyasa raia. Na mimi nilishawahi kukutana na saga la askari wa namna hiyo pale kitua cha polisi wazo hill, niliwahi kuapa kulipiza kisasi, lakini baadaye nilipojifunza neno la Mungu, niliona ni upuuzi mtupu. Na inawezekana askari huyo na wenzake, walikuwa na kawaida ya kuwageuza wananchi kama ATM, sasa jamaa wamechoka au wanaona badala ya kulindwa, ndo kwanza wanageuzwa ATM.

  Lakini nije kwa wanaharakati, maana ndo msingi wa mada yangu. askari akiumiza mtu akiwa kazini kila mtu atamponda, wenye roho ngumu kama akina Ritz na rejao, katiba mpya ndo huwa wanawaunga mkono kwa hoja hawakuwa na namna ya kufanya isipokuwa kuua au kujeruhi. na wanaharakati na vyombo vya habari vitalisema sana hili.

  Sasa kwa nini anapoumizwa askari kwa uzito ule ule wa kuheshim haki za binadam, kwa nini tusiwasikie wakilaani wananchi kutojichukulia sheria mkononi? mimi naamini askari huyo akipona, ipo siku atalipiza kisasi, na kisasi chake kitakuwa kibaya zaidi kuliko alivyofanyiwa.
   
 15. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  nimekusoma mkuu mawazo yako, lakini unajua athari ya unayoyatamka? ipo siku tutachinjana sisi kwa sisi. na sababu kubwa ni ile kulipiza kisasi. chukulia kwa mfano, askari aliyeshambuliwa siku akipata upenyo wa kulipiza kisasi, hali itakuwaje?
   
 16. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hii ni stori ya upande wako wewe uliyejitanabaisha waziwazi kwamba ni mshabiki wa CCM au mmoja wa mapolisi wa ovyo ovyo tulio nao; bado hatujasikia simulizi za upande mwingine. Sasa unataka tuwahukumu wananchi kwa hadithi yako ya kutungatunga tena ya upande mmoja?
  Hakuna Mtanzania asiyejua kwamba Gongo, bangi na madawa ya kulevya na makosa ya trafiki vimekuwa vyanzo vikubwa vya mapato kwa polisi wanaolipwa chini ya viwango kwa kujipatia fedha kutokana na rushwa. Ni mara ngapi vidhibiti kama gongo, bangi na madawa ya kulevya vimeyeyuka vilipofikishwa mahakamani? Pia hakuna Mtanzania asiyefahamu wahalifu wanaokamatwa na kupelekwa rumande na mahakamani ni wale tu waliokosa uwezo wa kuwahonga polisi wala rushwa waliosheheni katika Jeshi hili, tena wengi wa 'wahalifu' hao wakiwa wamebambikiziwa kesi za kupatikana na hizo bange, madawa ya kulevya ? Laiti tungekuwa na polisi wanaowajibika kikamilifu vijana wetu wangenusurika na janga la madawa ya kulevya yanayosambazwa nchi nzima kwa msaada wa hao hao polisi. Wanaharakati wanafanyia kazi facts - proven beyond reasonable doubts na siyo hizi hadithi zenu za Kalumekenge. Shame on you police officers.
   
 17. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  huu ni udhaifu wa wanaharakati lakini nachojua wananchi hasa wa vijijini ambao wengi wamekata tamaa(na hali ndivyo ilivyo) hawajui hata nini maana ya mwanaharakati wala juhudi zao...yawezekana kabisa hata hawawajui ni akina nani... kinachotakiwa hapa ni polisi na serikali yao kuwaelimisha wananchi mipaka ya haki zao pamoja na kikomo cha sheriana kwa hili serikali HAINA MUDA...utawaona kila siku kweye ma TV tu lakini huwezi kuwasikia wamefika vijijni kwa hawa wanywa gongo......ila wakati wa kampeni wanawafikia
   
 18. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  ninachojua gongo nsi haramu kama tunavyosadikishwa(ukilinganisha na vinywaji na baadhi ya whisk) ila inahitaji uangalifu sana katika maandalizi ili kuncontrol alcohol content, na pia mnywaji inabidi azingatie sana mlo vinhinevyo inamtafuna mpaka maini...ila kuna baadhi ya nchi GONGO NI KINWAJI HALALI KABISA KISHERIA
   
 19. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  USHAWAH
  I KUKAMATWA kwa KOSA LOLOTE? ULIWAJIBIKAJE? TWAMBIE KWANZA HILI NDIPO NMI NIKUPE EXPERIENCE YANGU
   
 20. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Hapa tayari umeshawahukumu wanakijiji!!Unaweza kuta jamaa kazidi kuchukua kitu kidogo kwa hao wapika gongo,ikawa mazoea kiasi kwamba hata wananchi wamewachoka!
  Issue ni kuwa ukimkamata polisi unamshtaki wapi?ukienda huko kwao hawakawii kukugeuzia kibao!
   
Loading...