Askari Magereza wanne kortini kwa kuua mfungwa

Askari Magereza wanne kortini kwa kuua mfungwa

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
28th December 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Askari wanne wa Gereza la Lilungu lililopo mkoani hapa, wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji ya mfungwa.
Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara jana na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Abdulhaman Mohamed mbele ya Hakimu Stepheni Mbungu.
Wakili Mohamed alidai kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kumuua mfungwa huyo namba 215, Kasimu Kumchaya. , Oktoba 31, mwaka huu katika gereza hilo.
Wakili huyo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari mwenye namba B 5147 WDR Swalehe, askari mwenye Namba A 854 Sajenti Mohamed, askari namba 4264 Sajenti Jason maarufu kwa jina la Machozi na askari mwenye namba A 5294
Sajenti Shaibu.
Watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji hadi watakapofikishwa Mahakama Kuu baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
Hakimu Mbungu aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 5, mwakani itakapotajwa tena na kuamuru watuhumiwa hao kurudishwa rumande kutokana na kesi za mauaji kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.
CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom