Askari huyu wa Korogwe Tanga kuna siku atasababisha ajali au yeye kufariki

Raia mtiifu

Member
Apr 26, 2019
17
53
Kuna baadhi ya mambo yanafanyika mpaka inafikia hatua ya kuanza kujiuliza huyu mtu alikuwa na maana ipi.

Leo nikiwa safarini natokea Arusha na basi ya kampuni ya Harambee,baada ya kupita Korogwe mjini kilometa chache mbele kuna kona ambapo majira ya jioni/usiku panakuwa na askari ambao hutimiza majukumu yao ya kila siku.

Kilichonifanya niandike andiko hili ni kitendo cha askari mmojawapo kati ya waliokuwa pale barabarani kusimama katikati ya barabara akiwa na tochi yenye mwanga mkali na kuelekezea kwenye kioo cha mbele cha dereva(tena akimlenga yeye).

Nilikuwa nimekaa mbele na kushuhudia dereva wa basi lile akihangaika kutafuta nini cha kufanya huku akiyumba na hatimae kufanikiwa kusimama pembeni.Kiukweli abiria tulioshuhudia tukio lile tulipatwa na butwaa huku hasira zikitawala na kuanza kumfokea yule askari na kwa aibu alijiondokea na kukaa pembeni na tochi yake.Hatukuweza kutambua sura yake wala namba yake kwa kuwa hatukushuka kwenye gari na ilikuwa giza limeshaingia.

Tunaomba vyombo vinavyohusika kuchunguza askari hawa hasa wanaosimama barabarani usiku maana inawezekana hawana utaalamu wa kazi hiyo.

Nawasilisha!
 
Acha kiherehere wewe. Kulikuwa na haja gani ya kuja kunichongea humu? Tunawasaidia nyinyi abiria msafiri kwa usalama halafu unanichongea. Ajali ngapi tumezuia kwa hili zoezi la tochi? Mbona nyie hamna shukran? Basi lenyewe Harambee. Kammmmonnn!
 
Ipo siku litamkuta jambo huyo askari!!

Kuna wenzake miaka ya nyuma,walikuwa wanafukuzia basi wakakimbiza kigari chao spidi wakalipita lile basi halafu kwa mbele wakablock barabara kwa kutumia kigari chao,weee mwenye basi hakusimama akapita nacho kile kigari askari wote hawakuomba maji palepale wakalala yoooo!
 
Mlishindwa kushuka na mkamkandamiza makofi?
 
Siku nyingine, achana na harambee! Panda ktk vyuma vya uhakika, Kidia, Esther, Extra. Achana na Harambee.
 
Hapo ndipo mlipokwama abiria wenzangu! Kwani mlizuiwa na vitu vizito kiasi gani cha kushindwa kushuka?

Huyo mshenzi ilibidi mumlambe makofi mawili mawili halafu hata kama gari ina makosa ilibidi mumshike yeye faini atoe na samahani za kutosha

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Acha kiherehere wewe. Kulikuwa na haja gani ya kuja kunichongea humu? Tunawasaidia nyinyi abiria msafiri kwa usalama halafu unanichongea. Ajali ngapi tumezuia kwa hili zoezi la tochi? Mbona nyie hamna shukran? Basi lenyewe Harambee. Kammmmonnn!
Ndo ummulike dereva machoni Mkuu? Ningekuwa humo ungetii Shuruti aisee!
 
Acha kiherehere wewe. Kulikuwa na haja gani ya kuja kunichongea humu? Tunawasaidia nyinyi abiria msafiri kwa usalama halafu unanichongea. Ajali ngapi tumezuia kwa hili zoezi la tochi? Mbona nyie hamna shukran? Basi lenyewe Harambee. Kammmmonnn!
Hii ndio faida ya kutokuelewa kilichoandikwa!Tochi gani unayozungumzia wewe afande!
"Usipoelewa swali tu kwenye mtihani ndio mwanzo wa kufeli"
 
Siku nyingine, achana na harambee! Panda ktk vyuma vya uhakika, Kidia, Esther, Extra. Achana na Harambee.
Ukiona mtu kapanda basi za aina hii ujue kuna sababu mkuu...sio lazima yote kuyaandika hapa.Hoja hapa ni huyo askari maana hata kama ingekuwa ni moja kati ya hayo mabasi uliyotaja bado isingetosha yeye kufanya kitendo alichofanya.

Na inawezekana wengine hawajaelewa tochi ninayoizungumzia(sio ile ya kuzuia mwendokasi) ni tochi ya kawaida(kurunzi) tena yenye mwanga mkali.Najua wanapaswa kutumia vile vifaa vyao vinavyotoa mwanga wa kijani na nyekundu(reflector).
 
Kuna siku nililipanda Hilo Basi. Arusha yenyewe tumetoka saa tatu likiwa na abiria kumbe nusu wanashuka Moshi.
Gari ilianza kutafuta abiria Moshi ili kujazia nafasi zilizo wazi. Abiria wanaoingia Ni wale waliochoka wenye TECNO za tochi, wamasai, wamakonde na wapare wachache. Gari mwendo halina humo ndani Ni milio ya TECNO na Aitel. Kila anayeongea na simu anaongea utafikiri anahubiri. Kifupi Harambee is a shithole bus.
 
Hi nikweli kabisa mimi pia ilinitokea kutoka Moshi kuelekea Arusha baada ya kuvuka daraja la kikavu kabla ya kufika kwasadala tulifanyiwa huo uhuni, almanunsura tupate ajali mbaya sana kilichosaidia hatukua mwendo mkali
 
Kuna baadhi ya mambo yanafanyika mpaka inafikia hatua ya kuanza kujiuliza huyu mtu alikuwa na maana ipi.

Leo nikiwa safarini natokea Arusha na basi ya kampuni ya Harambee,baada ya kupita Korogwe mjini kilometa chache mbele kuna kona ambapo majira ya jioni/usiku panakuwa na askari ambao hutimiza majukumu yao ya kila siku.

Kilichonifanya niandike andiko hili ni kitendo cha askari mmojawapo kati ya waliokuwa pale barabarani kusimama katikati ya barabara akiwa na tochi yenye mwanga mkali na kuelekezea kwenye kioo cha mbele cha dereva(tena akimlenga yeye).

Nilikuwa nimekaa mbele na kushuhudia dereva wa basi lile akihangaika kutafuta nini cha kufanya huku akiyumba na hatimae kufanikiwa kusimama pembeni.Kiukweli abiria tulioshuhudia tukio lile tulipatwa na butwaa huku hasira zikitawala na kuanza kumfokea yule askari na kwa aibu alijiondokea na kukaa pembeni na tochi yake.Hatukuweza kutambua sura yake wala namba yake kwa kuwa hatukushuka kwenye gari na ilikuwa giza limeshaingia.

Tunaomba vyombo vinavyohusika kuchunguza askari hawa hasa wanaosimama barabarani usiku maana inawezekana hawana utaalamu wa kazi hiyo.

Nawasilisha!
Mkuu ulibeba mswaki na dawa ya Meno?? Harambee duh mlifika lini?
 
Kuna siku nililipanda Hilo Basi. Arusha yenyewe tumetoka saa tatu likiwa na abiria kumbe nusu wanashuka Moshi.
Gari ilianza kutafuta abiria Moshi ili kujazia nafasi zilizo wazi. Abiria wanaoingia Ni wale waliochoka wenye TECNO za tochi, wamasai, wamakonde na wapare wachache. Gari mwendo halina humo ndani Ni milio ya TECNO na Aitel. Kila anayeongea na simu anaongea utafikiri anahubiri. Kifupi Harambee is a shithole bus.
Ila kiukweli mkuu unadharau sana
 
Ipo siku litamkuta jambo huyo askari!!

Kuna wenzake miaka ya nyuma,walikuwa wanafukuzia basi wakakimbiza kigari chao spidi wakalipita lile basi halafu kwa mbele wakablock barabara kwa kutumia kigari chao,weee mwenye basi hakusimama akapita nacho kile kigari askari wote hawakuomba maji palepale wakalala yoooo!
Mwaka gani na wapi?
 
Back
Top Bottom