Kwa jinsi ninavyofahamu mji wa Arusha, yote haya yanayozungumzwa wanaweza wakayafanya na makubwa zaidi kuliko hata watu wa Mikoa ya Mbeya na Mara hasa ukizingatia huu ukurasa aliyoufungua IGP kati ya wananchi na chombo chao.
Isitoshe, wengi wetu humu mmezoea mpaka mmpeweushahidi wa kipolisi tena mikononi ndio muamini. Nasema, kitendo cha kusikia kwamba Mhe Kikwete majuzi katembelea mji huo kwa kificho ili zahama zisimuangukie na kwamba hivi sasa kuna Mkurugenzi wa Wilaya ya Arusha asemekana kuwapigia magoti watu wa Arusha kwamba wafungue vifua vyao na chuki walizonazo, sasa hadi hapo nyinyi bado mnataka nini zaidi??
Jambo zito liko kwenye jiji la Arusha na viunga vyake, endelea kukinga sikio lako kusikia vishindi kwenye ardhi.