Ni kosa kubwa sana kiimani kutumia maneno ya Mungu, manabii na mitume kama vibwagizo.
Maneno ya Mtume Paul:
"Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.
Mtume Paulo aliyasema hayo akiwa gerezani kwaajili ya kuihubiri injili ya Kristo.
Paulo aliyasema hayo akijua kuwa anakaribia kuuawa, baada ya kukataa kuacha kuihubiri injili. Alikubali kufa kuliko kuikana imani yake.
Haya maneno siyo ya kutamka kwa kila mtu, bali ni kwa wale walioamua kuyaishi mafundisho ya Kristo kikamilifu. Paulo aliyatamka maneno hayo yeye mwenyewe kabla hajauawa, hayakutamkwa na watu wengine baada ya yeye kufa.
Kwa huyu, ambaye hatuyajui maisha yake yalikuwaje, yatosha tu kueapa pole wafiwa, na kumwomva Mungu ampokee kwenye makao ya milele na amjalie pumziko jema kama katika maisha aliamini uwepo wa Mungu, na alijitahidi kuyaishi mafundisho ya Kristo mwokozi wetu.