Elections 2010 Askari Police Wawili Walichinjwa Kama kuku Arusha!!

inawezekana kweli kwani nani anajua kama Generali Kombe aliuwa kwa bahati mbaya au ilikuwa njama tanzania kama huijui habari zote zaweza kuwa tetesi wakati ni za ukweli
 
Idadi kamili ya watu waliouawa sio watatu bali ni zaidi. Maana yupo mtu mmoja nae nasikia aliuawa kwenye maandamano hayo na kupelekwa kuzikwa kwao Moshi kijiji cha Mijongweni. Lakini taarifa haijasemwa. Tuendelee kusubiri mambo yaafumuka tu.
 
Na mimi kuna taarifa nilizipata kuwa askari polisi waliwaua kama mbwa koko wa mitaani wakereketwa wa CDM kama tisa hivi, tena ilikuwa kama mazoezi ya shabaha maana jamaa hawakuwa na njia ya kujitetea? watu arusha tuhabarisheni.
 
Kwa jinsi ninavyofahamu mji wa Arusha, yote haya yanayozungumzwa wanaweza wakayafanya na makubwa zaidi kuliko hata watu wa Mikoa ya Mbeya na Mara hasa ukizingatia huu ukurasa aliyoufungua IGP kati ya wananchi na chombo chao.

Isitoshe, wengi wetu humu mmezoea mpaka mmpeweushahidi wa kipolisi tena mikononi ndio muamini. Nasema, kitendo cha kusikia kwamba Mhe Kikwete majuzi katembelea mji huo kwa kificho ili zahama zisimuangukie na kwamba hivi sasa kuna Mkurugenzi wa Wilaya ya Arusha asemekana kuwapigia magoti watu wa Arusha kwamba wafungue vifua vyao na chuki walizonazo, sasa hadi hapo nyinyi bado mnataka nini zaidi??

Jambo zito liko kwenye jiji la Arusha na viunga vyake, endelea kukinga sikio lako kusikia vishindi kwenye ardhi.
 
Mimi sidhani kama ni kweli! Kama ingelikuwa ni kweli Askari wameuwawa, si ndio wangepata sababu tosha na ushaihidi dhidi ya Chadema???!!!!

Hii 'point' inamaliza hoja nzima ya post hii...kubali usikubali, kwa akili ya kawaida tu...kweli ingetokea hivyo ilikuwa ni hoja nzuri mno kwa polisi kutaka kuionesha jamii ya nyumbani na kimataifa kuwa CHADEMA walikuwa na dhamira mbaya
 
Lisemwalo lipo, kama halipo..... IGP jiandae next incidence utaona experience uliotupa mtaani. Endeleeni kutufunza jinsi ya kudeal na polisi.
 
Mimi sidhani kama ni kweli! Kama ingelikuwa ni kweli Askari wameuwawa, si ndio wangepata sababu tosha na ushaihidi dhidi ya Chadema???!!!!
keren umesema kweli kama angeuawa askari ndipo wangepata sababu kuu yakupakazia ktk media kua wafuasi wa chadema waliua polisi napolisi ktk kujihami nao wakalazimika kuua,ikumbukwe hata kule wete pemba alichinjwa askari kama kuku,ndipo kina mahita walipopata kuhalalisha uharamia wao,wakat polisi ndio walianza kuua watu kama kuku.
 
ahahaaaaa mabo mengine bana. Tukijadili kila msiba hapa hatutafika. Ikiwa kama anayekufa arusha ni sababu ya CDM ba CCM, tutakuwa watu wa ajabu kwani kabla ya conflict ya tarehe 5.1.2010 watu walikuwa hawafi? ahahahaha
 
Habari zilizopo ni askari mmoja alimpiga risasi raia na yeye kuchomwa na kitu chenye ncha kali na alikufa.Alizikwa 6 jan
 
nimesikia askari police wawili walichinjwa kama kuku arusha!! Hivi tanzania tumefikia hapa?
Serikali imeamrisha vyombo rasmi vya habari kutozungumzia jambo hili,je hii siyo kuingilia uhuru wa vyombo vya habari?
Waliopo arusha jambo hili lilitokea?:shut-mouth:

si kweli ni uzushi tu hakuna kitu kama hicho. Askari wanapeta tu na mkuu wa andengenya na kiboko ya chadema ocd town zubari
 
Imagine kama Polisi watangaze kuwa wameuliwa Askari wawili Arusha.hii ingewapa Confidence wakazi wa Mbeya,Mwanza etc kuona Kha! kumbe hili linawezekana,hapo unadhani nini kingefuata?
e.g walipokuwa wakitangaza matokeo ya uchaguzi wa kila jimbo ,mwisho wakagundua kuwa wananchi wanaenda na kukesha ktk vituo vya kuhesabu kura,Amri ikatolewa matokeo yatangazwe from Makao makuu tu.na waandishi wote wa habari wakawekwa ktk kumbi moja.
And what happened to Mh.Tido wa TBC......read between the dots/lines ktk vyombo vya habari
 
Saa zngine mtu unatamani kucheka... Ni msiba mkubwa unaosikitisha! Na kwa njia hii tunatarajia kwenda tunakotaka kwenda?!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom